Kuna mdau ameni PM kuhusu ni gari gani achague kati ya Subaru Forester na Nadia. So I thought I would share it with all of you and get more input from the entire community.
Subaru Forester ni gari ngumu, kama ilivyo RAV 4 (Engine 3S-FE model 1994 - 2000, 1997 - 2003 RAV4 EV). Spare zake kwa wastani zipo juu, zaidi hata ya RAV4.
Kwa kifupi, Subaru Forester ina compete na RAV4, na zote zimetolewa almost at the same time.
Subaru Forester ina engine kubwa, 2500cc (RAV4 2000cc), hivyo lazima ujiandae kuweka mafuta ya kutosha, ukizingatia na foleni zetu za bongo.
Engine kubwa ni nzuri kwa safari, au kama una mizunguko ambayo hakuna foleni. Kama kula foleni, injini kubwa itakula mafuta mengi zaidi ya engine ndogo. Unapochagua ukubwa wa engine, zingatia matumizi na uwezo wako kiuchumi.
Kwa kifupi, kwa mtu wa kipato cha chini anaeanza maisha, Subaru Forester si gari ya kununua period.
Toyota Nadia.
Nadia inatumia engine ya D4, na hii ni pamoja na RAV4 (Engine 1AZ 2000 - 2005) na gari nyinginezo.
Kwa kifupi, D4 engine ni technologia mpya, mafundi bongo hakuna.
In short, KAA MBALI na D4 engine.
Soma hizi links:
Toyota Nadia with a D4 engine - AA New Zealand
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/49023-mtaalam-wa-engine-za-d4.html
Bottom line:
Kama unaanza maisha, kati ya Subaru Forester na Nadia hakuna la kununua hapo.
Kama una budget ya kutosha na uchumi mzuri, Forester in not a money wester.
You are welcome,
Ramthods