Ushauri: TCU kutowatambua waliosoma Engineering Science kusoma shahada za Sayansi inawaumiza waliosoma Shule za Ufundi

Waliosoma Moshi Tech evening program wanaumia mtaani maana hawatambuliki na TCU.
 
Sidhani kama Tcuhawaitambui Engineering Science, Vyuoni kuna ujanja mwingi wa nafasi ukiangalia TCU guideline ya 2020/21 wameandika Engineering/Physics
 
Hebu nielewesheni vizuri. Kuna masomo ya engineering science bila ya physics???? Hiyo inakuwaje? Mimi ukitaja neno engineering tu natarajia uwe gwiji wa physics na chemistry na math.
Shule za tech huwa wanaopt bios na chem na phys..na huwa Wana SoMo lao la engineering. Sijajua Nini kinazingua mbaka wasichaguliwe degree hata Kama ni diploma holder, Ila tuende mbele turudi nyuma hao jamaa ni wepesi Sana Yan,.....Kuna jamaa alifanya msala shule moja ya tech Waka msuspend kwa muda, akaja skull kwet nikawa nikicheki danta zake daah wanakula Bata Sana, yaan ukichukua Engineering na phys ukilinganisha wao ni very kitonga Yan,,,, kwa tathmin ya haraka haraka phys ni ngumu Mara tat au Zaid ya engineering, may be ni kigezo, sema advantage yao wanapga vipractical Ving japo magumash tu nao, Ila ni wepes Sana achen mzaha na afya zetu ,,target yangu so kuelekeza jinsi gan hawafai, Bali kuwaeleza kuwa masomo Kama physics na math hayajawa magumu kutukomoa lahasha ni kwasabab yanasolve problems direct pia mtu akisoma masomo magumu ni rahs ku generate concepts for the new problems, pia Kama mtu atafanyia hesabu ngumu na ndefu bila kukosea za kifizikia pia tuna uhakika anauwezo wa kufanya vitu vinavohtaji umakini mkubwa bila kukosea katika field husika ...but yote Tisa kumi kwann TCU wasiwaruhusu washikaji kupenya Kama wanamatokeo mazuri diploma .. Ila engineering wepes sana
 
Hizi taarifa za TCU kuwakataa waliosoma engineering science umezithibitisha?

Shule za tech huwa wana opt kati ya Biology au Geography. Physics hawasomi isipokuwa Eng. science. Chemistry ni must.

Na engineering science haina(ga) practical 'kiivo'. Unapewa concept then calculations zinafuata kwa sana tu. Na sjui unapowaita hawa jamaa wepesi umemaanisha nini.
 
Namaansha ukilinganisha na mbadala wake physics
 
Namaansha ukilinganisha na mbadala wake physics
Kwa wepesi au ugumu nadhani hakuna mpishano mkubwa hicho, isipokuwa contents.
Kuna baadhi ya topic huzikuti kwenye Eng. Science ila zipo kwenye Physics, na kuna zingine zipo kwenye Eng Science hazipo kwenye Physics.
 
Hauko serious na elimu yani unalinganisha ubabe wa Eng Science na Physics?

Ngoja nikwambie, lets say ukichukua paper la form two la Eng Science ukawapa form four Physics walifanya watalia na kusaga meno. Ukichukua paper la Physics form 3 ukawapa form 2 Eng Science watachekelea ingawa hawa wote wanatofautiana mitaala.

Nimesoma Physics nikaenda A level shule ambayo wanasoma Eng Sci nina hakika na ninachoongea. Imagine kuna maswali ya Advance walikuwa wanajibu
 
Wewe sasa ndio unajua Science subjects. Huyo jamaa hayuko sahihi, Technical schools wanaopt Biology au Geography na hawana History.

Ukitaka kujua tafuta matokeo ya Tech yoyote uone A za Maths na Chemistry zilivyozagaa afu tafuta za Eng Sc unakuta chache. Ukutane na hizo Electrical Drawing, Plumbing, Architecture, etc ulinganishe na Literature?
 
Nakumbuka projectile and angular motion lazima uziguse kwenye Eng. Science.
 
Mechanical drafting, architectural drafting. Electronic and electrical engineering watu wamekimbizana nazo sana Olevel.
 
Sio kweli. Advance wanaenda vizuri tu..labda kama hiyo sheria imeanza mwaka huu
Ni kweli advance wanaenda kama pcm,pcb ila shida ipo kwa wale ambao baada ya form 4 wakaenda diploma ya afya akija kuomba degree anapata changamoto
 
Acha uongo TO Form six 2013 Olevel alimalizia Bwiru Tech. Ukilaza wa mtu mmj usitoe conclusion ya watu wote, tofauti ya Engineering Science na Physics ni Practical kwa physics ila topic zote za physics zipo kwenye Engineering Science na nyongeza chache ya vijisehemu kwa physics ya Advance
 
Mimi nimesoma Tech Projectile motion, Angular Velocity yote yamo olevel changamoto tu ni kutokufny practical sijui nani alipitisha huo upuuzi
 
TCU waache mambo yao tunawaomba wawape vijana wetu nafasi waendelee na masomo ya juu.
 
Mkuu tathmini yako ya wepes ama ugumu wa engineering science sio sawa sijui umezingatia nn kutoa majibu yako. Ila kiukweli kama ww sio mtu makin kwenye somo kutaga ni kugusa tu.
 
Mkuu engineering science sio sawa na physics ndo maana iko hivyo( engineering science ni subset ya physics)
 
Duh wewe hujui kitu kuhusiana na Engineering science.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…