Ushauri: Tuache kukosoa stori kwa kusema "chai"

Ushauri: Tuache kukosoa stori kwa kusema "chai"

Elias K

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2021
Posts
213
Reaction score
607
Kama unaona stori ni ya uongo na hujatozwa hela kwanini umkatishe msimuliaji tamaa?! Sisi wengine tunanufaika na simulizi za humu kwani zinatupunguzia stress.

Sasa unakuta stori ni nzuri sana na ungependa kusoma muendelezo wake, wanaibuka watu wa kumkatisha tamaa msimuliaji kwa kumuambia "unatupiga kamba" au "chai ya leo balaa" wengine wanaenda mbali zaidi na kiandika lugha mbaya! Au mods niwafundishe kazi?!

Hujaombwa hela ya bundle, kwanza humfahamu mleta story wala hujamnunulia hiyo device anayotumia kuandalia simulizi lakini unaibuka na kumkatisha tamaa!

Aisee wenye tabia hizi acheni mambo yenu ya ajabu
 
Back
Top Bottom