Kiswahili kinakuwa sana na Tanzania tunapata heshima sana kwa lugha yetu hii. Hii naina maana tusifundishe watoto wetu kiingereza-English kuanzia darasa la kwanza. Inasikitisha sana viongozi wetu wana aminisha kwamba hakuna umuhimu wa kujua kufundisha English kwa elimu ya msingi wakati watoto wao karibu wote wanasoma shule ambazo zinafundisha kiingereza kuanzia msingi!. Hili swala halitakiwi kuwa na watu wenye uwezo na hali ya juu pekee.
Mimi sipendi sana kuongea vitu kwa hisia nitatoa mfano wa ukweli kwa familia yetu. Mtoto wa Kaka yangu amesoma Tanzania English media kuanzia darasa la kwanza amekuja huku akiwa na miaka 18 na kujiunga na community college kwa miaka miwili na baadae akaenda kumaliza degree ya Accounting Mississipi. Mwaka jana akiwa na miaka 22 kabla hajafika miaka 23 tayari kapata kazi, kampuni imempa visa maalumu ya miaka mitatu ya wafanyakazi HB1 visa, na analipwa dollar $65,000 kwa mwaka ambayo ni Tsh 152,490,003. Huyu mtoto ameweza kushindana na wenzake kupata kazi kwasababu ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kujua kiingereza vizuri. Nasema hivi si kwa kujigamba bali kuonyesha hili sio swala la watu fulani linawezakana kwa kila mtoto kupata elimu ya hivi.
Tanzania tunaenda kwenye kushindana kampuni nyingi za teknologia mfano zinaenda kuwekeza Kenya kwasabbu ya mfumo wa elimu yao wakati Tanzania tumepata uwekezaji usiozidi $200M wenzetu Kenya wamepata uwekezaji zaidi ya $2B kwenye teknologia kuanzia microsoft, google na kampuni nyingine kubwa. Tofauti ni English tu na ukiangalia wanafunzi wetu wanaosoma english media wakienda Kenya au kuja nchi kama USA wana uwezo sawa au hata zaidi ya wale wa Kenya.
Nashauri tusiweke mazingira ya uongo ya kuaminisha wananchi kwamba tukifundisha watoto wetu english kuanzia darasa la kwanza ni kutokuwa wazalendo wakati viongozi wetu wanasomesha watoto wao english media. Kama tunatatizo la walimu basi tulitatue ikiwa na pamoja na kubadilishana walimu na kenya na uganda kwa sisi tuwapeleke kwa muda walimu wa kiswahili kwao na wao watupe walimu wa english
Tukishinda hapa kupigana madongo ukweli ni kwamba watoto wa masikini tu ndiyo wanakosa nafasi. Kuweni makini sana na mashabiki.