Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Usijali jipe moyo, wewe omba uzima. Hata JF kuna dada mmoja alimalisa chuo hakusubiri ajira akauza uji mtaani kwa raha zake. Mwisho wa siku ana pesa nzuri japo watu wanamcheka. Hivyo usichague kazi ila angalia mahesabu jioni
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
Pole sana ndugu Yangu.
Maneno yako yameugusa moyo wangu.
Wakati nilipomaliza shule, nilikaa Kitaa, hadi nikaona kusoma hakuna faida. Nilishindwa maisha na rafiki zangu bodaboda, nikajiuliza maswali bila majibu japo sikuwa njaa sana ila nilijiona vibaya mno.

Kwa sasa, niko vizuri kiasi changu. Huwa nikijitathmini na kucheck nilipofikia, napiga magoti na kumshukuru huyu Yesu Kristo tunayemuabudu.

Usikate tamaa ndugu Yangu, Mungu hajakusahau. Ipo siku yako tu.
 
Pole sana ndugu Yangu.
Maneno yako yameugusa moyo wangu.
Wakati nilipomaliza shule, nilikaa Kitaa, hadi nikaona kusoma hakuna faida. Nilishindwa maisha na rafiki zangu bodaboda, nikajiuliza maswali bila majibu japo sikuwa njaa sana ila nilijiona vibaya mno.

Kwa sasa, niko vizuri kiasi changu. Huwa nikijitathmini na kucheck nilipofikia, napiga magoti na kumshukuru huyu Yesu Kristo tunayemuabudu.

Usikate tamaa ndugu Yangu, Mungu hajakusahau. Ipo siku yako tu.
Asante mkuu kwa kunitia moyo,be blessed chief
 
Nahisi shida yako ni malengo na mtazamo wako wakimaisha mjomba.

1. Ulivo kuwa unasoma ulisoma kwa malengo yapi??...Je ulijitahidi kwa nguvu zako zote kuwa mmoja wa wanafunzi bora darasani kwako?? Ulijenga urafiki na wanafunzi wenzako na waalimu wako??

2. Je..hapo kwenye kazi yako ya sasa unafanya kwa malengo yapi? Unajitahidi kwa mfanyakazi bora au unaweka jitihada zozote za ziada kuwazidi wenzako?? Je wewe ni kwanza kufika, wa mwisho kutoka?? Unafanya kazi hata wikiendi au sikukuu ukihitajika?? Mahusiano yako na wenzako na boss yakoje?? Unatambua thamani yako kama mfanyakazi?? Je, mwajiri wako akitaka kufukuza watu kazini...je atakufukuza kirahisi au wewe ni mtu tegemeo sana kwake??

3. Kama umejiajiri, unafungua ofisi yako au biashara yako saa ngapi?? Na je unafunga saa ngapi?? Ubora wa huduma yako kuwazidi wengine ukoje?? Je ni mcheshi, mchangamfu na mtu wa watu.... au ni mtu mwenye stress na mawazo mda wote? Je unawapa wateja wako sababu yakuja kwako na wasiende kwa wengine??

4. Kwenye kila hatua ya maisha..jiulize unataka kufanikisha nini....na nini unachokifanya cha ziada kuwazidi wengine kufanikisha malengo yako. Wasomi ni wengi, uwe msomi bora.....wafanyakazi ni wengi uwe mfanyakazi bora......mamantilie ni wengi uwe mamantilie bora......machinga ni wengi uwe machinga bora....n.k..........FANYA KITU CHA ZIADA KILA SIKU UJE UTUPE MREJESHO BAADA YA MWAKA.
Madini haya
 
vitabu vichache nilivyo pitia vinasema kuwa kwa wengi wanao fanikiwa huwa wana miaka 40 mpaka 60! ndo kipindi cha mafanikio hicho, ni nadra sana kupata utajiri na kuuendeleza ukiwa na umri chini ya huo. weka malengo na kuyasimamia vizuri.
 
Duh! Inauma sana na mwaka mpya ndio huo inamaana age inazid kwenda.. usikate tamaa mpaka tamaa ikatike yenyewe
 
Duh mkuu umenena hauko mwenyewe brother elimu hii Mimi najuta kabisa kufika chuo sina hamu,nawazaga hadi nachoka heri hata wew unamishe broo na mtoto,mim sinahata mtoto kila shughuli inakufa achatuu,mungu atukumbuke sasa nimechoka sana,inafika mahali unasaka channel ukaoshe vyombo uarabuni,
 
Elimu ya Bongo haina shida,shida ni kupenda kuajiriwa,Tumia elimu yako kuanza kujiajiri. Kama elimu ya Bongo ina shida hakuna mwajiri angependa kuwaajiri wa bongo.
 
Material Possessions Drives people Crazy while its nothing to worry about at all! Jambo la msingi kwenye maisha ya binadamu ni kuweza kuingiza kipato kila siku kinachokuwezesha kusukuma siku..Umiliki wa mali na vitu sio jambo la msingi kama wengi tunavyoamini. Wengi tumegeuka kuwa watumwa wa vitu.
 
Yaan mkuu una akil sna , hakika halio ndo hali halisi haswa

Nina kaka angu yupo uk hapa bongo ana majumba hayana idadi
Ma eka ya mashamba had mengine hayajui

Ila kumseidia mtu shida yaan kukupa kamtaj hawez labda sh 10000 ili sku yapili umuombe tena aone huwezi ishi bila yeye nikaona. Bora nijiongeze saiv sina habar nae kabisa japo km ni kaka baba mmoja ma mmoja ila sina mawasiliano nae tena nafanya yangu

Jaman chonde chonde msitegemee vya ndugu mtakufa masikini
Usiwalaumu watu wa hivyo mkuu anatamani sana kuwasaidia ndugu zake, ila hizo pesa hana mamlaka nazo
 
We siyo graduated ni graditude huwezi kuwa zoba kwa kiasi hicho nikimuona MTU ana degree halafu analalamika ajira natamani nimtemee mate huna Tina kwa taiga hili kabisa .si ajabu umeacha mashamba kijijini nawe IPO mjini unabanana na washua wakati umeacha Mali ,Mimi na degree ya HRM nibahatika kufanya field wilaya flani hadi Leo nafanya shughuri zangu kwenye wilaya hiyo na sina mpango wa kuajiliwa kabisa .
Wewe sio mjanja, ni bonge la mjinga hata kama unafanya shughuli zako
 
Usiseme huna unachomiliki wakati una kende komavu kabisa. Hicho ni kiwanda!!!
 
Acha Mbwebwe huwezi kufanikiwa ukiwa na Mbwebwe utaki ajiriwa unajua adhaa ya kuajiliwa na kujiajili au Unasikia tu, sasa badilika ukiwa na Kitu mkononi ndio uanze hizo Mbwebwe
 
Back
Top Bottom