Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Usijali jipe moyo, wewe omba uzima. Hata JF kuna dada mmoja alimalisa chuo hakusubiri ajira akauza uji mtaani kwa raha zake. Mwisho wa siku ana pesa nzuri japo watu wanamcheka. Hivyo usichague kazi ila angalia mahesabu jioni
 
Pole sana ndugu Yangu.
Maneno yako yameugusa moyo wangu.
Wakati nilipomaliza shule, nilikaa Kitaa, hadi nikaona kusoma hakuna faida. Nilishindwa maisha na rafiki zangu bodaboda, nikajiuliza maswali bila majibu japo sikuwa njaa sana ila nilijiona vibaya mno.

Kwa sasa, niko vizuri kiasi changu. Huwa nikijitathmini na kucheck nilipofikia, napiga magoti na kumshukuru huyu Yesu Kristo tunayemuabudu.

Usikate tamaa ndugu Yangu, Mungu hajakusahau. Ipo siku yako tu.
 
Asante mkuu kwa kunitia moyo,be blessed chief
 
Madini haya
 
vitabu vichache nilivyo pitia vinasema kuwa kwa wengi wanao fanikiwa huwa wana miaka 40 mpaka 60! ndo kipindi cha mafanikio hicho, ni nadra sana kupata utajiri na kuuendeleza ukiwa na umri chini ya huo. weka malengo na kuyasimamia vizuri.
 
Duh! Inauma sana na mwaka mpya ndio huo inamaana age inazid kwenda.. usikate tamaa mpaka tamaa ikatike yenyewe
 
Duh mkuu umenena hauko mwenyewe brother elimu hii Mimi najuta kabisa kufika chuo sina hamu,nawazaga hadi nachoka heri hata wew unamishe broo na mtoto,mim sinahata mtoto kila shughuli inakufa achatuu,mungu atukumbuke sasa nimechoka sana,inafika mahali unasaka channel ukaoshe vyombo uarabuni,
 
Elimu ya Bongo haina shida,shida ni kupenda kuajiriwa,Tumia elimu yako kuanza kujiajiri. Kama elimu ya Bongo ina shida hakuna mwajiri angependa kuwaajiri wa bongo.
 
Material Possessions Drives people Crazy while its nothing to worry about at all! Jambo la msingi kwenye maisha ya binadamu ni kuweza kuingiza kipato kila siku kinachokuwezesha kusukuma siku..Umiliki wa mali na vitu sio jambo la msingi kama wengi tunavyoamini. Wengi tumegeuka kuwa watumwa wa vitu.
 
Usiwalaumu watu wa hivyo mkuu anatamani sana kuwasaidia ndugu zake, ila hizo pesa hana mamlaka nazo
 
Wewe sio mjanja, ni bonge la mjinga hata kama unafanya shughuli zako
 
Usiseme huna unachomiliki wakati una kende komavu kabisa. Hicho ni kiwanda!!!
 
Acha Mbwebwe huwezi kufanikiwa ukiwa na Mbwebwe utaki ajiriwa unajua adhaa ya kuajiliwa na kujiajili au Unasikia tu, sasa badilika ukiwa na Kitu mkononi ndio uanze hizo Mbwebwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…