Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Siku ukiadili mindset na kujua kwamba u are reaponsible for ua future na ukaacha kutupa lawama kwa mtu yoyote itakuwa ni siku kubwa maishani mwako
 
Pole sana kijana, mara nyingi ugumu unakuwa kwenye mind zetu kuliko uhalisia. Hebu amua kujiajiri kwa kuanza kidogo kidogo na mtaji mdogo. Kuanza na mtaji mkubwa sio muhimu wengi unawaona wanabiashara kubwa walianza mbali kidogo kidogo, hivyo basi wewe kwa akili uliyo nayo na utayari unaweza kufanya chochote na kufika mbali sana ndani ya muda mfupi.

Wekeza kwenye kutatua changamoto wachana na mazoea ya kuwa umesomea digrii fulani unapswa kuajiriwa sekta fulani. Fikiria kuna fursa fulani nawezaje kutoa solution na kupata kipato.

Kuna mdau ameeleza kufanikiwa ni suala la unatatua changamoto ipi na sio yale mazoea ya naijiriwe wapi ndani ya miaka 10 utashukuru kwanini ulikosa ajira maana utapiga hatua kubwa sana.
Kesho ukiamka andika mambo ma 2 au 3 unayotaka kuyafanya kisha yafanyie utafiti, baada ya hapo amua lipi la kufanya.
Kisha andika unahitaji kuanza na vitu gani, endelea kuainisha unavipataje hivyo vitu. Unaweza shangaa kumbe unaweza na mambo sio magumu kama unavyohisi.
 
kuna concept moja ukiielewa inaweza kuchange your life forever (kama utaifanyia action)

"Money owned= value created/delivered to others"

na "consumption doesn't care about education level"
JE, ushawah kwenda kununua kitu unachoitaji, lkn b4 hujalipa ukaulizia "eti muuzaji,una degree ngapi? ".... NO, kama unacho kitu ninachoitaji...you got my money, haijalishi nimesoma/sijasoma....ndio maana utakuta watu std seven wana hela kibao kuliko graduates.....making money is about solving the needs/wants of people... That's how you'll get their money

AF kwny VALUE ss, the more value u provide via solving needs/wants....The more money you'll make....

Soma these books: UNSCRIPTED na THE MILLIONAIRE FASTLANE
Chief kama una soft copy msaada
 
We siyo graduated ni graditude huwezi kuwa zoba kwa kiasi hicho nikimuona MTU ana degree halafu analalamika ajira natamani nimtemee mate huna Tina kwa taiga hili kabisa .si ajabu umeacha mashamba kijijini nawe IPO mjini unabanana na washua wakati umeacha Mali ,Mimi na degree ya HRM nibahatika kufanya field wilaya flani hadi Leo nafanya shughuri zangu kwenye wilaya hiyo na sina mpango wa kuajiliwa kabisa .
Mjinga Mkubwa wewe
 
Umeandika kwa uchungu sana, ni kweli wakati mwingine unaweza kuhisi hauna bahati kwenye maisha kwa kukosa hiki na kile, mara nyingi katika nyakati hizo huwa napenda kwenda muhimbili au ocean road hospital kama nipo Tanzania, pale nitaona watu wenye shida za ukweli, kwa kufanya hivyo, nitatazama mbingu na kumshukuru Mungu baba kwa kuniinulia uso wake na kunifadhili, afya njema na uhai ni zawadi kubwa kwangu kutoka kwa Mungu, hayo mengine ni ziada. Usikate tamaa endelea kupambana maisha hayana formula, wala hautaweza kuipata formula hapa JF.
Umenena hamna kitu chenye dhamani kama afya njema mengine mungu anajua juu yetu sisi.
 
Umeandika kwa uchungu sana, ni kweli wakati mwingine unaweza kuhisi hauna bahati kwenye maisha kwa kukosa hiki na kile, mara nyingi katika nyakati hizo huwa napenda kwenda muhimbili au ocean road hospital kama nipo Tanzania, pale nitaona watu wenye shida za ukweli, kwa kufanya hivyo, nitatazama mbingu na kumshukuru Mungu baba kwa kuniinulia uso wake na kunifadhili, afya njema na uhai ni zawadi kubwa kwangu kutoka kwa Mungu, hayo mengine ni ziada. Usikate tamaa endelea kupambana maisha hayana formula, wala hautaweza kuipata formula hapa JF.
Nakuunga mkono kuna siku nilikuwa naenda kutafuta ajira mahari nikiwa kwenye daladala nikawa najihisi mtu nisiye na bahati, pembeni yangu alikaa dada fulani alikuwa na kidonda shingoni Kwa nyuma nikawa naongea nae na kumuuliza kulikoni hicho kidonda akanijibu kuwa anaumwa kansa. Ilibidi nimshkr MUNGU na kujiona mweny bahati Kwa kunipa afya njema maisha yanabadilika sana huwezi jua kesho yako..
 
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki

Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Naomba niongezeee kidogo,hakuna ndugu anayetaka Ndugu yake afanikiwe kimaisha bora mtu baki anaweza kukusadia ukatoka kimasha sio Ndugu.
 
Hahaha pole ila usikate tamaaa maisha ni safari ndefu, na utakacho pata kitakuwa chako haswa siyo vile vya "daddy gave me" unajua eeeh, halafu familia ni factor kubwa japo siyo validy kivile labda kama una wadogo home unasaidia kuwa somesha au kutunza wazazi nk!! Kikubwa komaaa mali inatafutwa mdogo wangu, mbona wewe ni billionea anza sasaa weka malengo
 
Mtaji mkubwa kupita yote ni afya njema. Pili ni akili yako na utashi wako. Unaweza kuanza na zero na baada ya muda ukawa milionea. Mfano unaweza kuhamia mahali pafaapo kwa kilimo ukawa unapiga kazi yako na hata ukachanganya na vibarua with determination unatoka. Ziko njia nyingi usipoangalia hivyo vyeti.
 
Ninachokupongeza ni kwamba mtaji muhimu na mkubwa ambao ni Uzima na Uhai.. Miaka achana nayo wewe ni mzima kuna siku mambo yatakaa Sawa tu.
 
kuna concept moja ukiielewa inaweza kuchange your life forever (kama utaifanyia action)

"Money owned= value created/delivered to others"

na "consumption doesn't care about education level"
JE, ushawah kwenda kununua kitu unachoitaji, lkn b4 hujalipa ukaulizia "eti muuzaji,una degree ngapi? ".... NO, kama unacho kitu ninachoitaji...you got my money, haijalishi nimesoma/sijasoma....ndio maana utakuta watu std seven wana hela kibao kuliko graduates.....making money is about solving the needs/wants of people... That's how you'll get their money

AF kwny VALUE ss, the more value u provide via solving needs/wants....The more money you'll make....

Soma these books: UNSCRIPTED na THE MILLIONAIRE FASTLANE
Nimekuelewa sana mkuu thumb up!
 
Kati ya watu usiotakiwa tegemea ni
Ndugu (Tumbo Moja au W Mbali)
Familia
Marafiki

Ukiwategemea Hawa utakufa masikini, hata wawe nacho hawawezi kukusaidia zaidi watapenda uwe hivyo ili uwaheshimu
Inategemea na ndugu wa aina gani. Wengine ni mayatima wamelelewa na kusomeshwa na ndugu. Jitazame wewe na ndugu zako kaka...sio wote ni wabaya.
 
Mizunguko ya Kutafuta Ni Mingi Kuna Siku Unapata Kuna Siku Unakosa, Katika Yote Usikatee Tamaa Stay Committee, Muda wa Mafanikio Unakuja, Endelea Kumwomba na Kumwamini Mungu Aliyekupa Uzima.
 
dah pole sana mkuu... hapo ni kujiongeza tu kukaa karibu na wasiosoma wanaofanya ujasiriamali.. utajofunza mengi sana ya mtaji mdogo na jinsi ya kukuza mtaji.. ukiwa karibu na wamachinga, mama ntilie, na wengineo vijiweni....

kuna vingi tu unaweza fanya kwa mtaji wa laki moja sisi wasomi hatuvijui.. ila wasiosoma wanavijua
Umeongea point sana. Wasiosoma sana wanatuzidi mbali sana katika elimu ya biashara nimejifunza sana hili. Wasomi huwa tunaangalia sana mitaji mikubwa. Ndio maana matajiri wengi hawana elimu kubwa ya darasani.
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
Nahisi shida yako ni malengo na mtazamo wako wakimaisha mjomba.

1. Ulivo kuwa unasoma ulisoma kwa malengo yapi??...Je ulijitahidi kwa nguvu zako zote kuwa mmoja wa wanafunzi bora darasani kwako?? Ulijenga urafiki na wanafunzi wenzako na waalimu wako??

2. Je..hapo kwenye kazi yako ya sasa unafanya kwa malengo yapi? Unajitahidi kwa mfanyakazi bora au unaweka jitihada zozote za ziada kuwazidi wenzako?? Je wewe ni kwanza kufika, wa mwisho kutoka?? Unafanya kazi hata wikiendi au sikukuu ukihitajika?? Mahusiano yako na wenzako na boss yakoje?? Unatambua thamani yako kama mfanyakazi?? Je, mwajiri wako akitaka kufukuza watu kazini...je atakufukuza kirahisi au wewe ni mtu tegemeo sana kwake??

3. Kama umejiajiri, unafungua ofisi yako au biashara yako saa ngapi?? Na je unafunga saa ngapi?? Ubora wa huduma yako kuwazidi wengine ukoje?? Je ni mcheshi, mchangamfu na mtu wa watu.... au ni mtu mwenye stress na mawazo mda wote? Je unawapa wateja wako sababu yakuja kwako na wasiende kwa wengine??

4. Kwenye kila hatua ya maisha..jiulize unataka kufanikisha nini....na nini unachokifanya cha ziada kuwazidi wengine kufanikisha malengo yako. Wasomi ni wengi, uwe msomi bora.....wafanyakazi ni wengi uwe mfanyakazi bora......mamantilie ni wengi uwe mamantilie bora......machinga ni wengi uwe machinga bora....n.k..........FANYA KITU CHA ZIADA KILA SIKU UJE UTUPE MREJESHO BAADA YA MWAKA.
 
Back
Top Bottom