Admin mimi nimeolewa na nina mtoto mmoja wa kiume kabla sijaolewa nilikua na mahusiano na kijana wa kichaga kiukwel tulipendana na yule kijana alinijali aliniheshimu kiufupi tuliishi vizur mikwaruzano ilikua michache sana. Kipindi hicho nilikua sina ajira bali nilikua nafanya kazi ya najitolea kwenye tasisi fulani,ila huyo kijana yeye ni mwajiliwa wa serikalini.
Tulifanikiwa kufungua duka kiukwel duka lilikua linaenda vizuri.niliwaza huyu ndie atakuja kua mume wangu lkn haikua hivyo.
Tulikua na ukaribu hatua hadi nyumban kwao nilifahamika, na yeye alifamika kwa baadhi ya ndugu zangu ila sio wazazi na tangu nimekua nae mambo yalikua vizur kiufupi nilienjoy mapenz yake kwa kipind chote hadi pale nilipoanza kuwasiliana na rafiki yang mwngne ambae kwa sasa ni mume wangu.
Huyu kijana (name hide) alikua rafik tu, tuliambiana mambo mengi na kushauriana sikuwai kukutana nae kimwili alikua rafiki tu.. ghafra huyu kijana akaniambia kua anataka kunioa kiukwel nilizani masihara lkn kadri siku zilivyozid niliona inakua serious, niliongea na mpenzi wang mchaga nikamwambia habari za kuoana akaniambia nisubir nimalize shule coz nilikua nasoma chuo alafu ndio tutanza hizo process.
Lakini pia alikua ananisisitiza nimzalie mtoto kwanza kiukwel tulipishana mana anataka nimzalie mtoto kabla ya ndoa nikimwambia swala la ndoa anasema mpaka nimalize chuo upande wangu niliona haijakaa poa.
Sasa wazo la rafik angu la kutaka kunioa likaanza kuniingia kichwani.
Sijui ni nini kilipata nikaanza kutamani ndoa hadi inafikia hatua tunagombana na mchaga wangu swala la ndoa.
Hiyo siku niliongea na rafiki alietaka kunioa akaniambia amenipenda na ananijua mda mref hivo anaona ninamfaa kua mke wake..akaniambia tupime afya kiukwel nilifanya hivyo bahati nzuri afya zetu zilikua vizuri.. na hakuchelewa ikabidi apeleke posa nyumbani wazazi walipokea na kufanya mandaliz yakujibu posa.
Kiukwel nilikua na wakati mgumu mana nilimpenda sana mchaga. Siku moja ilibidi nimwambie mchaga kua nyumban kuna mtu ameleta posa na bado haijajibiwa yule mchaga alikasirika akaniambia kua nilikua na mahusiano mengne wakati nipo na yeye jambo ambalo sio kweli..
So alijibu kwa hasira kaniambia kama unataka kuolewa olewa na kama utanisubir sawa binafsi lile jibu sikulipenda na hapo ndio lipowaza kua mchaga alikua ananichezea tu hana haja na mimi ilibidi niwambie wazazi wajibu kua nipo tayari kuolewa, wazazi walifanya hivyo na ikawa inasubiriwa tarehe ya mahari.
Kipindi yote yanafanyika bado bipo na mchaga hatujaachana na tangu anijibu vile hatukuwai tena kuzungumzia hilo swala hivyo nilikua nafanya mambo yangu kimya kimya bila yeye kujua.
Tarehe ya mahali ilipangwa tukaenda ni nje ya mji hivyo nilimdanganya mchaga kua naenda kusalimia nyumbani kumbe naenda kutolewa mahali.
Niliporudi tu nilionana na mchaga kiukwel nilimuona hayupo sawa kabisa kwanza alikua kapungua nikamuliza shida nini akasema hakuna shida ila anahisi homa. Pia nilikua natafuta namna ili tuachane niendelee na mambo ya ndoa.
Siku iliofuata alikua kazini akanipigia simu sikupokea siku nzima iliniuma lkn nilikua natafuta namna achukie tuachane kweli siku iliofuata tena akapiga sikupokea akatuma ujumbe kuwa nipokee anajambo lamuhimu hapo nikapikea simu yake kiukwel aliongea maneno makali sana akasema anajua kila kinachoendelea na ana namba hadi ya huyo bw harusi mtarajiwa na akanitumia baadhi ya sms tulizokua tukichat na bw harus mtarajiwa na akaniambia niendelee na mambo yangu kamwe sitokuja kufurahia ndoa kiufupi aliongea maneno shiti na vitisho juu alipanik sana na ndio siku tuliovunja uhusiano wetu.
Niliolewa na Mungu akatubarik mtoto mwanzoni nilifurahia sana ndoa lkn hivi sasa naona majuto. Mwanaume amebadirika sana kwanza anataka aoe mke wa pili.. cha pili nimefatilia nyendo zake ni mtu mwenye mambo mengi hasa ya wanawake, ni muongo na tangu tumefunga ndoa hakuna mafanikio yoyote tuliopata zaid ni kupoteza na kwa upande wangu mambo yamekua ovyo sana kuna mda najitaid kuvumilia lkn roho inaniuma sana na inanipelekea namkumbuka mchaga..
Siku moja nilijaribu kutext no ya mchaga kiukwel ilikua hewani na alijibu na kunipigia tuliongea sana na nilimuomba msamaha nikamwambia nikwel nilimkosea lkn asiwe na kinyongo na mimi nilimbembeleza sana akaniambia ameshanisamehe lkn bado hajanisahau tukawa tunawasiliana tu kama friends. Lakini kadri vituko vya mume vinavyozidi namtafuta mchaga kiukwel anaifariji ikafika mahala nilimweleza kua mambo sio mazuri alihudhunika na akaniambia anaomba turudiane hata kama nimeshazaa pia akaniambia mimi nina nguvu ambayo inampa mafanikio kwahio akiwa na mimi mambo yake yanaenda vizur.. siku moja ilibidi nikutane nae na tulikaa sehemu tukaongea kwa kirefu sana na hatukufanya chochote japo alinilazimisha sana.
Kiukwel pamoja na yote yanayoendelea sijawai kumsaliti mume wangu, sasa hivi karibuni mchaga alifiwa na bibi yake ambae ninamfaham ilinibidi niende msiban nilifanikiwa kuonana na ndugu zake kiukwel bado wananipenda.
Pia na lile duka tulilofungua bado lipo baada ya msiba mchaga alinipigia simu akaniambia anataka anioe hivyo akaniambia kwakua mume wangu anataka kuongeza mke wa pili nitumie hio kama fulsa ya kuvunja ndoa ili anioe yeye na akarudia tena kusema akiwa na mimi mambo yake yanaenda vizur japo hapa kati tulivyopotezana alishakua na mahusiano lkn hayajadumu.
Kwa sasa nipo njia panda sielewi nawaza je anania kweli yakunioa au anataka alipize kisasi?
Kwasabu ni haraka sana anataka hili jambo na je ananipenda kweli au anatumia ushirikina mana anasema mimi ndio nguvu yake yamafanikio naogopa na sielewi nifanye maamuzi gani nipo njia panda au nibaki tu kwenye ndoa nivumilie lbda atakuja kubadirika...
Nimelileta kwenu naomba ushauri nipo njia panda nashindwa kufanya maamuzi nachotaka niwe na furaha.