Ni nafasi nyingine tena kukutana katika jukwaa hili. Leo nataka tuzungumze kwa habari ya ushauri vile ambavyo unafanya kazi, na vile ambavyo unaweza kubadilisha maisha ya mtu yakawa mazuri au mabaya kulingana na vile utakavyotumika huu ushauri kwa aliyeupokea.
Maisha ya mwanadamu anaeishi chini ya jua yanategemea kwa kiasi kikubwa ushauri wa marafiki, ndugu zetu na watu wa karibu yetu katika kufanya maamuzi. Ushauri huo unaweza kuleta mafanikio chanya au hasi kulingana na namna alivyoutendea kazi yule alieshauriwa.
Watu hutoa ushauri kulingana pengine na matakwa yao, tamaa zao au mapenzi yao juu ya wale wanaowashauri. Ushauri utokanao na tamaa au matakwa ya mtu huleta matokeo ambayo si mazuri kwa alieufanyia kazi.
Mfano; mtu akikutukana na kukutupia maneno mengi mabaya, ukaamua kunyamaza, wapo wengine watakuja wakikushauri "aah, usikubali kukaa kimya, usimwache tena inabidi umfundishe adabu maana atakuzoea, hawezi kukutukana vile na kukuaibisha mbele za watu". Kumbe kwa sababu ya chuki zao binafsi juu ya yule mtu ndio maana wanakushauri hivyo. Hivyo basi ushauri wa aina hii hutokana na matakwa, tamaa au mapenzi ya mtu tu.
Lakini uko ushauri utokanao na matakwa au mapenzi ya Mungu na huu ushauri huzaa au kuleta matunda mema.
Mfano; mmegombana na rafiki yako mara akaja ndugu akawa anawasuluhisha bila kuegemea upande mmoja huku akiitafuta amani baina yenu. Hapo hupandwa mbegu njema yenye amani na uzima.
Watu wengi sana duniani wanaishi maisha ambayo si mpango wa Mungu wao kuishi maisha hayo, lakini ni kwa sababu tu wamesikiliza ushauri ambao umewafanya waishi hivyo.
Mfano mzuri katika maandiko matakatifu biblia, vile ambavyo nyoka alivyoweza kumdanganya yule mwanamke hawa kwa kumwambia, "hakika hamtakufa" wakati Mungu aliwaambia mkila matunda hayo "hakika mtakufa" na hatimaye kuwafanya adam na mkewe waishi maisha ambayo si mapenzi ya Mungu wao kuishi hivyo. Hata katika maisha ya uhalisia, ndoa nyingi haziko na amani ndani yake kufuatana na hao wanandoa kusikiliza au kufuata ushauri pengine wa wazazi wao au taratibu za makabila au tamaduni zao.
Ni kweli kwamba Mungu hutumia watu kufikisha ujumbe kwa watu wake hali kadhalika na shetani nae hutumia watu.
Je huo ushauri ulioufanyia kazi kwenye maisha yako ulitokana na Mungu au ulitokana na shetani?. Na je umeleta matokeo gan kwako?. Kwa sababu Mungu akimtumia mtu husema yaliyo ya Mungu ambayo si matakwa ya akili yake au tamaa zake bali huyanena yatokanayo na mapenzi ya Mungu mwenyewe, bali mtu akitumiwa na shetani hutoa ushauri utokanao na matakwa au tamaa zake mwenyewe ikiwemo chuki, wivu na tamaa ya mwili.
Hebu tazama ushauri ambao mke wa ayubu anamshauri mumewe, ulikuwa ni ushauri wa kumpotosha na kumwondoa katika mapenzi ya Mungu (ayubu 2:1-10).
Hatukatai ushauri lakini tunatakiwa kupima sana shauri tunazopewa na marafiki au ndugu zetu, je zinatokana na mapenzi ya Mungu juu yetu? Hata kama ni mzazi wako anakushauri, upime huo ushauri wake kwamba utakuletea matunda mazuri au mabaya?. Na ukikuta huo ushauri haukuletei mafanikio, tafadhali sana achana nao.
Usije ukapishana na baraka zako au mafanikio yako kwa kuwasikiliza watu kumbe hao watu hawapendi wewe ufanikiwe, wanataka tu kuona ukiwa masikin kila siku, ukiteseka katika huo ugonjwa, ukipoteza tumain juu ya maisha na kadhalika. Tujitahidi sana kuchambua maneno ya kuyafanyia kazi yenye tija kila mara tunapopewa ushauri na watu, maana wengi hutoa ushauri kwa nia zao za miili na tamaa zao.
Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti tu siku zote, bali nia ya roho ni uzima na amani. Mtu akikupa ushauri utokanao na Mungu huo umebeba nia ya roho mtakatifu na huleta uzima na amani ndani yake, sasa je, huo ushauri uliopewa wewe, una uzima ndani yake? Au unaleta amani kwenye maisha yako? Au ndio kwanza unachangia kuondoa amani ndani yako na kukufarakanisha na Mungu wako?.
Wengine hutoa ushauri kwa sababu ya wivu, uchungu na ugomvi ndani yake, hivyo basi huo ushauri ukifanyiwa kazi huzalisha tu machafuko. Bali ule utokanao na Mungu ndani yake hakuna hila, fitina, unafiki, magomvi, umejaa rehema, amani, upole na husikiliza watu. Mungu atusaidie sana kuyajua mambo yafuatayo katika maisha yetu ya kila siku kwa habari ya kupokea ushauri kutoka kwa watu wengine;
Kwanza ni kujua kuwa huu ushauri utaniletea matokeo gani nikiufanyia kazi. Maana pasipokujua matokeo yake ya baadae hauwezi kuchambua kati ya ushauri mzuri au mbaya.
Pili, je huu ushauri unatokana na Mungu? Maana kama unatokana na Mungu huleta amani ndani ya mtu na una uzima rohoni
Tatu, tamani sana kumjua kwa undani huyo anaekupa ushauri kabla hujaufanyia kazi huo ushauri wake, maana mtu aweza kukupa ushauri kutokana na chuki au wivu wake juu yako.
Na mwisho pia jaribu au tamani kujua huyo anaekupa huo ushauri anatarajia kupata nin baada ya hapo?. Ukiona huyo mtu anakupa ushauri akitaraji kupata kitu baada ya hapo, uchunguze sana huo ushauri na uupime kwa andiko la Kimungu.
Yako mambo mengi ya kuzungumza lakini ninachotamani ukijue katika makala hii ni hili suala la ushauri ambalo watu wengi hulidharau na kuliona jambo la kawaida tu lakin kumbe ndani yake limebeba mambo mazito na hatma za maisha ya watu ambayo mtu asipoyajua anaweza kujikuta anapoteza mwelekeo wake na kuharibu mfumo mzima wa maisha yake.
Natamani sana Mungu akupe uelewa juu ya jambo hili ili ikitokea umekutana nalo ujue namna ya kukabiliana nalo. Maana pasipo kupewa ushauri pia tunaweza kujikuta tumeharibu katika kufanya maamuzi juu ya hatma kwenye maisha yetu.
Tujitahidi tu kupambanua shauri za kutumia au kufanyia kazi katika kile ambacho tunataka kufanya, kwamba kinaendana na huo ushauri au matokeo yake yatakuwaje?. Nihitimishe kwa kusema, kila jambo na wakati wake, hivyo bas wakati wake hilo unaloliwaza au unalotaka kulifanya ni huo, na linaendana na huo ushauri uliopewa.

Upvote
0