Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Naomba kujuzwa, naweza kupata Rav 4 lile toleo la mwanzo kabisa au toleo la pili kwa Mil 7? Shukran wadau
 
Wakuu mambo vipi Nahitaji kuagiza gari ya kiamerica especially hummer but Nataka kuagiza direct from American ni website gan ni nzur na uhakika inayouza Magari direct from American nimeshazoea japan sina ujuzi na American
Kama hujapata msaada check na kampuni hii ya kibongo watakuelekeza www.kalumbilo.online
 
Habar wapendwa nataka kununua Suzuki Jimny je ni nzuri?VIP spare zinapatikana?
 
Nataja kununua Suzuki Escudo ya 2001 nimewasiliana na SBT Japan wameniambia 16ml.vp wadau hawa jamaa wako safi?

Pia nishaurini ni gari ya kazi kwa road zetu bongo?
 
Wakuu kuna haice yangu nimeipaki ina tatizo la injini naomba mwenye kujua garama itakost sh kufanya overholl ngapi kurudi barabarani tena. Na kulipia tra, bima na Sumatra itanicost how much
 
Wenye uzoefu wa Suzuki Jimny. Manual Vs Automatic kwa hapa bongo, vp spea na services zake? Zina tatizo lolote?
 
Mwenye uzoefu na Toyota SPACIO. Natarajia kuichukua! Vipi ni Gari nzuri kibongobongo?
 
Naomba kujuzwa, naweza kupata Rav 4 lile toleo la mwanzo kabisa au toleo la pili kwa Mil 7? Shukran wadau

Mimi ninayo old model ile toleo la kwanza nyeusi milango mi5, namba A engine iko poa kinoma ila 7m siuz,hiz Gari ni ngumu ajabu! BT 7m unaweza pata zile ndogo za milango mi3 au ukapata ya milango mi4 ambayo utahitaji kubadili engine na gear box.
 
Nataka kuagiza gari kupitia befoward au SBT au Trust sasa naogopa kuibiwa kwenye mitando, na niko mikoani ambako siwezi kufika dar kirahisi nitaagiza vp na nitajuaje kama pesa zangu zi salama sijaibiwa? Swali la pili, gharama ninazoziona kwenye tra calcultor +cif ndo basi nalipata gari langu au kuna nyongeza ya makato? msaada plz urgently!
 
Back
Top Bottom