Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Milioni 6 sijui kam utapata. Ila kwenye Starlet siku hizi zinatengenezwa? Maana highest version ya Starlet ni Ist.

Kwa nini usigoogle tradecarview, ukacheki bei (cif), then nenda Welcome to GariYangu.com - GariYangu.Com ucalculate tax. Ingawa hutopata exact amount lakini utapata idea uandae bei gani?

Natumaini wataalam watakuja kukupa mwongozo zaidi
 
Kwa milioni sita utapata gari iliyotumika miaka 4-5 hapa bongo, hupati gari lilioagizwa mwaka huu.
 
Nawashukuru sana wanajamii kwa maoni yenu, nitayafanyia kazi. Anatakiwa siku njema na mbarikiwe sana.
 
Nawashukuru sana wanajamii kwa maoni yenu, nitayafanyia kazi. Anatakiwa siku njema na mbarikiwe sana.
Vits nzuri tena ya mwaka 2003 kupata ni ngumu sana .ila kwa Starlet unaweza pata

Starlet inadumu sana afu kidogo body yake ni imara na ngumu kuliko Vits. Jaribu kuangalia ustaarabu wa kuagizia Starlet.
 
Nashukuru sana mkuu, nitayafanyia kazi ubarikiwe sana.

Vitz ni nzuri coz haili mafuta lkn ukiagiza bei itakuwa zaidi ya 6m kwa jinsi ushuru ulivyopanda, Starlet ni nzuri ila inakula mafuta zaidi ya Vitz angalia model nyingine kama Duet nayo ni nzuri kwa ulaji wa mafuta
 
Kwa ufaham wangu mdogo, latest version ya starlet ni ya mwaka 1998, inaitwa CARAT. Sidhani kama baada ya hiyo kuna starlet ilishatengenezwa, labda nakosea

Starlet ni durable na fuel consumption ni safi, pia spares zipo kwa wingi, it is the best car uki compare na vits.ukiagiza japan hiyo 6m inaweza ikatosha kabisa, ikizidi itakuwa kwa kiwango kidogo because of charge ya uchakavu. Kila la kheri.
 
Mupirocin,
Mkuu ulivyoanza kujieleza hadi nikasahau kama unaomba ushauri wa kununua gari. Anyway, mimi nilinunua Vitz mwaka jana mwanzoni kwa Tsh. 7Mil so jipige pige uongeze dau angalau ifike 7M kaka ndio utakuwa na uhakika wa kupata Vitz ya uhakika.
 
Wadau nashukuru sana kwa maoni yenu nitayafanyia kazi, JF ni zaidi ya mtandao unaboresha maisha pia, nashukuru sana.
 
Dear Members,

nataka kununua gari kupitia Sakura Automobile je ni waaminifu maana ninawasiliana na Nalaka De soysa naomba ushauri wadau.

Thanks
 
Hell guys!

I want to buy a car but sijui ni aina gani kati ya haya la gari litakalo nifaa kwa matumizi ya kawaida na pia ndio litakuwa my first car sasa mimi sio mjuzi sana wa magari, i have a lot of choice of car like Spacio, Raum,na Escudo haya ndio ninayoyapenda lakini je ni mazuri kwa matumizi ya mafuta pamoja na spare?

Nategemea ushauri toka kwenu wapendwa
 
Kama kipato chako ni kama changu basi go to Raum

1- Spea zake bwerere kwani zinaingiliana na Toyota Corola, Starlet
2- Bei ya spea ni sawa na chee, na ukitaka used basi pale Ilala never ever kuulizia maduka mawili
3- Kiwese ni kama inanusa tu, vum vum tayari upo Bagamoyo
4- Service yake ni cheaper sawa na Bajaji
 
vipik2
Raum, kitu Used kitumie mafuta kwa kunusa? Matumizi ya mafuata kwa RAUM ni wastani wa 10km/l, town; 13-15km/l, highway. Bei ya spea ni sawa: Spacio au Corrola na Raum bei yake ni nafuu.

Kama ilivyo kwa Road licence na insurance. Kwa Escudo spea ni bei mbaya, na ni shida kuzipata kama hauko DSM. Nakushauri ununue Spacio new model.
 
Mimi sipo katika spare wala kusumbua, usifate gari imetembea mileage kiasi gani, angalia gari iliyotengenezwa 2004 na kuendelea, vinginevyo unaweza kulipa CIF 2000 kule Japan halafu hapa ukaja ukaambiwa ushuru 8m ukaikimbia bure!
 
Naomba kujua bei ya gari hizi kwa wastan, ikiwezekana nijue tofauti ya kuagiza na kununua hapa , na nasikia kuwa Zenji bei poa je ni kweli?

Mark 2 Grande - 15,000,000 - 18,000,0000
Verossa - 16,000,000 - 20,000,000
Mark X - 18,000,000 - 25,000,000
Toyota Harrier
- 14,000,000 - 16,000,000 zile model za zamani hizo LX ni 30,000,000 up to 40,000,000
 
Back
Top Bottom