Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Naomba kuuliza wadau, kama gari zinazouzwa yard, Dar zipo za kuaminika. Napata shida sana nikiwaza kuagiza gari (used) toka Japan au kwingineko kwa kuwa muda wa kusubiria ni mrefu sana. Naomba kama kuna mtu ana info ya mahali Dar, naweza kupata gari za kuaminika na bei reasonable.

Yard nyingi wanacheza na adometer, yani gari imetembea 200,000km inarudishwa hadi 70,000 km then unauziwa mbuzi kwenye gunia, gari nyingi hua zimetumika hapa bongo then wamiliki wanazidisplay yard then ikiuzwa wanamlipa commision yule mwenye yard. vile vile gari nyingi huwa zinatoka uarabuni "Dubai" ambako wao sio wazalishaji wa magari, hua wananunua gari used kutoka japan au uk, wanaitumia then wana recondition kwa hiyo wewe unakua "third hand"

Niliagiza gari zangu Nissan Civillian bus mara tatu kupitia kampuni moja ya Japan. kila gari ikifika sikuamini macho yangu kwa jinsi ilivyo nzima. Pia kuagiza gari ni risk sana kama hauna uzoefu. watu wengi wamelia, "sikutanii"

Ninachoweza kukusaidia, ni kukuagizia gari kwa kutumia uzoefu wangu, risk zote ntazibeba mimi. Tutafunga mkataba na nitaweka dhamana gari yangu moja, kama hiyo gari haitakuja ndani ya miezi miwili ntakurudishia pesa yako.

Kama uko interested wasiliana na mimi kwa namba 0763294739,ila utanilipa commision kidogo. Zaidi ya hapo nakuhakikishia gharama ya kununua hilo gari itakuwa chini kwa zaidi ya 3million ukilinganisha na bei za yard.
 
no name no name, Kukuhakikishia usalama wa pesa yako, utaituma pesa ya CIF moja kwa moja kwa muuzaji, that means mimi sitaishika pesa yako hata kidogo, then gari ikifika, TRA utawalipa kwa mkono wako mwenyewe.
 
no name no name, Model nyingi za baada ya 2003 ukifanya hili haziwaki kwa vile ni digitised au likiwaka basi litaleta shida punde tu. Halafu usifuate sana odometer mtu anaweza kukuuzia gari iliyopiga 50,000 ya ukweli lakini hakuna service wala maintanance iliyofanyika wakati unaweza pia kununua lenye 200,000(hasa toka UK) lakini likawa limetunzwa vizuri.

Hilo za la Dubai si kweli kwa kuwa Dubai hawaruhusu kuendesha used cars na pia wao wantumia upande wa kulia wa barabara na magari toka UK na Japan yanatumia kushoto
 
Naomba kujua bei ya gari hizi kwa wastani, ikiwezekana nijue tofauti ya kuagiza na kununua hapa, na nasikia kuwa Zenji bei poa je ni kweli?

- Mark 2 Grande
- Verossa
- Mark X
- Toyota Harrier
 
Naomba kuuliza wadau, kama gari zinazouzwa yard, Dar zipo za kuaminika. Napata shida sana nikiwaza kuagiza gari (used) toka Japan au kwingineko kwa kuwa mda wa kusubiria ni mrefu sana. Naomba kama kuna mtu ana info ya mahali Dar, naweza kupata gari za kuaminika na bei reasonable.

Sio reliable kwa sababu uwezi kupata genuine full details za hayo magari. Nenda kawaulize grade za hizo gari utapata jibu la nini nina maanisha!
 
Model nyingi za baada ya 2003 ukifanya hili haziwaki kwa vile ni digitised au likiwaka basi litaleta shida punde tu. Halafu usifuate sana odometer mtu anaweza kukuuzia gari iliyopiga 50,000 ya ukweli lakini hakuna service wala maintanace iliyofanyika wakati unaweza pia kununua lenye 200,000 (hasa toka UK) lakini likawa limetunzwa vizuri. Hilo za la Dubai si kweli kwa kuwa Dubai hawaruhusu kuendesha used cars na pia wao wantumia upande wa kulia wa barabara na magari toka UK na Japan yanatumia kushoto

Magari nayajua vilivyo, lakini scientifically depreciation ya gari inategemea sana mileage, kwa jinsi nilivyo najua hiyo ni opinion ya mtu na sio fact. by the way magari mawili moja lina 50,000 na limetunzwa vizuri na jingine lina 200,000 na limetunzwa vizuri hayafanani. usiwe compromised na opinions unaponunua kitu cha gharama.

Kwa kusema baadhi modeli za 2003 and above haziwezi kuchezewa adometer automatically umekubali magari mengi below 2003 yanaweza kuchezewa adometer, Vile vile hiyo sio Fact kwa sababu inategemea ni gari gani mbona kuna benz za mwaka 1998 ziko digital kwelikweli na kuna gari za above 2004 tunazijua zilichezewa adometer.

Dubai ni kariakoo ya Uarabuni, Magari yale yanakua hayajatumika pale dubai ila yamepelekwa sokoni, kukuhakikishia nenda kwa waagizaji wengine wa magari waulize hii ishu. Take time kufanya utafiti " NO DATA NO RIGHT TO SPEAK"

Simshauri mtu kununua gari dogo lenye 100,000 and above, hayo mambo ya "lilikuwa well maintained" ni kuingizana mjini tu, wewe utajuaje wakati alokua mmiliki wake humjui.

After all mtu anae uza gari yard anatafuta faida kubwa, so lazima aweke cha juu 3,000,000 then anakula kiulaini.

Mfano hai, nilienda kuuliza yard zaidi ya tano bei ya Nissan Civillian jamaa wanaanzia 37,000,000 and above nakumbuka alikubali kunipunguzia laki mbili tu. Lakini nimeagiza gari hadi kodi kila kitu nimelipa 29,000,000. Na nimepata gari nzuri.

Inategemea ni supplier gani anakuuzia kule japan, kuna upuuzi mwingi ambao kama sio mzoefu sikushauri kabisa kuagiza gari nje coz unakua huajaliona physically. Unapokuwa na supplier wa kuaminika kama niliye naye mimi kununua gari yard ni gharama sana.
 
Model nyingi za baada ya 2003 ukifanya hili haziwaki kwa vile ni digitised au likiwaka basi litaleta shida punde tu. Halafu usifuate sana odometer mtu anaweza kukuuzia gari iliyopiga 50,000 ya ukweli lakini hakuna service wala maintanace iliyofanyika wakati unaweza pia kununua lenye 200,000 (hasa toka UK) lakini likawa limetunzwa vizuri, hilo za la Dubai si kweli kwa kuwa Dubai hawaruhusu kuendesha used cars na pia wao wantumia upande wa kulia wa barabara na magari toka UK na Japan yanatumia kushoto

Kuna miji ua Uarabuni ambayo imechoka kama hapa kwetu namikweche yao ambayo imekua reconditioned wanauzia kariakoo ya uarabuni "Dubai", kwa mfano sehemu kama Al Rahba, Madha, Swaihan, Abu dhabi zimechoka tu na ni RHD drivers. So kuhusu mitumba ya uarabuni sio reliable.
 
Model nyingi za baada ya 2003 ukifanya hili haziwaki kwa vile ni digitised au likiwaka basi litaleta shida punde tu. Halafu usifuate sana odometer mtu anaweza kukuuzia gari iliyopiga 50,000 ya ukweli lakini hakuna service wala maintanace iliyofanyika wakati unaweza pia kununua lenye 200,000(hasa toka Uk) lakini likawa limetunzwa vizuri. Hilo za la Dubai si kweli kwa kuwa Dubai hawaruhusu kuendesha used cars na pia wao wantumia upande wa kulia wa barabara na magari toka UK na Japan yanatumia kushoto

CAMARADERIE magari arabuni yanapita tu hayaingii hata mjini. Yakitoka bandarini yanaenda yard tatizo ni kuwa wanachomoa vitu muhimu na kuleta kama used huku kwetu ndio tatizo lao mkuu tu. Na kuhusu mileage ni kweli kuwa kama gari inakuwa inahudumiwa ipasavyo mileage si issue sana.
 
Wakuu nauliza hivi, ukinunua gari mnadani ambalo halijalipiwa kodi, unatakiwa kulipa kodi zipi? I mean rate zake! Nawasilisha wakuu.
 
Kwa hiyo kimsingi kumsaidia Tuko, ni wapi Dar aende kununua gari bila kuwa na wasiwasi wa kuchakachuliwa?
 
Nakushauri agiza kama huna haraka tena watumie TRUST COMPANY magari yao yaliyotumika Japan kabla ya kuyauza yamnafanyiwa service ya ukweli then unauziwa huwezi tapeliwa pesa yako. Yard za Bongo wanatoa spea wanauza then wewe unapewa gari yenye vifaa vibovu.hata kama utaenda na fundi anaweza kudakishwa kitu kidogo ili akwambie gari ni nzuri uichukue.
 
Wakuu naomba kuuliza hivi hawa jamaa wanaojiita TRADE CAR VIEW wanaaminika kweli maana bei zao ziko chini ukilinganisha na wengine wengi
 
Wakuu naomba kuuliza hivi hawa jamaa wanaojiita TRADE CAR VIEW wanaaminika kweli maana bei zao ziko chini ukilinganisha na wengine wengi


Mkuu siyo kila kampuni iliyojiandikisha kwenye TradeCarview inaaminika! Kuna baadhi hata haziaminiki, ninachokushauri kama unataka kununua gari kupitia hiyo kampuni, basi nunua kupitia huduma yao inaitwa PayTrade. Ila inakubidi kulipia gharama kidogo, mfano kama CIF ni $ 3000 basi utaongeza $150 zaidi.

Nadhani nimesomeka kwa kiasi flani
 
Wakuu naomba kuuliza hivi hawa jamaa wanaojiita TRADE CAR VIEW wanaaminika kweli maana bei zao ziko chini ukilinganisha na wengine wengi

Tradecarview wanaaminika,tatizo lao ni kuchelewesha tu,ukishalipia utasubiri sana nadhani ni kutokana na wateja wengi bookings za meli zinawazingua.ukipata BeForwad lipia bomba sana hao jamaa wako fasta mbaya!
 
Kuna mtu amashawai kuagiza na kampuni ya REAL MOTOR JAPAN? Vipi kuaminika kwao?
 
Kwa hiyo kimsingi kumsaidia Tuko, ni wapi Dar aende kununua gari bila kuwa na wasiwasi wa kuchakachuliwa?

Kuna kampuni kadhaa za Wajapani zenye ofisi zao Dar, wanauza magazi mazuri tu. Jamaa yangu alinunua GX 100 miaka miwili iliyopita, bado inadunda mpaka sasa. Mfano wa makampuni hayo ni Car Junction (Opposite Ubungo Plaza), Yuasa (wapo pale Victoria, Ali Hasan Mwinyi rd), kuna kampuni nyingine (nextage cars) wapo Haidery Plaza) City centre, nao bei zao ni nzuri. Jaribu bahati yako
 
Wana JamiiForums,

Nahitaji kununua Vitz, IST au Rav 4 ambayo iko kwenye hali nzuri. Kwa mwenye uwezo wa hili naomba ani inbox kwa details zaidi.
 
Wakuu mimi ni mwajiriwa mpya ninamiezi miwili tangu niaze kazi mimi na wife tunafnya kazi moja na shirika moja.

Huku tulipo usafiri kidogo ni shida kiufupi nipo nje kidogo na songea mjini kama km 25 hivi. Lakini pia malengo yangu ni kumiliki ardhi pamoja na business nyingine lakini pia nataka usafiri coz kila wiki lazima nifike town kwa shopping sasa napata shida mizigo.

Tumekaa na wife tukafikiri tununue gari simple kama starlet au vitz naamini haziwezi nikamua sana lengo kuu ili mambo yote yaende kuliko nikiplan kununua labda gari ya zaidi ya 10m afu nikaandaa almost one year na mambo mengine yasiende.

Msaada:
Kati ya Vitz na Starlet ipi ni imara? Nataka ya kati ya 2003-2007/ Je nikinunua hapa bongo na kuagiza kutoka Japan lipi ni nafuu? Kwa ujumla wanaJF hili wazo mnalionaje?

Kumbuka kwa sasa sina source nyingine ya money zaidi ya mshahara, na mimi na wife tunasave 1m each month. Ushauri wenu wanajamii na wachumi kwa ujumla, na naamini mchango wenu utanisaidia sana kuboresha maisha yangu.

Natanguliza shukrani.
Bajet nitaandaa 6m.
 
Back
Top Bottom