Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Jamani hii kampuni vipi genuine au wa NIGERIA wa JAPAN?

Used Cars from Japan » Japanese Used Vehicles » JapanTradeCar.com
 
TZINVESTOR, Achana na Tradecarview, kuna gharama zaidi. Mambo ni BEFORWARD.JP hawa jamaa wana magari ambayo hayajachoka na bei reasonable, huduma safi na kila kitu systematic. Mimi tayari nimeshanunua magari matatu ndani ya mwaka huu toka kwao. Ukitaka ushauri zaidi utaupata.
 
nahitaji Carina lakini kuagiza huko nje sitaweza kwakuwa bajeti yangu ndogo, million tank hadi sita. ni gari yangu ya kwanza kabisa maishani. nawezapata hapa bongo jamani wataalam?

Ni sawa bongo utapata hata kwa millioni 4 ila angalia utajuta baadae. Uzoefu wangu ni huu, wabongo wengi tunaagiza nje magari used, tunatumia hadi tunachoka tunauza kwa mtu ambaye nae labda ndo atakuuzia wewe ikiwa tayari imemsumbua au hata kama haijamsumbua lakini itakua ktk hali ya kuchoka. Utakua hutoki garage na usumbufu mwingine ambao utaona bora ungeongezea hela ukaimport toka Japan?!

Kama una mil 6 nakushauri tafuta nyingine moja ziwe 7 uagize Japan gari zima kabisa lililokimbia km chini ya laki moja. Ukitaka ushauri utaupata kwetu wazoefu na uagizaji wa magari.
 
Achana na Tradecarview, kuna garama zaidi. Mambo ni BEFORWARD.JP hawa jamaa wana magari ambayo hayajachoka na bei reasonable, huduma safi na kila kitu systematic. Mimi tayari nimeshanunua magari matatu ndani ya mwaka huu toka kwao. Ukitaka ushauri zaidi utaupata.
BEFORWARD Hawa naowajua pale Ocean Road naona watu wanalia labda BEFORWARD ya Japan nitakusoma sio hawa makanjanja kwanza wanauza magari daraja la chini yaani machakavu hiyo nakupa siri.
 
na hii suzuki swift

Version/Class


L LIMITED
Chassis #HT51S-830281
Engine Size1,320cc
Engine CodeM13A
Drive-
Ext. ColorLight Blue
SteeringRight
Transmiss.Automatic
FuelGasoline/Petrol
Seats5
Doors5
Dimension
(L×W×H)
3.61×1.60×1.54 m
M38.895
Weight920 k

TOTAL PRICE = FOB Price + Shipping Cost + Insurance + Inspect + Cer=USD $2,275

Nahitaji bei gani hapo mpaka car on the road kwa bei za kitanzania wadau?
 
Mkuu si kweli unayosema. Kwenye tradecarview magari yaliyopopale tayari makampuni yake yameonyeshwa na baei za magari yao pia na si kwamba magari yanauzwa na tradecarview, wao ni mkusanyiko tu wa makampuni mengi yanayouza magari. Uzuri wa kwenye tradecarview kuna wigo mkubwa wa kuchagua magari tofauti na hiyo beforward.jp maana nimeangalia ni wachovu kwelikweli hawana Harrier ya kuanzia mwaka 2001 hata moja, Suzuki escudo ya kuanzia mwaka 2001 hakuna hata moja na pia hawaonyeshi mileage ya magari yao kitu ambacho ni hatari maana unaweza kununua gari lililokongoroka hasa. Kuna watu kadha wa kadha niliokaribu nao wamenunua kupitia tradecarview magari mazuri kabisa kwa bei nzuri.
Mkuu hivi kwa mfano naamua kwenda Japan ili nikanunue magari,nitakutana na hizi bei ambazo ziko kwenye mawebsite au itakuwa kubwa/ndogo zaidi ya hizi bei?
 
Mkuu hivi kwa mfano naamua kwenda Japan ili nikanunue magari,nitakutana na hizi bei ambazo ziko kwenye mawebsite au itakuwa kubwa/ndogo zaidi ya hizi bei?

Mkuu huko utanunua mwenyewe kwenye minada ambako hawa makampuni wananunua na kutuuzia hivyo utapata Kwa bei ndogo zaidi.
 
Mkuu huko utanunua mwenyewe kwenye minada ambako hawa makampuni wananunua na kutuuzia hivyo utapata Kwa bei ndogo zaidi.
Najitahidi ku google ili niweze pata maelezo zaidi juu ya hiyo minada lakini sipati majibu sahihi. Je,unazijua address au website za hao wafanya minada ili unisaidie?
 
Washawasha

Mkuu minada hawauzi kwenye mitandao. Wao wanauza ana kwa ana vinginevyo wataua biashara za haya makampuni ya kwao yanayotuuzia kwenye mitandao. Kwahiyo huwezi kununua moja Kwa moja kwenye mnada vinginevyo upate mtu aliyeko huko aende akakununulie.
 
Mkuu minada hawauzi kwenye mitandao. Wao wanauza ana Kwa ana vinginevyo wataua biashara za haya makampuni ya kwao yanayotuuzia kwenye mitandao. Kwahiyo huwezi kununua moja Kwa moja kwenye mnada vinginevyo upate mtu aliyeko huko aende akakununulie.
Nimekuelewa kiongozi,vipi nikifanya mpango wa kwenda mwenyewe si itakuwa kidogo afadhali au taratibu zao za kutoa visa zinabana?
 
Wakuu naitaji kununua suzuki swift 2007, cc <1500 toka japan. Na viela vyetu ndio hivi hivi vya kuunga, nilikuwa nauliza kwa yeyote mwenye kujua chochote hivi ulaji wake ya mafuta upoje? Upatikanaji na bei za spare zake upoje? Alafu kwa kuzingatia hii bajeti mpya hushuru wake unaweza ku-range vipi kwa hawa jamaa zetu wa TRA? Msaada wenu.
 
Si kweli, ile ilijadiliwa ila haikupitishwa, walirudi kwenye makubaliano ya ileile miaka 10.
 
Kwa Japan hawa Be Forward ndio kampuni inayonunua magari yaliyochoka zaidi minadani
 
BIGURUBE, sina hakika na hilo ulilolisema, maana mitaani naona gari kutoka website ya befoward zipo kibao mitaani na zinatembea, maana kama kungekuwa na ubovu tusingeziona gari toka kwao zikizunguka mitaani
 
Back
Top Bottom