FEDRICK SANYA
New Member
- Jul 21, 2021
- 1
- 1
VIJANA TUAMKENI MUDA HAUTUSUBIRI
Habarini ndugu, jamaa na marafiki.
Kwanza kabisa nitumie fursa hii kuwakumbusha Mafanikio yoyote ni Kuchukua hatua tuache kukaa nakuzungumza bila kuchukua hatua.
Katika kutafuta mafanikio, vijana tuzingatie sana sana Uaminifu.
Hivyo basi nianze kueleza mambo machache ili tuweze kufanikiwa kama vijana
MOJA
Kama nikijana umemaliza chuo na bado hujaajiriwa jambo la kwanza kufikiria ni kwamba muda haukusubiri anza kupambania ndoto zako.kumbuka Kadri siku zinavyokwenda ndivyo majukumu yanavyokujia taratibu.
Nini ufanye
1. Kwakuwa mtaji ni tatizo basi tumieni mitandao yenu kuunda magroup ya vijana mnaofahamiana kutoka vyuoni mlikosoma andaeni jukwaa lenu jadilini vipi mnaweza kupata mtaji. Mwaweza kupata mtaji kupitia kuchanga wenyewe taratibu, kuna m-koba navingine vingi, pia mnaweza kukopa kutoka taasisi za fedha.Na kufanya hivyo mnaweza mkaanzisha biashara.
USIOGOPE
Hakuna jambo Duniani lisilo la risk. Kila biashara na kila jambo kuna risk, lakini wote waliofanikiwa ni watu wasiogopa risk.
Kuna biashara za makampuni ya weka fedha baada ya wiki au mwezi upate fedha mpka asilimia 60%
Hii pia yaweza kuwasaidia vijana kupata mitaji yenu nakuanzisha biashara.
2. Pia kuna fursa zinazo tuzunguka kulingana na eneo ulilopo mfano nitaje kwa uchache
(a)Kuna suala la kuuza matunda. Tafuta eneo zuri. Liboreshe uza matunda pandisha thamani kwa kuandaa mazingira safi na vifungashio bora kabisa. Hii haihita sana uwe na mtaji mkubwa. Anza na mtaji mdogo kabisa kuliko kukaa nyumbani unagombania remoti nawatoto
(b)Kuna suala la Fresh juice. Pia hii ni fursa kubwa mno ukiifanya kwa ustadi kulingana na wapi ulipo.kuna maeneo ya viwanda, maofisi, shule na kadharika.unaweza kuandaa vizuri, ukazipaki vizuri na ukafanya biashara ukajiingizia kipato.hapa ni kujitambua na uthubutu
(c)Kuna suala la usambazaji wa bidhaa(distributers) Hii nayo ni biashara nzuri sana, suala hapa ni kufikisha bidhaa kwa mteja kwa wakati. Unaweza kutangaza biashara online mfano mavazi, vyombo vya ndani, electronics(simu,komputa) na vingine vingi then unapata mteja unampelekea mpka alipo.hapa uaminifu na kujibrandi Uaminifu wako. Inawezekana kabisa kabisa
La kuzingatia tazama wapi ulipo jaribu kufikri, share nawatu mawazo yako. Usikae kupiga story zisizo nafaida unapoteza mda na pia mda ukipotea umepotea, huwezi kuurudisha.
3. Kuna fursa Minadani au sehemu yenye mikusanyiko ya watu kama kwenye viwanja vya mipira(ndondo),saba saba, mikutano na makongamano ya dini na siasa, vijana tunaweza kutumia kuuza bidhaa ndogo ndogo ambapo hizo mikusanyiko inapokwisha wewe unakua imefaidika na uwepo wao. Fikiria nini waweza kufanya je nikuuza chakula,maji au vinywaji au nini ufanye.
MBILI
Lipo jambo la KILIMO ambalo mimi binafsi nalikubali asilimia 100%.vijana tuamkeni. Tumesoma kweli ila Tusibaki kua wasomi tusiokubali hali ya jamii kwasasa ikoje.
Katika kilimo kuna mambo yafuatayo
Nini ufanye
Kuna kilimo cha mbogamboga hii inafaida sana soko lake lipo mda wote na hasa kiangazi hiki. Bei ya mbegu ni rahisi mno haizidi elfu 5. Maeneo yapo unaweza tumia eneo dogo na ukalima kisasa ukapata faida vizuri sana.
Kuna kilimo cha nyanya yaani hekari moja unaweza kuvuna mpka ukachanganyikiwa kwanini hukujua mapema. Mfano Gairo Morogoro, Moshi, iringa. Maeneo karibia yote Tanzania nyanya inakubali niwewe tu kuchukua hatua.
Kuna ufugaji wa kuku wakienyeji au wakisasa jinsi wewe utakavyopendelea kulingana na eneo ulilopo pamoja na soko. Kuku wa kienyeji, kwanza gharama yake ya ufugaji ni rahisi unaweza kutengeneza banda lako lakawaida kabisa na ukafanikiwa kufuga ukafaidika. Acha kusubili kesho kesho amka chukua hatua.
Mungu atusaidie sana kufikiri.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu wabariki vijana.
Asante.

Upvote
2