Ushauri: Vyama vya siasa ndio vipewe haki ya kuitisha maandamano kwa uwajibikaji na matokeo ya maandamano

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
Kwako ,
Rais wetu Dkt. Samia Suluhu na Serikali kwa ujumla,

Nakusalimu kwa jina la JMT,

Nina ushauri wa kudhibiti hali ya tishio la maandamano la mara kwa mara. Katika matishio hayo inavyoonekana kwa nje , wananchi ndio wanayoratibu na wanayataka wao lakini ukweli ni kwamba maandamano hayo yanaratibiwa na vyama vya siasa na ili vyama hivyo vijiweke mbali na matokeo ya maandamano vinajifanya ni ya wananchi.

Ushauri wangu utajikita zaidi katika kufanya Siasa ilinde amani, kwa kuwa tunajua Siasa ni jumla ya shughuli na Maisha ya watu hivyo ninashauri kuwa na mabadiliko ya katiba au katika katiba mpya iweke wazi kuwa Chama Cha Siasa ndicho chenye mamlaka ya kuratibu na kuitisha maandamano hata yasiyo ya kisiasa nikiwa na maana ya kwamba kwa mfano kama madaktari au walimu wanataka kuandamana basi wakutane na uongozi wa Chama cha Siasa chochote wanachoonq kitawasaidia wawaeleze kusudi lao na kama wakiwaelewa Chama hicho ndio kitakuwa na jukumu la taratibu zote za maandamano ili ikitokea maandamano yakiwa ya Fujo basi Chama hiko kitawajibika. Nashauri hivi kwa sababu

1. Vyama vya siasa vinachochea Fujo mitandaoni na wanahamasisha maandamano bila wao kujitokeza kwa kukifanya ni ya wananchi hivyo kwa kuwa wananchi wanajua sapoti kubwa wataipata wapi.

2. Lengo ni kufanya Siasa ilinde amani kupitia vyama vya siasa , Nina amini vyama vya siasa vina jukumu kubwa kulinda amani hivyo kama vikitumika kulinda amani , vitasaidia kudhibiti maandamano ya kichochezi.

3. Ninaamini maandamano yakiratibiwa na kufanikishwa kupitia vyama , itakuwa ni rahisi kukiwajibisha Chama kwa matokeo ya baada ya maandamano na hivyo Chama hiko kitakuwa walinzi wa maandamano

4. Siasa ni jumla ya maisha ya watu hivyo hata kama mtu Hana Chama lakini anapotaka kuandamana ni kwa sababu ya hali na sera za kisiasa hivyo atumie Chama Cha Siasa kufikisha kero kama ni kupitia maandamano.

Baada ya ushauri huu kutekeleza ,nayaona haya kama matokeo

1. Jukumu la juu kabisa la kulinda amani kupitia maandamano litabebwa na vyama vya siasa na vyama vitabeba kwa tahadhari

2. Itasaidia Serikali kumjua mwenye maandamano na uwajibishaji wa zaidi.

Utaratibu wa Chama uwe wazi kuhusu Chama kukubaliana kusalati maandamano na kuwe na ridhio la pamoja na makubaliano ya kamati kuu ya Chama husika ambalo litawasilishwa kama kibali Cha kuomba maandamano hayo.
 
Mkuu Karilo, KARLO MWILAPWA , japo nia yako ni njema, ili kuwepo na uwajibikaji, sikubaliani na ushauri wako kwa Rais Samia, kwasababu, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kuandamana na uhuru wa kufanya mikutano ni haki za kikatiba zilizotolewa na katiba yetu kwa Watanzania wote, kitendo cha kushauri haki hizo zitolewe kwa vyama vya siasa tuu, huo ni ubaguzi na udikiteta!, Watanzania wanataka katiba bora na sio bora katiba!.

Kwa vile mikutano na maandamano ni haki, ila kila haki ina wajibu, vijana wetu Gen Zii, wao wanajua tuu kupigania haki zao lakini masikini vijana wetu, hawajui wajibu wao kwasababu hakuna yeyote, aliyewafundisha wajibu wao!, hivyo nimeshauri serikali yetu PostGE2025 - Pongezi Serikali Kudhibiti Maandamano, Pongezi Gen Z Kwa kutoandama. Kwa vile maandamano ni Haki, Gen Zii Wetu wafundishwe Kuandamana!
p
 
Kwa hiyo kama maandamano ya ushindi wa Simba na Yanga,Nayo yapewe vyama vya Siasa?
 
kwa mfano kama madaktari au walimu wanataka kuandamana basi wakutane na uongozi wa Chama cha Siasa chochote wanachoonq kitawasaidia wawaeleze kusudi lao na kama wakiwaelewa Chama hicho ndio kitakuwa na jukumu la taratibu zote za maandamano
Hii siyo sawa kwa sababu zifuatazo:

1. Watumishi wa umma kama hao walimu, madaktari, nk, Kikatiba hawatakiwi kuwa na upande kisiasa. Wakitakiwa kuchagua chama cha siasa cha kusimamia madai yao tayari watakuwa na misimamo ya chama husika, na madhara yake ni kama ya policcm ambao wamepoteza dira.

2. Wananchi wataanza rasmi kubaguliwa na kubaguana kwa misingi ya itikadi zao za kisiasa
 
Ahsante sana kaka mayalla, ninajua kwa sasa kuandamana ni haki ya kikatiba na ushauri wangu katikati nimezungumzia kuwe na mabadiliko ya katiba au katika katiba mpya
 
Kwa hiyo kama maandamano ya ushindi wa Simba na Yanga,Nayo yapewe vyama vya Siasa?
Yale ya Simba na Yanga sio maandamano ni mikusanyiko ya kusheherekea ushindi na maandamano yanataka kufikisha ujumbe maalumu, mikusanyiko ya namna hiyo hayana tatizo kwa sababu hayana dhamira nyingine tofauti na kusheherekea
 
Yale ya Simba na Yanga sio maandamano ni mikusanyiko ya kusheherekea ushindi na maandamano yanataka kufikisha ujumbe maalumu, mikusanyiko ya namna hiyo hayana tatizo kwa sababu hayana dhamira nyingine tofauti na kusheherekea
Na Kama wakajibiwa vizuri madai Yao na karudi Kwa furaha hao wa vyama,Yanahama kutoka maandamano na kuitwa Sherehe?!!
 
Akili mbovu kabisa, deep down unafaidika kwa lipi haswa na huu upumbavu unaoendelea?
Nafaidika kwa amani ndio maana na
Lengo la uzi wangu ni kufanya Siasa izungumze kwenye kero na changamoto kupitia vyama vya siasa na sio kuleta Siasa kwenye utumishi. Sauti za watu zisikike kupitia Siasa
 
Kwani chadema hakijafanya maandamno ya amani mikoa yote nchini Tanzania 2024?
 
Ahsante sana kaka mayalla, ninajua kwa sasa kuandamana ni haki ya kikatiba na ushauri wangu katikati nimezungumzia kuwe na mabadiliko ya katiba au katika katiba mpya
Hicho ndicho nisichokubaliana na wewe, kwa mujibu wa katiba yetu, binadamu wote ni sawa, na haki zinazotolewa kwenye katiba ni haki kwa watu wote, ushauri wako ni kushauri tuweke ubaguzi kwenye katiba mpya, hivyo tuwe na katiba baguzi?.
Naheshimu maoni yako, ila sikubaliani nayo, haki za kikatiba ni haki za watu wote.
P
 
Kwamba siku ndugu zako, jamaa na marafiki wamedhulumiwa haki sehemu wanahitaji kufikisha ujumbe lazima wamtafute mwenyekiti wa chama cha siasa? Aisee.
 
Kwamba siku ndugu zako, jamaa na marafiki wamedhulumiwa haki sehemu wanahitaji kufikisha ujumbe lazima wamtafute mwenyekiti wa chama cha siasa? Aisee.
Siasa ndio iwe njia ya kusikiliza na kufikisha kero na vyama vya siasa vihusike moja kwa moja kwa sababu Siasa ni jumla ya maisha ya watu na shughuli zao hivyo kama Kuna kero basi Siasa ndio zitoe majibu nje ya hapo hatari yake ni kubwa.

Vyama vya siasa vina jukumu kubwa la kufanikisha amanni bila makundi yenye milengo tofauti.
 
Naweza nikawa sifahamu vizuri ni haki ipi zaidi katiba inaizungumzia, ni haki ya maandamano au haki ya kukusanyika? Ninachozungumzia ni kuhusu kuandamana ,kama katiba inazungumzia kukusanyika na kuandamana kama jambo moja basi maboresho yafanyike kwenye haki ya kuandamana na iwe ni sharti kuitishwa na vyama vya siasa lakini kama ni kukusanyika haki hiyo ilindwe kwa kuzingatia sheria
 
Lengo la uzi wangu ni kufanya Siasa izungumze kwenye kero na changamoto kupitia vyama vya siasa na sio kuleta Siasa kwenye utumishi. Sauti za watu zisikike kupitia Siasa
Ni vizuri watumishi wa umma ambao siyo wanasiasa wasilazimishwe kuingia siasani kupitia kulazimika kutafuta usaidizi wa vyama vya siasa kushughulikia madai yao. Hao watumishi wana vyama vyao vya kitaaluma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…