Ushauri wa Benki ya kuweka akiba

Ushauri wa Benki ya kuweka akiba

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2015
Posts
9,558
Reaction score
12,335
Baada ya BOT kufuta benki 5 na kuona wananchi wanalia nje ya majengo ya benki kuwa akiba zao za fedha zimekwenda na maji,
Je ni benki gani nzuri kwa sasa zinafaa kuweka akiba ili kuepusha kasumba hiyo?!
 
Baada kuona yaliyotokea nimechonga kibubu hicho, ambacho kesho naeka kukomba akiba yangu yooote naweka humu
a812def5e040e407099062b0e107ac3b.jpg
 
Ingawaje mimi sio mwanauchumi au chochote karibu na hapo ila nadhani ni busara zaidi kuihifadhi fedha yako kwenye mzunguko fulani wa biashara wenye uhakika. Au kama una fedha za kutosha unaweza ukawekeza kwenye kitu fulani cha muda mrefu mfano shamba la miti nk (economists mnisaidie kuweka baadhi ya mambo sawa hapo)
 
ilivyofungwa ile ya Kule songea Mbinga community Bank ... hakuna aliyewalilia wale wamatengo wamepigwa kimya kimya ... wamekula 1.5M wametulia mitaji yao ya biashara na amana zao wanasubiri mfilisi akamilishe utaratibu na hawajapiga kelele popote....... sasa zimefungwa bank za ukanda wenu ndiyo mnagundua kuwa ni soo... vumilieni tu yatapita hayo
 
Back
Top Bottom