Ushauri wa biashara ya kuagiza vitu China

jerryempire

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
5,530
Reaction score
9,550
Habari,

Nimepitia kwenye mitandao mingi kama ebay, aliexpress na mingineyo ya kuagiza vitu toka China hivyo kuwa interested na kujaribu kuanza biashara hii.

Ombi langu ni ushauri/uzoefu/changamoto, ni biashara gani/bidhaa gani zinalipa kwa sasa kuanza nazo,ninatarajia kuuzia zaidi online.

Mtaji nmepanga kuanzia kwanza na 2m nione

Ahsanteni
 
1. Fungua account alibaba, aliexpres
2. Ni vizuri kulipa kwa kutumia credit/ debit card, ukitumia paypal ukitapeliwa huna means ya kurudisha michuzi yako.
3. Kabla ya kununua tumia muda kuchat na suppliers usinunue direct.
4.Nunue mzigo mdoko kwa kuanzia ili upate kujua vizingiti viko wapi.
4. Usijiulize masuala mengi wala usiogopo kuagizia , anza kuagizia kidogo mengine utayaelewa wakati unaagizia.
5. Wasiliana na supplier watatu mpaka wanne kwa bidhaa unayonunua, uone tafauti ya bei, kama bei zinatafautiana sana uliza masuala mpaka uridhike.
5. “You get what you paid for” huu ni msemo maarufu kwa china, usitegemee kupata mercedes wakati umetoa hela ya toyota corolla.
Kama unanunua aliexpress numua vitu ambavyo viko kwenye aliexpress direct, hivi una gurantee utavipata na jama kuna matatizo watakurudishia michuzi.

Sasa wewe llilobaki ni kujitosa tu, kama una masuala zaidi uliza tu.
 
Ukisha agiza unavipataje, yaani unavichukulia wapi vitu vyako?
 
Uwo ni uamuzi wako, mimi navichukulia Dubai, na kama uko TZ unavichukulia Tanzania, vinafikia Dar port, unakwenda kufanya clearance mwenyewe kama umechukua full container, kama mzigo wako hautimii container load, wanauingiza kwenye container la mfanyabiashara mwengine na watakupa details za kufuatilia, au unamfuata agent yeyote alieko TZ akusafirishie kutoka china.
Kama unasafirisha kwa ndege unatoa address yako nafikiri kwa huko ni address ya posta baadae posta watakuarifu ukauchukue, utaratibu wa huko nyumbani inabidi uufuatilie mwenye, unaweza kwenda posta au kwa mawakala kuwauliza.
 
Back
Top Bottom