jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
Mitambo kama ipi hiyo mkuuBiashara za huduma/services
Lete mitambo ya kufanya kazi mbalimbali haswa kwenye construction industry au Manufacturing.
Kama kawaida ya wabongo kunyimana connectionWamegoma
Mkuu we siunaagiza vitu China tupe connectionSawa
Unataka kuagiza nini mkuuMkuu we siunaagiza vitu China tupe connection
Mikanda ya tumbo,chupi,tight Za matako,vyomboUnataka kuagiza nini mkuu
Tumia Alibaba mkuuMikanda ya tumbo,chupi,tight Za matako,vyombo
Wanataka kuanzia pc nagap alibabaTumia Alibaba mkuu
Kulingana na supplier mtakavyo elewanaWanataka kuanzia pc nagap alibaba
Mzigo unachukua siku ngapi kufika tz.navip faida ipo? Ukilinganisha na kununulia kariakoo or ugandaKulingana na supplier mtakavyo elewana
Kwa meli siku 30-45Mzigo unachukua siku ngapi kufika tz.navip faida ipo? Ukilinganisha na kununulia kariakoo or uganda
Ukisha agiza unavipataje, yaani unavichukulia wapi vitu vyako?1. Fungua account alibaba, aliexpres
2. Ni vizuri kulipa kwa kutumia credit/ debit card, ukitumia paypal ukitapeliwa huna means ya kurudisha michuzi yako.
3. Kabla ya kununua tumia muda kuchat na suppliers usinunue direct.
4.Nunue mzigo mdoko kwa kuanzia ili upate kujua vizingiti viko wapi.
4. Usijiulize masuala mengi wala usiogopo kuagizia , anza kuagizia kidogo mengine utayaelewa wakati unaagizia.
5. Wasiliana na supplier watatu mpaka wanne kwa bidhaa unayonunua, uone tafauti ya bei, kama bei zinatafautiana sana uliza masuala mpaka uridhike.
5. “You get what you paid for” huu ni msemo maarufu kwa china, usitegemee kupata mercedes wakati umetoa hela ya toyota corolla.
Kama unanunua aliexpress numua vitu ambavyo viko kwenye aliexpress direct, hivi una gurantee utavipata na jama kuna matatizo watakurudishia michuzi.
Sasa wewe llilobaki ni kujitosa tu, kama una masuala zaidi uliza tu.
Uwo ni uamuzi wako, mimi navichukulia Dubai, na kama uko TZ unavichukulia Tanzania, vinafikia Dar port, unakwenda kufanya clearance mwenyewe kama umechukua full container, kama mzigo wako hautimii container load, wanauingiza kwenye container la mfanyabiashara mwengine na watakupa details za kufuatilia, au unamfuata agent yeyote alieko TZ akusafirishie kutoka china.Ukisha agiza unavipataje, yaani unavichukulia wapi vitu vyako?