Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Habari wakuu,
Natumai mmeunza vyema mwaka huu mpya. Nijikite kwenye mada yangu.
Mimi ni kijana ninaemaliza chuo mwaka huu 2021. Baada ya kuona changamoto ya ajira mtaani hasa kipindi kile cha likizo ya corona mwaka jana nimeona hata kupata kazi tu ya kujishkiza ili kusukuma maisha ni kazi mno.
Ile likizo ilinikuta sina kitu, na niliishi kwa tabu kidogo hadi kuimaliza ile likizo na kurudi kuendelea na chuo tena december mwaka jana.
Nimekuja kuomba ushauri kwenu ndugu zangu, mimi ni mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu hivyo nimeona ni vyema nikaanza kuweka akiba ili nikimaliza chuo niwe na kianzio naamini bado sijachelewa.
Lakini nimeona pesa kukaa tu bila kazi yoyote ya kujizalisha kwa takribani miezi 6 ni kazi kidgo hivyo naomba ushauri wa biashara yoyote ambayo inaweza kuzungusha pesa wakati bado nikiendelea kujichanga zaidi huku nikimaliza mwaka wangu wa masomo.
Nipo jijini Dar es salaam
Nina kiasi cha Tsh. 200,000/= tu.
Nawasilisha