Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote!

🤔🤭
 
Mkuu hauna hoja zingine badala ya kutuletea hoja ambazo zimezikwa kitambo?

Kwani hujaliona hilo deni la Taifa himilivu?
 
Nchi hii ishakuwa ya kitu kidogo. Nafsi yangu inanisukuma kukushutumu Pascal Mayalla kuwa umepewa kitu kidogo na akina Halima Mdee & Co kuja kuwaombea msamaha.

Ni hisia ZANGU tu lakini mkuu, sina ushahidi wowote.
Mkuu G4N , ni rukhsa kwa mtu yeyote kuhisi chochote, kuhusu jambo lolote, hivyo rukhsa kuhisi nimepokea chochote kitu kwa hawa wadada.

Ukweli ni mimi ni mtetezi huru wa haki wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo nawafanyia utetezi kwa kijitolea tuu, silipwi chochote na yeyote.
P
 
👏👏👏🛡️
 
👏👏👏👍
 
Paskal, ushauri mzuri kabisa ila kwa chuki, akili mbovu na roho mbaya za wale wanaume waliokosa ubunge 2020 hasa wale walishindwa sidhani kama watakusikiliza. Inaelekea Mbowe, Heche, Msigwa, Sugu waliumia sana waliposhindwa kurudi bungeni, wanajua utamu wake na nje ya bunge ni sawa kama kumtoa samaki majini
 

Unataka iachane nao vipi?

Walishaachanishwa mahakama long time ago..!

Labda ungeshauri CHADEMA ifute maamuzi yake ya kuwafuta uanachama kitu ambacho ni kigumu..

Hata hivyo, ilishatangazwa na chama kuwa wako huru kurudi chamani kwa kuomba uanachama upya kwa kufuata taratibu za kikatiba..
 
Walishafukuzwa wabebane huko WALIKOBEBWA

Mbona mnalazimisha huo mzigo mlioubeba wenyewe wapewe Chadema....pambaneni na hali zenu!!!
Wakifanya hivyo italeta shida kwa mwenendo wa chama maana kila
Wakifanya hivyo watajiweka katika hali ngumu ya kuendesha chama maana kila atakayefanya kosa atarejea kwa Covid-19 na viongozi watalaumiwa kwa upendeleo. Jambo la pili Covid-19 watakuwa untouchable na may even boast of it. Waendelee tu na msimamo wao. Tatu watawezaje kuwasamehe watu ambao wao wenyewe hawaonyeshi kukubali kwamba walikosea na hivyo hawaoni haja ya kuomba msamaha? Ni justification gani Chadema watatoa wakaeleweka kwa kufanya hivyo? Yaani Kila mtu atawapuuza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…