Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Kweli wewe naye mtu. Bado una utoto mwingi au kichwa bongo fleva. Maana mwenye hekima na busara hawezi ongea upuuz huu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond hajawahi kukataliwa acheni fixi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu mwenyewe hawezi kumsamehe shetani.
Kufikia hapo mungu kanifundisha kutosamehe, roho nzuri nishaona ni udwanzi, Diamond anaufala wake ila kwenye kutomsamehe mzee wake hajakosea, haiwezekani utelekeze familia hata wanyama pori wanatunza familia zao. (mimi nimekulia nyumbani malezi ya baba na mama ningetelekezwa sijui ingekuwaje).

Namkubali Malcolm X ila baada ya kuslimu akapata akili akasema
"Ima Muslim because its a religion that teach me to respect everybody and treat everybody right and it also teach me an eye for an eye and tooth for tooth"
mambo ya kusamehe sijui staying positive in a negative situations hapana aisee.
 
Baba mtu apambane na hali yake kama tu either
1.alimkana dai akiwa mdogo
2.aliwaita wachawi na kuwafukuza wasimuombe msaada wowote enzi anajiweza
3.alimtaka au kumshawishi mama dai aichoropoe mimba ya dai(hii style ya enzi na enzi eti itoe haraka)
4.hakumjali kijana wake enzi za utoton.

enyi wababa acheni kuwatelekeza watoto madhara yake ndo haya ya mzee mzima kulia kwenye media kila kukicha
 
Simpendi diamond ... lakini kwakuwa katika maisha yangu nilichagua kuwa positive ... katika hili niko kwenye upande wake ....

Majuzi nilikuwa na bishana na watu kuhusu suala hili hili tweeter ", na hatimae walielewa tu "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnakazana tu " oohh vitabu vya dini vime sema. .vitabu vya dini Vimesema"...... sasa kama baba aliyakimbia majukumu yake ya kulea' Mnauhakika gani kuwa diamond anajua hayo mafundisho yaliyopo kwenye vitabu vya dini"........,

Kwa sababu Ni jukumu la mzazi kuhakikisha kuwa anampeleka mtoto wake kuanza shule" iwe inayotoa elimu dunia au ya huko sijui ndio akhera"......., so kama hayo mafundisho hayajui", hamuoni kuwa hawezi kutambua umuhimu wa hicho mnacho muambia", na hapo hapo lawama tena zinarudi kwa baba huyo huyo maana alishindwa kumpatia mtoto wake elimu ili aweze kuyajua hayo mafundisho ya imani ".... so wakumlaumu ni huyo mzee sio domo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume leeni familia mnatelekeza watoto afu saizi unakuja tia huruma kwenye media pole sana baba diamond you weep what u have sawn gademn mkomage ....mnatelwkeza watoto wakikua na mafanikio ndo mnaleta pua zenu huku mnatia huruma heheheh

am better here
 
Hakuna kitu cha thamani hapa chini ya jua kuliko kusamehe..inakuweka huru,inavunja maagano ya kishetani,inaleta heshima,inakupa hadhi mbele za Mungu na wanadamu.
Daudi aliwahi kuandika Ee bwana Kama usingelirehemu,ni nani angesimama mbele zako?lakini kwako kuna msamaha ili wewe uogopwe"
Binafsi sishindwi kusamehe kosa lolote lile hata la mtu nisiyemjua..napendaga sana kusamehe kwa sababu inanipa furaha na amani.
NB:simanishi kuwa huwa sikasiriki,ila siwezi kuishi na kisasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nikuambie siku zote Mungu hatoi laana endapo mzazi haja timiza majukumu yake na mimi nakuambia na nimeshuhudia mzazi akikupa laana au akinung'unika basi kama kweli Mzazi alitimiza majukumu yake ya malezi lazima Kuna baya litamkuta mtoto, kilio cha mzazi Mungu anakisikia sana.

Hivi nikuulize Mondi leo angekuwa hana kitu huyu mzee angemtafuta?

Haya basi tufanye Mondi kakosea, lkn ukirudi kwa Doreen lawama ni zile zile mpaka akamtukana matusi makubwa kwenye kipindi cha Shilawadu, sasa ww hujiulizi mtu mmoja lkn anarudia kosa lile lile kwa watoto wawili tofauti ambao amezaa na wanawake tofauti, huoni huyu mzee ni type zile za kuzalisha na kutambaa.

Mimi nakuambia kama huyu mzee angekuwa responsible kwa Mondi na Doreen nina uhakika Mondi yangemkuta mabaya sana kwani laana ya mzazi haimalizi hata mwezi (nishashuhudia kwa watu watatu tofauti) lazima impate mtoto, lkn huyu mzee tokea aanze kulalamika ana miaka zaidi ya mitano lkn Mondi kila siku anazidi kutusua, kutoka kuwa mwanamziki mpaka CEO.

Kiubinadam na kidini hata mm napenda Mondi amsamehe mzazi wake, ila approach ya mzee hata mimi nisingemsamehe. Mimi mtaani Kuna mzee mmoja, mdogo wake alimtelekeza mtoto, babu wa huyu mtoto aliwafuata ili kujua hatma ya mwanae na mjukuu wake lkn walimjibu hovyo nakumfukuza. Yule mtoto kakua kamaliza chuo, baba yake kaanza kumfuata babu yake ampatanishe na mwanae alitimuliwa na mpaka akatumia njia kibao akachemka. Kaka yake huyo jamaa kamfuata mzee wangu, sababu baba na babu wa huyu binti wanaheshimiana sana akatafuta na wazee na ndugu ambao yule babu anawaheshimu wameenda wakaongea na kuyamaliza.

Tatizo huyu mzee anakosea kwenda kwenye vyombo vya habari, alafu anaonekana hata yy mwenyewe ni bado anatabia za kisela (nineshamuona ktk interview mbili) na ndio maana hata yy mwenyewe anashindwa kuwatafuta watu au ndugu ambao Mondi na mama yake wanawaheshim ili wamsaidie ktk kupatana na mwanae. Lakin kama angeitumia hii njia kimya kimya nina uhakika wangemsamehe. Ila hii kila siku kwenye vyombo vya habari hata mimi simkubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…