Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Timizeni wajibu wenu kama maandiko hayohayo yanavyotaka,munatelekeza ili muje kujificha kwenye msamaha,alichomfanyia mwanawe,ndicho anachofanyiwa.
Amepanda na leo anavuna.,hili litufundishe wanaume nanhata wanawake kutotelekeza watoto,lea kwa uwezo wako.
Sure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.

Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.

Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.



Anasubiri afariki ili afanye mazishi ya kifahari, wakati dini yake pia haimruhusu kufanya mazishi ya kifahari, kikubwa ni kumstiri maiti,
ipo siku atajutia
 
Diamond akumbuke bila kujali Baba kakosa nini ila ni maamuzi yake (Baba) ndio yamesababisha yeye kuwepo.

Huwezi jua ni magumu gani alipitia mpaka kukutana na Mama, na kama angekata tamaa wala kusingekuwa na kiumbe wa kuitwa Nasib.

Huenda hata jamaa alilazimika kuiba au labda aliuza kitu ili Mtoto (ambaye sasa hivi ndio Mama Diamond) aingie kingi, Mondi mwenyewe anajua gharama za kupata Totoz.
 
Na wewe Diamond, hujui kama charity begins at home?? unaanzaje kusaidia watu baki usio na nasaba nao na kumuacha mzazi wako akidhalilika kwenye media??

Your a big man now and have kids too don't forget that KARMA IS A DOG.
 
Diamond akumbuke bila kujali Baba kakosa nini ila ni maamiuzi yake (Baba) ndio yamesababisha yeye kuwepo.

Huwezi jua ni magumu gani alipitia mpaka kukutana na Mama, na kama angekata tamaa wala kusingekuwa na kiumbe wa kuitwa Nasib.

Huenda hata jamaa alilazimika kuiba au labda aliuza kitu ili Mtoto (ambaye sasa hivi ndio Mama Diamond) aingie kingi, Mondi mwenyewe anajua gharama za kupata Totoz.
Mi siamini kama kumzaa mtoto ni kumsaidia ,mzazi amemzaa mtoto Kwa Raha zake
 
Tatizo ni Visasi vya Wanawake.....
Usikute hata chanzo cha Baba kuondoka ni Mama......!
........Mama keshachimba Mkwara, kuwa nikisikia umemsaidia Baba yako nakuachia radhi!!
 
Ambao mmebahatika kuishi na wqzaz wenu wote wawil mtaona mond anamakosa sana Ila hamjui maumivu yake ya maisha bila mzazi au masha ya kukataliwa na mzazi

Hii ni kawaida sana kibinadamu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena afadhali huyo Mond mzazi wake aliondoka kwenye maisha yake lakini mimi baba yangu alikuwepo and he did nothing, unamuomba msaada anakukata jicho kali kisha anakupush na kuondoka hahaha alisahau kua kazi zina mwisho na mwili huchoka, mwanzo tulimkunjia sana kwenye kikao alisema "Sorry" neno moja tu lililainisha mioyo yetu na sasa tupo nae fresh tu,

Msimpe kichwa Mond angalau yeye anajiweza saaa hivi kwa hiyo ni jambo la kushukuru, kukataliwa na baba ake ndio kulimpa nguvu ya kufight na sasa kafika hapo alipo pengine angekuwepo kwenye maisha yake asingekua hapo alipo.

Ajue pia anavyoendelea kumkunjia baba ake na akifa bila kuwekana sawa basi hiyo laana itaitafuna kizazi chake yaan atashangaa atakuja kuteswa na mmoja wa watoto wake au hata mjukuu wake na itaendelea hivyo hivyo.
 
watoto waliotelekezwa na baba zao wanakujaga kutusua sijui kwa nini...diamond amshukuru baba yake kwa kumtelekeza ukute asingemtelekeza asingepambana kufikia hapo. Sijasema ampe hela, mzee bado ana nguvu kabisa yule
 
Back
Top Bottom