Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Hujajua maumivu ya kukataliwa na mzazi wewe tena hilo neno la kumdharau futa.
Ni maumivu yasiyoelezeka wewe unazungumza tu kwa sababu ulipata malezi ya wazzi wote.

Kupewa pesa si tatizo yule mzee pesa anapata, tatizo ni msamaha ni kitu kigumu sana mwanadamu kukitoa, haihitaji media ili kupata msamaha anahitaji wasuluhishi shauri yake.
Ndugu uko timamu kweli kichwani ama haukifahaumu unachokiongelea!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe endelea kukarili tu hizo Hekaya " Maisha ni zaidi ya hivyo unavyo fikiria
Hakuna kitu cha thamani hapa chini ya jua kuliko kusamehe..inakuweka huru,inavunja maagano ya kishetani,inaleta heshima,inakupa hadhi mbele za Mungu na wanadamu.
Daudi aliwahi kuandika Ee bwana Kama usingelirehemu,ni nani angesimama mbele zako?lakini kwako kuna msamaha ili wewe uogopwe"
Binafsi sishindwi kusamehe kosa lolote lile hata la mtu nisiyemjua..napendaga sana kusamehe kwa sababu inanipa furaha na amani.
NB:simanishi kuwa huwa sikasiriki,ila siwezi kuishi na kisasi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume ni Mkulima anaye miliki mbegu",(sperm) ambazo huwa anazipanda kwenye shamba lake ambalo ni mwanamke" na( kutunga mimba)

Unapokuwa mkulima Inamaana kwamba tayari unakuwa katika sifa ya u-bwana shamba", ile mbegu ambayo umeipanda shambani ", ili iweze kuchipua (kuzaliwa) na kisha kukua mpaka kufikia hatua ya kuzaa matunda " Ambayo yataweza kukunufaisha " Yakupasa ukiwa kama mkulima kusimamia majukumu yako vyema nakuhakikisha mbegu hiyo inapitia katika hatua zote salama " kama kuimwagilia maji mbolea kuliandaa shamba ili liweze kuwa na mazingira rafiki kwa mbegu hizo (Matunzo)

Baada ya mbegu kuchipua (mtoto kuzaliwa) nyinyi wazazi mnapaswa kuwekeza juhudi zenu za matunzo katika mbegu (mtoto) hiyo ili iweze kustawi vyema ..

Namaanisha mtoto anayo haki yakupatiwa malezi toka kwa wazazi wake ..malezi hayo yakiwa ni pamoja na zile basic needs zote " haki yake ya msingi ya kupata elimu dunia' elimu ya mafundisho ya kiroho ' na kumsaidia mambo mbali mbali ambayo yataweza kumsaidia kuzitimiza ndoto zake"..........., itakapo tokea mzazi ukashindwa kutekeleza kuyatimiza machche katika haya " kutokana na ufinyu wa maisha " basi haupaswi kuikimbia family yako unapaswa kuwa nayo huku ukiendelea kuionyesha upendo " kwa sababu kabla ya yote hayo kitu kikubwa mnoo ambacho watoto wana kihitaji toka kwa wazazi wao ni upendo kabla ya chochote", watakapo kuja kukua watatambua kwamba ulishindwa kuwa timizia baadhi ya mambo fulani kwakuwa haukuwa na kipato ... ila hiyo haikuwa sababu ya wewe kuweza kushindwa kuwaonyesha upendo wako kwao ''------,

Ila ukijiroga na kuwatelekeza aisee", ikitokea hapo baadae watakapo kuja kufanikiwa usirudi kwao tena"--- kwa sababu tayari utakuwa umeshapoteza ile sifa ambayo anapaswa kuwa nayo mzazi ambayo ni upendo ",Utakuwa hauna tofauti na mkulima aliyepanda mbegu zake shambani kisha akalitelekeza na kuliacha likiwa na magugu " halafu baada ya miezi kadhaa anarudi tena kwenye lile shamba kwa minajili ya kuvuna yale mazao ....

Kwanza mtu hauoni haya " Mtoto umemzaa bila ya ridhaa yake", mmemzaa kwaajili ya starehe zenu' Haya kaja duniani pia badala ya kumlea na kumtunza " mnaanza kumpitisha kwenye nazingira ya tabu na shida wakati yeye hakuwaomba mumzae " wala hakuwaambia kuwa anashida ya kuja duniani "

AISEE TUKIWA KAMA WAZAZI TUSIMAMIE MAJUKUMU YETU TUACHE UFALA.. HALAFU KAMA HAMTAKI KULEA HUWA MNATIA MIMBA ILI IWEJE"..... hivi huwa mnachulia poa " Una mleta mtu duniani haunpatii mazingira chanya " Tabu anazo zipitia katika maisha hivi mnachukulia poa eeh" Hivi kuna asiye jua kuwa maisha huwa yanaumiza" Yamejaa tabu na misuko suko kibao"... kama haujajiandaa kuwa mzazi bora kwanini umlete kiumbe duniani aje ateseke".......!? Imagine huyo mzee hata kumsomesha diamond haja msomesha which means kama asingekuwa na kipaji cha kuimba sasa hivi angekuwa boda boda".... hivi kweli angapaza shingo na kuanza kumlilia lilia shida kama anavyo fanya hivi sasa"..........!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro unachosha aosee ili gazeti lote la nini apa aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.

Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.

Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.

Hata kama siendi kanisani wala msikitini siwezi kuunga mkono kitendo kama hiki yaani baba yako mzazi hana hata hela ya matibabu anabangaiza halafu ww unagawa bima bure kwenye show za birthdays sijuw kwa watu pori kutafuta sifa kama si laana ni nn?
Ww ugomvi wa baba yako na mama yako ww unakuwasha nn?
Tupo tulotelekezwa had na mama wazazi lakn inapofikia habar ya mzaz ni mzaz hayo yote tunatupilia mbal maana tunajua nenda uendako sikio halitokuja kuzidi kichwa!!!hatuombei ila likitokea la kutokea utashangaa watu wanaongozana na maspika na makamera for show off!!!!!!! Watu had kuchomwa na majimoto tumechomwa lkn kwa wazaz hewala tunafurahia uwepo wao maana huwezi kubadilisha k2 hapo maana wazaz si marafiki useme utabadilisha!!!!!
Yaan inauma sana mzee wako hali yake ni kama vile halafu uko busy kujirekodi video ukihesabu mapesa na malaya zako yaan alokuloga nahisi alishakufa!!!!!!
 
Ndugu uko timamu kweli kichwani ama haukifahaumu unachokiongelea!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakijua vyema sana, yani maumivu unayoyajua ya kuachwa kimapenzi na mtu unaye mpenda hayafikii hata theluthi ukija tambua haya ya diamond.

Psychologist wenyewe wanatambua ugumu wa hili.

Kapige mimba sehemu alafu potea ukapigike baada ya miaka 23 kamfuate huyo mtoto akikusamehe nahama hii dunia. (Sumu atakayokuwa analishwa ni zaidi ya black mamba inayouwa within 1hour)
 
Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.

Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.

Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.
Umefikiria iwapo Diamond angekuwa maskini, huyo mzee angemjali mwanae?
 
Kwanza nikuambie siku zote Mungu hatoi laana endapo mzazi haja timiza majukumu yake na mimi nakuambia na nimeshuhudia mzazi akikupa laana au akinung'unika basi kama kweli Mzazi alitimiza majukumu yake ya malezi lazima Kuna baya litamkuta mtoto, kilio cha mzazi Mungu anakisikia sana.

Hivi nikuulize Mondi leo angekuwa hana kitu huyu mzee angemtafuta?

Haya basi tufanye Mondi kakosea, lkn ukirudi kwa Doreen lawama ni zile zile mpaka akamtukana matusi makubwa kwenye kipindi cha Shilawadu, sasa ww hujiulizi mtu mmoja lkn anarudia kosa lile lile kwa watoto wawili tofauti ambao amezaa na wanawake tofauti, huoni huyu mzee ni type zile za kuzalisha na kutambaa.

Mimi nakuambia kama huyu mzee angekuwa responsible kwa Mondi na Doreen nina uhakika Mondi yangemkuta mabaya sana kwani laana ya mzazi haimalizi hata mwezi (nishashuhudia kwa watu watatu tofauti) lazima impate mtoto, lkn huyu mzee tokea aanze kulalamika ana miaka zaidi ya mitano lkn Mondi kila siku anazidi kutusua, kutoka kuwa mwanamziki mpaka CEO.

Kiubinadam na kidini hata mm napenda Mondi amsamehe mzazi wake, ila approach ya mzee hata mimi nisingemsamehe. Mimi mtaani Kuna mzee mmoja, mdogo wake alimtelekeza mtoto, babu wa huyu mtoto aliwafuata ili kujua hatma ya mwanae na mjukuu wake lkn walimjibu hovyo nakumfukuza. Yule mtoto kakua kamaliza chuo, baba yake kaanza kumfuata babu yake ampatanishe na mwanae alitimuliwa na mpaka akatumia njia kibao akachemka. Kaka yake huyo jamaa kamfuata mzee wangu, sababu baba na babu wa huyu binti wanaheshimiana sana akatafuta na wazee na ndugu ambao yule babu anawaheshimu wameenda wakaongea na kuyamaliza.

Tatizo huyu mzee anakosea kwenda kwenye vyombo vya habari, alafu anaonekana hata yy mwenyewe ni bado anatabia za kisela (nineshamuona ktk interview mbili) na ndio maana hata yy mwenyewe anashindwa kuwatafuta watu au ndugu ambao Mondi na mama yake wanawaheshim ili wamsaidie ktk kupatana na mwanae. Lakin kama angeitumia hii njia kimya kimya nina uhakika wangemsamehe. Ila hii kila siku kwenye vyombo vya habari hata mimi simkubali.
Mzee aende zile ofisi za pale karume yataisha faster[emoji28][emoji28]

Nimekuelewa vyema mkuu.

Ni wazi kuwa mzee huyu ana matatizo yake, tena makubwa tu. Hana zile busara za utu uzima. Angeweza kutafuta watu wenye heshima zao ili wamsaidie. Kuongea mara kwa mara kwenye media kwamba watoto wake hawamsaidii, wakati inajulikana wazi kuwa hana haki ya kusaidiwa pia inaongeza hasira.

Mawazo yangu mimi ni kwamba, kuendelea na hali hii hakumsaidii chochote Diamond, sana sana kunamuaibisha tu baba yake na kumvunijia heshima yeye mwenyewe (devided opinion). Anaweza akamsaidia kama anavyowasaidia wanajamii wengine asio wajua na maisha yakaendelea. Kwanza yeye mwenyewe anaanza kupata lawama sasa hivi, kutoka kwa mama za watoto wake, kwamba hatimizi majukumu yake ipasavyo.
 
Platnumz hajafanya fair,Ila Kwa wazazi Pia unapokuwa na nguvu angalia nguvu zako zisiwe dhidi ya familia yako,huna kitu admit tu Kwa familia yako kwamba Mimi napumulia gesi a suala la kutelekeza familia,ipo siku utakuja kuwa mnyonge tu na wale uliowabeza watakuwa na nguvu kuliko wewe,utawapigia goti tu na Mungu atakuweka hai Hadi unabii utimie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom