severinembena
JF-Expert Member
- Jun 2, 2018
- 2,435
- 2,402
Kama baba yangu angenitelekeza nisingemsamehe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Diamond hajaingilia huo ugomvi ndio maana Hana tatizo na mtu,MWANAUME RIJALI HAWEZI KAMWE KUINGILIA MAAMUZI YA UGOMVI WA WAZAZI WAKE.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli , yaani uzae mtoto umtelekeze halafu useme hakosei ? Mzazi ndio ana jukumu la kumtunza mtoto wake kuliko mtoto kumtunza mzaziMKUBWA HAKOSEI SIKU ZOTE HADI KUFA KWAKO.
BABA NI BABA NA HATAKUWA MTOTO NA NI YEYE PEKEE DUNIANI KOTE.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hujajua maumivu ya kukataliwa na mzazi wewe tena hilo neno la kumdharau futa.
Ni maumivu yasiyoelezeka wewe unazungumza tu kwa sababu ulipata malezi ya wazzi wote.
Kupewa pesa si tatizo yule mzee pesa anapata, tatizo ni msamaha ni kitu kigumu sana mwanadamu kukitoa, haihitaji media ili kupata msamaha anahitaji wasuluhishi shauri yake.
Mkuu ningekua mimi ndio uyo Baba Diamond nisingemtafta wa nini! Nitahesabu2 kua ni kama vile nilipiga punyeto, Diamond uyo kajazwa akili na mama yake, mwanamke ni ibilisi mbaya sana,Wewe utakuwa umelelewa na single mother,wanawake ni watu wabaya sana,sasa mama amefanikiwa kumjengea Diamond chuki kwa baba yake,je Diamond kwa imani ya dini yake kutokusamehe atapenya kwenye pepo gani?maana hata angezidi kuwa na pesa kiasi gani,mbele za Mungu he is useless...
Sent using Jamii Forums mobile app
Diamond ana moyo mgumu sana
DIAMOND MWENYEWE MARA YA MWISHO KUWAONA WATOTO ZAKE ILIKUWA NI LINI VILE?Sio kweli , yaani uzae mtoto umtelekeze halafu useme hakosei ? Mzazi ndio ana jukumu la kumtunza mtoto wake kuliko mtoto kumtunza mzazi
Huyo hana helaYule queen darling lipo lipo tu, sijui na yeye ana bifu na baba yake
Sent using Jamii Forums mobile app
KUCHUKUA MAAMUZI YA KUMCHUKIA MZAZI MMOJAWAPO NDIYO KUINGILIA KWENYEWE HUKO KWA UGOMVI WA WAZAZI WAKE.Diamond hajaingilia huo ugomvi ndio maana Hana tatizo na mtu,
Yes , kama YY Baba diamond alivyomdharau mwanae wakati Yuko mdogoMimi kama ningekua ndio Baba Diamond nisingemtafta wala nisingeenda uko cjui kwenye Media, wa kazi gani? Mtu akikudharau awe mwanao awe ndugu awe jirani hta awe nani katika nchi hii na ww mdharau2, kwani uyo Diamond ndio mtoa Riziki!, kwanza uyo Diamond wenu hana Dini
Sent using Jamii Forums mobile app
Hana hela anaishije ?
Huyu jamaa hana imani na haamini Mungu
Anaishi anavyoona yeye ni sawa
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Unajua kumzaa Mtu sio kusaidia maana mtoto hata hasingezaliwa kwake sio tatizo,KUCHUKUA MAAMUZI YA KUMCHUKIA MZAZI MMOJAWAPO NDIYO KUINGILIA KWENYEWE HUKO KWA UGOMVI WA WAZAZI WAKE.
LAITI ANGEKUWA NI MWENYE HEKIMA, ASINGETHUBUTU KUMCHUKIA BABA YAKE MZAZI KAMWE SABABU KUPITIA HUYO BABA YAKE MZAZI NDIYOMAANA KAZALIWA DUNIANI.
KWANI MAMA YAKE DIAMOND ALIJITUNGIA UJAUZITO PEKE YAKE BILA KUJAMIIANA?
MZAZI NI MZAZI TU HAIJALISHI ALIKUTELEKEZA, ALIKUWA MCHAWI, JAMBAZI AU TABIA MBAYA YA AINA GANI MAANA MUNGU NDIYE MLIPIZA KISASI PEKEE.
NA KWA TAARIFA YAKO FIMBO/ADHABU/MALIPO YA MUNGU HUWA NI MACHUNGU SANA KULIKO YA BINADAMU.
SO DIAMOND NI MTU TU KIMWILI LAKINI KWA KITENDO CHA KUMTENGA BABA YAKE, HANA CHEMBE CHEMBE ZA UTU WALA UBINADAMU HATA 0.1%
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nakijua vyema sana, yani maumivu unayoyajua ya kuachwa kimapenzi na mtu unaye mpenda hayafikii hata theluthi ukija tambua haya ya diamond.
Psychologist wenyewe wanatambua ugumu wa hili.
Kapige mimba sehemu alafu potea ukapigike baada ya miaka 23 kamfuate huyo mtoto akikusamehe nahama hii dunia. (Sumu atakayokuwa analishwa ni zaidi ya black mamba inayouwa within 1hour)
Point mkuuNaandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.
Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo. Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!
Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.
Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.