Ushauri wa bure kwa abiria wa Bodaboda; Usipande bodaboda kama...

Ushauri wa bure kwa abiria wa Bodaboda; Usipande bodaboda kama...

Nchi zilizoendelea zilishapiga marufuku haya matakataka mjini.

Kwanza zinachafua mji, zinaongoza kwa kuleta ajali na kuua vijana.

Godbless lema alisema vyema kabisa, Bodaboda ni laana.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Bodaboda ziendelee kupewa airtime maana fikiria maelfu ya vijana waliojiajiri kwenye bodaboda wakiwepo mtaani bila ajira.Vibaka na majambazi wataongezeka
 
Siku ya ajari hutoijua japo precautions Ni muhimu Sanaa...

Yes,
Mimi Ni muhanga wa hizi ajar muda huu napo andika ndio nimeanza kujaribu kusimamia mguu (mazoezi ya kukanyagia mguu)

Hofu, woga kwenye kukanyagia japo Nina CRUTCHES Ila mdogo mdogo with time ntazoea..

NB.
Sito panda tena USAFIR WA BODABODA
Pole sana Mkuu
 
-Boda boda kanyoa kiduku
-bodaboda ana kandambili/yebo
-Bodaboda kavaa pensi
-Bodaboda anayekuita kwa makelele
-bodaboda yenye mziki
-Bodaboda aliyevaa singlendi.

Kimbia fasta.
 
Kama unatumia Bodaboda hasa maeneo ya MJINI pitia hapa!

1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii

2. Usipande pikipiki ambayo dereva hajavaa Kofia/helmet
Ile kofia inakioo kinachozuia wadudu wanaoingia machoni na hata vumbi anapopishana na magari makubwa; Fikiria boda anakimbia KMS 70, halafu wadudu wamuingie machoni; ushukuru sana Mungu kama hutaishia kwenye mtaro au hata kugongwa...

Ushauri: Vile vioo vya pembeni vyote viwili havizidi shs 10,000 hivyo kama una bodaboda wako, unaweza kumnunulia/kumkopesha. Kofia ngumu ya kawaida ni kwenye shs 20,000=

Mwisho: Ukiona pikipiki ipo ovyo ovyo (haina sifa), ujue na muendeshaji yuko hivyo hivyo, uamuzi ni wako!

-
Thanks
 
Namba 1 hiyo muhimu sana aisee mie usafiri wangu ni pikipiki yaani naendesha mwenyewe kwenda kwenye shughuli zangu ila hawa bodaboda ambao wameamua kung'oa side mirror ni moja ya changamoto kubwa sana aisee ajali muda wowote usipokuwa makini anakusababishia na wapo wenge sana ila na huwezi kukuta boda anayejiheshimu kang'oa side mirror
Hivi kwanini wameng'oa? Hawataki usumhufu wa kuangalia nyuma au?
 
105: Usipande bodaboda yenye mziki mnene ni hatari sana. Unaweza kujikuta ndani ya tairi za semi au tipa
 
Kwa wa Arusha usipande boda boda Isio kua na taa[emoji81][emoji81]wahuni wana chomoa taa Og .wana weka mishumaa kabsa ile
 
FB_IMG_1711899724152.jpg
 
Back
Top Bottom