Ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima: Ukivuliwa nguo, ukabaki utupu! Ustaarabu ni kuchutama!

Ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima: Ukivuliwa nguo, ukabaki utupu! Ustaarabu ni kuchutama!

Wanabodi,

Mimi ni mkazi wa Jimbo la Kawe, Mbunge wetu, Mhe. Askofu Josephat Gwajima, japo ni mtu mchapakazi na mkweli sana, ila tatizo lake ni mtu wa maneno mengi, ahadi nyingi ambazo baadhi bado hazijatekelezwa.

Japo alipanga kuzitekeleza awamu ijayo, lakini kukatokea bahati mbaya, mdomo umeponza kichwa!, kwa kuusema ukweli mchungu ambao watu wenye nguvu na mamlaka, hawapendi kuusikia
, ukweli huo mchungu umemfanya ameteleza na kuanguka kwenye tope zito, hivyo amevuliwa nguo!.
Ukivuliwa nguo, Chutama!.

Hivyo imetokea amevuliwa nguo hadharani na kubaki mtupu!, uchi wa mnyama!. Dawa pekee ya kumnusuru na aibu na kumtunzia kaji dignity kadogo alichobakiwa nacho, Mbunge wetu wa Kawe na MNEC wa CCM, Baba Askofu Dr. Josephat Gwajima, ni kuchutama tuu!, kujisetiri!.

Miongoni mwa sifa zake kuu za pekee, Askofu Gwajima, zilizomfanya ateuliwe kuwa mgombea wa Kawe ni hiyo sifa ya kuusema ukweli no matter what, na akitibuliwa ni
ni mzee wa kuliamsha dude!, na hua analiamshia kanisani kwake katika ibada zake za siku za Jumapili.

Kuna vitu fulani mimi navijua lakini sivisemi, hivyo namshauri mbunge wangu, Askofu Gwajima, this time around, asiliamshe DUDE!, na badala yake aendeshe tuu ibada yake kama kawaida as of nothing happened!, atanishukuru!

Najua kuna wengi wangetamani kumuona akiliamsha DUDE, sii busara kuliamsha DUDE this time around kwasababu fulani!.

Kuna type fulani ya watu ni impulsive, ukimprovoke, anaprovokika, analipuka!, lakini kumbe hawajui kuwa kumbe sometimes kunyamaza kimya ni jibu kubwa na zuri kuliko kulipuka!.

Hadithi ya Kuoga Mtoni na Nguo Kutokomea!
Kuna simulizi ya watu wawili waliokuwa wanaoga mtoni.
Kuogo mtoni ni unavua nguo zote unabaki kama ulivyozaliwa.

Kumbe yule jamaa anayeoga ni kichaa! kijiji kizima wanamjua huwa anatembea hivyo kama alivyo zaliwa!.

Mara yule jamaa akachoropoka kwenye maji hapo mtoni, akaenda kuzichukua nguo zote za yule jamaa!.

Ungekuwa wewe ungeamua nini?.
1. Kwasababu wewe ni fighter, huwezi kuacha mtu akuchezee, hivyo utaamua kutoka kwenye maji na kumkimbiza mwizi wako kuokoa nguo zako ambazo ni haki yako?

2. Kuchutama, na kuziachia nguo ziende!, japo utaonekana zoba, jinga, hujui kupigania haki yako, utachekwa na kudharaulika jitu lioga, linashindwa kukimbiza mwizi!.

Uamuzi huu wa kuchutama ndio uamuzi sahihi na wa busara!.

Je tumchagize Askofu Gwajima aliamshe DUDE au achutame?.

Paskali
Porojo zote hizi hujajibu hoja hata moja unabaki kumshambulia bila kujibu hoja zake
 
Mayalla=Buku saba

Mayala wewe ni moja ya watu wanaong'ata na kupuliza huna unachokisimamia isipokuwa unafki kiufupi unazeeka vibaya na hata hizo teuzi unazotaka hutapata sababu wewe ni mnafki
Mtu akiwa neutral mnasema ni mnafiki, mie namuelewa sana Paskali anaeleza hali ya mambo pasipo kuegemea upande flani
 
Wanabodi,

Kuna vitu fulani mimi navijua lakini sivisemi, hivyo namshauri mbunge wangu, Askofu Gwajima, this time around, asiliamshe DUDE!, na badala yake aendeshe tuu ibada yake kama kawaida as if nothing happened!, atanishukuru!

Najua kuna wengi wangetamani kumuona akiliamsha DUDE, sii busara kuliamsha DUDE this time around kwasababu fulani!.
Paskali
Barua kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya inasomeka kama ifuatavyo:-

KUFUNGWA KWA SHUGHULI ZA KANISA LA GLORY OF CHRIST CHURCH - KANISA LA UFUFUO NA UZIMA

Chini ya Kifungu cha 17(b) na kifungu cha 2 cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 kama kilivyorekebishwa na kifungu cha 39(b) cha Sheria ya Marekebisho Mbalimbali ya Sheria Namba. 3 ya Mwaka 2019

Tafadhali, rejea somo tajwa hapo juu.

2. Katika siku za hivi karibuni, kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, umeonekana ukiwa katika mimbari ya Kanisa la Glory of Christ Church @ Kanisa la Ufufuo na Uzima, ukitoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi. Vitendo hivi ni kinyume cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337na vinaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.

3. Kwa Mamlaka niliyopewa, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia inafuta usajili wa Glory of Christ Church @ Kanisa la Ufufuo na Uzima, kuanzia leo tarehe 02 Juni 2025. Hivyo, unatakiwa kusitisha shughuli za Kanisa lako mara moja.

4. Chini ya kifungu cha 19(1) cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, Kanisa lina haki ya kukata rufaa juu ya uamuzi huu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia kwa Katibu Mkuu, ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya barua hii.

5. Kwa Amri ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia.

Asije kusema hakujua au hakuambiwa kabla!, watu muwe mnasikiliza ushauri!.
P
 
Asije kusema hakujua au hakuambiwa kabla!, watu muwe mnasikiliza ushauri!.
P
Binafsi ile siku ya kwanza baada ya tamko lile nilimpigia simu Gwajima nikamwambia CCM ni mwenyekiti na mwenyekiti ndiye CCM! Nikamkumbusha tena waliowahi kushindana na kiti cha enzi na walipoishia! Nilimkumbusha yeye bado ni mwanaCCM waliyemhifadhi kwa mengi!!

Kwa Yale yaliyokua yamepangwa yafanyike before and post election Samia ameonesha uanamke wa shoka!
 
Back
Top Bottom