Mhe. Mpina nimekuona kwenye clip na pia kwenye mitandao ya kijamii kuwa unashawishiwa na ACT- Wazalendo kuwa ugombee nafasi ya Urais kupitia Chama hicho. Nakupa ushauri wa bure. ACHA KABISA wazo hilo. Kama unataka cheo chochote kupitia siasa gombea nafasi ya ubunge hata kwa kupitia Chama chao.
Wanachotaka ACT- Wazalendo kutoka kwako pindi utakapogombea nafasi ya Urais ni viti maalum vya akina mama kule Bungeni. Wana uhakika ukigombea nafasi ya Urais kuchuana na Mhe. Samia unaweza kupata angalau asilimia 30 ya kura zote na hii itawawezesha kuwa Chama Kikuu cha upinzani na kuwa na viti maalum vingi kwa akina Mama kule Bungeni. Kwa hakika Mhe. Samia huwezi kumshinda ila hawa wanataka kukutumia tu kwa manufaa yao.
Kaa nao mezani na uwaambie bila 3bn/= hiyo kazi haiwezekani. Wasije wakakutumia tu baada ya uchaguzi wanakutupa na kukusahau.
Nawasilisha.