Mhabarishaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2010
- 1,007
- 600
Sitta, ninakupa ushauri wa bure, baada ya kuwa umechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum la Katiba. Tatizo lako kubwa, ni kwamba, you talk too much! Kificho ameweka standard mpya ya Spika (Mwenyekiti), so be careful, au siyo kazi yako nzuri ya nyuma inaweza kuingia mchanga.
Biblia inasema katika MITHALI 10:19,"Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili." Kificho yuko makini, hasemi maneno mengi, na ni mwangalifu sana katika kuchagua maneno ya kuzungumza.
Mind you, kwa kila jambo sasa, unapimwa katika mizani na kulinganishwa na Mwenyekiti wa muda, Kificho, na wala siyo Anna Makinda! Watu wengi wanatarajia kwamba Mwenyekiti wa kudumu, atakuwa na uwezo na hekima zaidi, kuliko Mwenyekiti wa muda!
Kumbuka kwamba kuanzia sasa, kila neno lako moja, lina tafsiri elfu moja, kwa maadui zako, na kwa mashabiki wako wa zamani! Neema ya Mungu ikufunike!