mi napenda kuangalia ukulima wa mazao mbalimbali. kuhusu ndizi nikapata habari zilizonipendeza nikasema nishirikiane nanyi.
ukipanda ndizi leo itachukua kati ya miezi kumi hadi kumi na mbili kuzaa mkungu. pia itategemea hali ya maji maana ndizi zinahitaji maji mengi sana. ukishuvuna mkungu huo mmea unaukata na itachukua miezi mingine kama hiyo kwa machipukizi ya ndizi kuvunwa. kuvuna huku kunaweza endelea kwa miaka 25 hapo ndio mtu unaweza kutoa mimea yote na kuanza upya. twende kwenye uzaaji.
kwa wakulima wa kawaida ekari ya ndizi huzaa tani 7 za ndizi ambazo ni sawa na kg 7000. kwenye vituo vya utafiti ilionekana ekari moja inaweza kuzalisha mpaka tani 24 yaani kg 24000. mkungu mmoja wa ndizi kwa wastani unauzito wa kg 12. kwa hiyo ukipata kilo 7000 utakuwa umepata mikungu 583 ya ndizi. kwa dar es salaam mkungu mmoja wa ndizi ni kati ya tsh 12000-18000 ikitegemea na kipindi.basi kwa mikungu 583 utapata tsh millioni 7 hadi milllioni 10!!. je ukiwa na ekari 10, 20 au 30 utakuwa wapi?. mambo ya kuzingatia nikuhakikisha migomba yako inapata maji ya kutosha na unaikinga na magonjwa na panya wala mizizi. pia ni vizuri ukalima eneo kubwa kidogo au mkakubaliana na majirani ili kuepuka kusafirisha mzigo kidogokidogo kitu kinachoweza kukupa hasara. wenye experiance na nyongeza naombeni muongezee.
Malila,
Chasha,
Sabayi,
Kubota etc
update 26/3/2015
wakuu nimepata ekari tatu nimeanza kuzipanda kidogokidogo. mmpaka sasa nimepanda miche 200 niliyopanda mwezi wa february. Ila napanga mpaka mwezi wa saba niwe nimemaliza. Nimefanya utafiti na kwa kauzoefu nilikopata nimejifunza yafuatayo.
Watafiti wa Uganda walifanya utafiti kuhusu spacing ya migomba. Kuna waliyoweka 3mx3m na kupanda migomba 400 kwa ekari. Mikungu iliyozaliwa ilikuwa na kilo 14. 2.5x2.5 walipanda migomba 640 kwa ekari na ilikuwa na mikungu ya kilo 12.5 hadi 13. Kuna mingine ilikuwa 2x2 na walipanda migomba 1000 kwa ekari na mikungu yake ilikuwa kilo 11.
Kutokana na hivyo mi napanda 2.5x2, ambayo itatoa migomba 800 kwa ekari. Huu ulikuwa utafiti wa ndizi Uganda ila mimi napanda mzuzu.
Shimo linakuwa kipenyo cha 60cm na urefu wa 60cm. au urefu wa hadi gotini kwa mtu mzima. Kila shimo wanachimbia sh 300 hadi 500 kulingana na ugumu. Maximum 400,000 kwa ekari.
Kila mche nanunua tsh 300 na kubeba hadi shambani ni tsh 200. Jumla itakuwa 400,000 kwa ekari.
Napandia debe moja la samadikila shimo. Nimeinunua 20,000 na kila debe wanabebea tsh 400. Jumla ni 340,000 kwa ekari. Kupanda ni 100 sawa na 80,000 kwa ekari.
Jumla ya kukamilisha eka itakuwa 1, 220,000. Gharama za palizi na zingine ntakuwa nawaupdate.