Kwa wakuu MziziMkavu na Mupirocin na wengine wowote wale naomba comments zenu kuhusu tiba hizi mbili mbadala za pumu (asthma).
1. VUO
Shangazi yangu(R.I.P.) hapo zamani alikuwa anasifika sana kuwa ni mganga mkuu (wa kienyeji) wa pumu. Magari yalikuwa yanajipanga nyumbani kwake kama kwa babu wa kikombe vile. Sasa, yours truely ndio mtu aliekuwa ananituma kumtafutia hizo dawa. Dawa yenyewe niliyotumwa ni majani ya mmea unaoitwa "kivunja hukumu". Jina hili linatumika sana sehemu za mwambao (Tanga, Pangani, Sadani, Bagamoyo). Anaejua jina lake la kitaalam anisaidie. Hivi ndivyo alivyokuwa anafanya (family secrets in the open):
Anachukua haya majani ya vivunja hukumu na kuyatia kwenye sifuria kubwa yenye maji na kuyachensha. Yakichemka anamuweka mgonjwa kwenye kiti, chini - kati ya miguu - anaweka lile sifuria linalofuka mvuke na kumfunikia huyu mgonjwa gubigubi na mashuka. Anachopaswa kufanya mgonjwa ni kupumua deep ule mvuke kwa muda (sijui dakika ngapi). Hii medicinal steam inaitwa VUO.
Kwa kuwa wagonjwa waliopona waliwa-refer wenzao inaelekea hii dawa pengine ilifanya kazi. Shangazi ali-claim kuwa wagonjwa walipona kabisa pumu na sio kupata nafuu tu - sijui kama ni kweli. Hapa ndipo ninapouliza kama wenzagu mmekwisha jifunza hii tiba.
Huu mmea unaitwa "kivunja hukumu" kwa sababu wenyeji waliamini kuwa kama una kesi mahakamani, ukitia jani la huu mmea mfukoni basi jaji akikuona tu anasema "case dismissed". Hapa hata mimi siamini kwa sababu mara nyingi nilipokuwa shule ya msingi na ikiwa nimechelewa kufika shuleni asubuhi nilitia haya majani mfukoni lakini mkong'oto wa henzirani niliupata tu.
2. ASALI
Kwa kuwa pumu (asthma) huletwa na alergic reaction ya pollens, nk., kuna school of thought inayoamini kuwa hizi alergies (pumu, macho kuwasha, nk.) zinatibika kama muathirika (wa alergy) atatumia ASALI (badala ya sukari). Sharti ni kuwa asali hii iwe imetokana na mizinga ya nyuki ambayo ni local. Dhana hapa ni kuwa kama utakula asali iliyotengenzwa na nectar + pollen ya maua (local), itakuwa ime-encorporate small quantities za hizi pollens (alergens). Hivyo basi hii itamfanya mtu (immune system yake) azoee hizi alergens na baada ya muda hata akipumua hizi alergens hazitamletea symptoms za pumu.
Maoni yenu wakuu.