Ushauri wa kina wakitaalamu wa haraka tafadhari

Ushauri wa kina wakitaalamu wa haraka tafadhari

Gagurito

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
5,600
Reaction score
806
Rafiki yangu anasumbuliwa na Asthma. Kwa muda wa mwaka sasa kifua hakijambana ILA jana kimembana sana, alikuwa anapumua kwa tabu, mapigo ya moyo yanakwenda kwa kasi na miguu na mikono kutetemeka kama vile mtu mwenye degedege, mwili kuchemka na kutoa jasho jingi pia analalamika kichwa kinamuuma. Tulimpeleka hospital kupata matibabu, kwa sasa ni mkono wa kulia tu ndio bado unamtetemeka. Je ni kawaida kwa watu wenye asthma kuwa hivi au kuna tatizo la ziada? Ushauri wenu please!
 
Mpeni Ushauri huyu ndugu yetu, wataalam mpo wapi?
 
Mkuu Gagurito mpe pole zangu huyo Rafiki yako anayeumwa na Maradhi ya Pumu nitajaribu kukupa Tiba Mbadala ya maradhi hayo

ya pumu ni nini afanye hapo baadae. Na kuhusu kutetemeka kwa mikono na mapigo ya moyo kwenda kwa kasi mwambie huyo

Rafiki yako aende haraka Hospitali wakamfanyie uchunguzi kwa kina ili Ma-Daktari wapate kujuwa ni kwanini moyo unakwenda mbio

na kutetemeka kwahiyo miguu na mikono watampatia dawa.

Na kuhusu Dawa ya Maradhi ya Pumu fuata ushauri wa Dawa yangu hapo chini:

Chukuwa karafuu 6 zitowe vichwa vyake kisha uzirowek hizo karafuu katika nusu gilasi ya maji usiku kusha kisha

unakunywa maji yake asubuhi kabla hujala kitu. Fanya hivyo kwa muda wa siku 15. Kisha uje hapa utupe

Feedback je Amepona Maradhi ya Pumu au bado?
 
Dr, hayo maji ya karafuu sita tu, yanakuwa kiasi gani ili yatoshe kunywa siku 15. Na yananywewa kiasi gani, glass ama kijiko?
Kuna uncle wangu anaumwa sana pumu, natumaini atasaidika, inshaallah!
 
Dr, hayo maji ya karafuu sita tu, yanakuwa kiasi gani ili yatoshe kunywa siku 15. Na yananywewa kiasi gani, glass ama kijiko?
Kuna uncle wangu anaumwa sana pumu, natumaini atasaidika, inshaallah!
Mkuu King'asti Kila siku usiku awe anaroweka karafuu sita alizotowa vikonyo vyake yaani atowe vichwa vyake vya juu hizo karafuu kisha aweke kwenye nusu glasi ya maji ya kunywa kisha anaamka Asubuhi anakunywa hayo maji ya karafuu kwa huo muda wa siku 15 mfululizo atapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu inshaa-Allah. Mwambie atumie Dawa yangu huyo mjomba wako kisha uje hapa baada ya siku 15unipe Feedback please.
 
Asthma ni ugonjwa ambao unarithiwa. It is among of the Chronic obstructive pulmonary disease. Matibabu yake kama kabanwa sana anachomwa hydrocortisone na aminophyline hizi dawa husaidia kupunguza kubanwa ndani ya dakika 5, kama ni asthma pekee. Na hii ni emergency anatakiwa kwenda hospital haraka.
Ikitulia atatakiwa kumeza dawa zifuatazo yeye atakuwa anajua.
1. Salbutamol
2. Predinisolone
3. Na antibiotic yeyote
angalau kwa siku tano.
Asthma ni allergy na allergy huwa hazina tiba, tunazo toa mara nyingi ni kwa ajili ya kutuliza tu. Na ndiyo maana huwa inajirudia.
Matibabu ya allergy ni kugundua kile kinachosababisha upate allergy na kuepukana navyo.
Kwa asthma mara nyingi hivi huwa visababishi.
Vumbi, poleni za baadhi ya maua, mafua, marashi ya mafuta au perfume au sabuni. Hivyo hawa hushauriwa kutumia sabuni za vipande hasa mbuni au codry mafuta mfano vestline yasiyo na harufu.
Sasa kwa hili la kutetemeka mkono tu hii tunaita degedege (localized seizure ) kwa ushauri wangu aende hospital iliyo karibu ili waone watamsaidiaje. Ikiwa itaendelea kumsumbua sana basi nafikiri atahitaji kutumia dawa muda mrefu za kifafa. Lakini kwa sasa apime na malaria pia tuone.
Nakutakia usiku mwema, mpe pole rafiki yako. Dr Mupirocin
 
Kwa wakuu MziziMkavu na Mupirocin na wengine wowote wale naomba comments zenu kuhusu tiba hizi mbili mbadala za pumu (asthma).

1. VUO
Shangazi yangu(R.I.P.) hapo zamani alikuwa anasifika sana kuwa ni mganga mkuu (wa kienyeji) wa pumu. Magari yalikuwa yanajipanga nyumbani kwake kama kwa babu wa kikombe vile. Sasa, yours truely ndio mtu aliekuwa ananituma kumtafutia hizo dawa. Dawa yenyewe niliyotumwa ni majani ya mmea unaoitwa "kivunja hukumu". Jina hili linatumika sana sehemu za mwambao (Tanga, Pangani, Sadani, Bagamoyo). Anaejua jina lake la kitaalam anisaidie. Hivi ndivyo alivyokuwa anafanya (family secrets in the open):

Anachukua haya majani ya vivunja hukumu na kuyatia kwenye sifuria kubwa yenye maji na kuyachensha. Yakichemka anamuweka mgonjwa kwenye kiti, chini - kati ya miguu - anaweka lile sifuria linalofuka mvuke na kumfunikia huyu mgonjwa gubigubi na mashuka. Anachopaswa kufanya mgonjwa ni kupumua deep ule mvuke kwa muda (sijui dakika ngapi). Hii medicinal steam inaitwa VUO.

Kwa kuwa wagonjwa waliopona waliwa-refer wenzao inaelekea hii dawa pengine ilifanya kazi. Shangazi ali-claim kuwa wagonjwa walipona kabisa pumu na sio kupata nafuu tu - sijui kama ni kweli. Hapa ndipo ninapouliza kama wenzagu mmekwisha jifunza hii tiba.

Huu mmea unaitwa "kivunja hukumu" kwa sababu wenyeji waliamini kuwa kama una kesi mahakamani, ukitia jani la huu mmea mfukoni basi jaji akikuona tu anasema "case dismissed". Hapa hata mimi siamini kwa sababu mara nyingi nilipokuwa shule ya msingi na ikiwa nimechelewa kufika shuleni asubuhi nilitia haya majani mfukoni lakini mkong'oto wa henzirani niliupata tu.

2. ASALI
Kwa kuwa pumu (asthma) huletwa na alergic reaction ya pollens, nk., kuna school of thought inayoamini kuwa hizi alergies (pumu, macho kuwasha, nk.) zinatibika kama muathirika (wa alergy) atatumia ASALI (badala ya sukari). Sharti ni kuwa asali hii iwe imetokana na mizinga ya nyuki ambayo ni local. Dhana hapa ni kuwa kama utakula asali iliyotengenzwa na nectar + pollen ya maua (local), itakuwa ime-encorporate small quantities za hizi pollens (alergens). Hivyo basi hii itamfanya mtu (immune system yake) azoee hizi alergens na baada ya muda hata akipumua hizi alergens hazitamletea symptoms za pumu.

Maoni yenu wakuu.
 
Mkuu Kifyatu huo Mti wa mvunja Hukumu au kwa jina lingine Mvunja kesi kama sikosee una mauwa meupe unaweza kusaidia ingawa sijawahi kujaribu kwa Dawa za pumu mimi huwa najari kwa mambo ya kesi unasaidia sana huo mti kuvunja kesi. Nitajaribu Dawa bibi yako hongera mkuu Kifyatu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom