Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Huwa najiuliza kama watu ambao ni wazima kabisa wa afya tena vijana; kuna muda maisha yanawapiga hadi wanashinda na njaa, hivi tunawafikiriaje ndugu zetu walemavu ambao hawana mikono, miguu, hawaoni n.k?
Katika misingi ya distribitive justice serikali kote duniani hukusanya kodi na kuzitawanya kulingana na mahitaji ya kijamii.
Badala ya hali ilivyo sasa ambapo walemavu wanaombaomba mtaani na hawapati msaada wa maana: Nashauri serikali ianzishe makambi ya kuhudumia walemavu kwa kila kitu maisha yao yote maana hawakupenda kuwa walivyo.
Ili kupata fedha ya kuwahudumia, serikali iweke kodi angalau ya Tsh.1 kwa kila huduma na naamini hakuna mtanzania mwenye ubinadamu anaweza kupinga sera hiyo.
Kwa maoni yangu maendeleo ni pamoja na utu na kuoneana huruma sisi kwa sisi hasa kwa watu wenye mahitaji maalum.
Naomba tuiuunge mkono hoja hii na tuishawishi serikali hadi ikubaliane nayo, tutakuwa tumefanya jambo la maana duniani na mbele ya Mungu tutakuwa mashahidi.