Ushauri wa kisheria kutokana na kuonewa na Afisa Elimu Idara ya Sekondari (W)

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
14,624
Reaction score
20,666
Wana JF naomba Ushauri na msaada wenu katika hili.
Nilikuwa masomoni katika chuo kimojawapo hapa Tanzania, kwa masomo ya shahada ya elimu (Sayansi) kwa mchepuo wa Fizikiana na Chemia, Bachelor of Education in Science- (Physics, Chemistry). Tangu Nov 2010 hadi June 2013 Nilipomaliza masomo.

Niliporudi toka masomoni nikakuta:-
-Barua ya shitaka la utoro kazini ya tarehe 15/06/2011
-Baraua ya Kusimamishwa kazi kwa nusu mshahara ya tarehe 15/06/2011
Nikaandika barua yangu ya utetezi, Tarehe 4/07/2013. Kamati ya nidhamu na maadili TSD ikaka kikao kifupi wakanihoji na kutoa maamuzi ya shauri langu la nidhamu barua ya tarehe 04/07/2013, Ambayo nilikabidhiwa nimpelekee mkuu wangu wa shule na niwe chini ya uangalizi wake. Kama inavyojieleza hapa chini.
jf attachment.PNG
Kilichofuata baada ya TSD wilaya kutoa Maamuzi
· Afisa Elimu Sekondari alipinga maamuzi ya kamati ya TSD kwa kuhoji kwanini swala langu limeshughulikiwa mapema.
· Nikiwa bado sijaondoka kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya, Afisa Elimu Sekondari (W), Alimpigia simu mkuu wa shule na kumpa agizo asipokee wala kupitisha barua yangu yoyote.
· (Katibu TSD ndiye aliyenijulisha kwamba simu imeshapigwa kwa mkuu wa shule hivyo akaomba nimrudishie ile barua sababu haitopokelewa). Haya matukio ni ya tarehe 04/07/2013

Tarehe 08/07/2013, Nilirudi halmashauri ya Wilaya ili kufuatilia barua iliyozuiwa.
Katibu TSD (W) na Afisa utumishi (W) wakaenda kwa afisa Elimu Sekondari na kujadiliana kwa muda, waliporudi wakanikabidhi barua na tarehe 10/07/2013 barua ikasainiwa na kupitishwa na mkuu wa shule.

Je ni sawa kwa Mwalimu alieenda kusoma na kurudi kituoni kwake kupewa adhabu hii.
· Kuanza na mshahara wa Daraja TGTS C kana kwamba ni mwajiriwa mpya wa Diploma mwajiriwa mpya. (Nilipaswa kuwa daraja D, Ni miaka mitano imepita tangu niajiriwe na Serikali,Nimeajiriwa March 2008),
· Kutokudai Mishahara/ Nusu mshahara yote ya nyuma kipindi chote nilipokuwa masomoni.
· Afisa Elimu Sekondari(W) kuzuia nisipewe vipindi labda mpaka nitakapoingizwa kwenye Payrol,ndio atanitambua kama mtumishi. Kumbuka shule zimefunguliwa tangu tarehe 15/07/2013

Na ikumbukwe kuwa shule haina mwalimu wa Sayansi hata mmoja kati ya walimu wapatao 17, ukiacha mkuu wa shule ambaye mara mojamoaja hufundisha chemia.

Je kipi kifanyike ili haki itendeke?, Maana Mwezi sasa nipo nyumbani na familia yangu bila kujua hatma ya maisha yetu hapa ugenini.

Je nani anahusika kumuajibisha huyu Afisa Elimu Sekondari (W)?
. Huyu Afisa Elimu kwa sasa ndiye anayekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji (w)

Kabla ya Kwenda masomoni: October 2010

· Niliomba ruhusa kwa maandishi nikiwa nimeamabatanisha Joining Instruction form toka chuo husika haikujibiwa.

· Nikamfuata ofisini Afisa Elimu Sekondari (W) kumuomba aweze kuniruhusu kwenda masomoni alikataa na kusisitiza “iwapo utaondoka kwenda masomoni bila ruhusa yangu na kutokuwepo kituoni kwa siku 5 mfululizo basi nitazuia mshahara wako”.

· Pia siku hiyo hiyo nilijadiliana naye kuhusu likizo bila malipo ili niende kusoma, bado alikataa kwa kunieleza yeye hausiki labda kama ningekua naenda kusoma masomo nje ya taaluma ya ualimu. (Sababu niliajiriwa kama mwalimu Baada ya kumaliza masomo ya astashahada ya elimu, Diploma Course in Education).

Nililazimika kwenda kuendelea na masomo mpaka nilipomaliza ndipo nikarudi kufuatilia mstakabali wa ajira yangu katiaka Halmashauri ya Wilaya husika. Kipindi chote nilichokuwa masomoni sikuwahi pokea mshahara wowote. Mpaka muda huu sina mshahara. Na haifahamiki nilini wataingiza taarifa zangu kwenye Payroll.

Utata katika hili la mishahara.
· Termination date ya mshahara inaonekana kwenye system ilifanyika tarehe 02/03/2012
· Slip salary ya mpaka Mwezi January 2012 Inaonyesha kuwa nimekuwa nikipokea mshahara kamili.
· Maelezo Hati ya shitaka ya 15/06/2011 inaonyesha nilipaswa kupokea Nusu mshahara mpaka shitaka langu litakapo kwisha.
· Mshahara ulisitishwa (kutokuingiza kwenye account yangu) tangu Mwezi November 2010.

Swali: Je hii fedha (mshahara) ambayo/ambao inaonekana kana kwamba nilikuwa nikipokea zilikuwa zinasainiwa na kuchukuliwa na nani?

Nawasilisha naomba mchango wenu wa mawazo wadau.

cc: Zitto , MALICK MUSSA , CHAMVIGA , Jimmy Kadebedebe , MKWELItu , Rajasili , onduru ogy , Evelyn Salt , Massawe G. I , Madame B , Mohamedi Mtoi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mwl.RTC.
Kwanza nikupe pole kwa mtihani huo uliokupata. Inasikitisha kiukweli kukosa mshahara wako halali kwa miaka yote hiyo. Hii ni dhulma ambayo watu wengi tunatendewa na waajiri au wasimamizi wetu hapa nchini.
Ishu yako iko too complicated kiukweli na mimi napatwa ugumu nianze kushauri kushughulikia lipi na kumalizia na lipi.

Labda niseme tu kuwa kuna tatizo ambalo hapa litakuandama, nalo ni kuondoka kazini kwako bila ruhusa ya Afisa elimu wako. Hii inawezekana wakaitumia kama fimbo ya kukuchapia ktk sakata lako hili.
Labda ushauri wangu ungeomba ajira mpya kwa maana ulipomaliza chuo kwa shahada yako hiyo upangiwe ajira mpya na kituo kipya cha kazi kipya. Baada ya hapo ndio uanze kupambana na Afisa elimu wako ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mshahara wako uliokosekana kwa kipindi chote hicho unalipwa. Unaweza lipeleka ngazi ya juu zaidi kama ataonekana kuwa mbabe ila ukweli busara inaitaji. Yeye anayosababu ya kukuadhibu kwa kuondoka kazini bila kupewa idhini.
Haya ni matukio ya kawaida na wengi yanawatokea sana.
By the way, wewe kwa sasa si mwalimu wa secondari tena kwa facult yako uliyosoma unapaswa kufundisha vyuo vya ualimu. Huko uliko upo kwa bahati mbaya. Mimi ni mfano wako nimesoma facult kama hiyo na specialization yangu ni Mathematics. Wewe ni marketable kuliko wanavyo kudiscredit. Fanya maamuzi ima upangiwe ajira mpya upiganie mshahara wako wa nyuma ukiwa unafanya kazi au.
Kama umeridhika kubaki hapo ulipo tumia busara na uombe busara za Afisa elimu(M) na wadau wengine.
Ngoja wengine watakuja.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwl.RCT kwanza pole sana kwa mkasa uliokukuta wa kunyimwa haki zako za msingi ambazo wewe ukiwa kama mwajiriwa ulipaswa uzipate.
Pia vile vile kwa kutopata hata kile kidogo ambacho ulipaswa upate
Ila mkuu Naomba unipe muda leo nikakague makabrasha yangu ya ofisi kisha nitakuja na jibu sahihi via PM.
Ila napenda kukueleza tu kwa ufupi kuwa hizo fedha za mshahara wako zinaliwa na ofisi ya Afisa Elimu Sekondari (W)
................nitaendelea kuwasiliana na wewe.......
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.

Kwanza pole sana kwa maswahibu unayo kutana nayo, na hongera kwa maamuzi magumu uliyo chukua awali ya kuamua kwenda chuo/kusoma bila kuwa na ridhaa ya muajiri wako. Hongera kwa kukamata shahada yako pia maana bila shaka ilikuwa ndio ndoto yako na ndoto ya mtu yoyote anaye penda mafanikio!

Naomba niijikite kwenye masuala kadhaa kuhusu hii kadhia inayo kukabili.

1. Lazima ujue kuwa pamoja na shauku yako ya kwenda kusoma ulipaswa kuhakikisha kuwa una pata release kutoka kwa muajiri wako, ungekuwa na release haya yasinge tokea. Wanakukaba sasa hivi kwa kuwa huna release (hiyo ndio silaha yao kwako).

2. Ulipaswa kuwa unarejea kituoni kwako kila wakati wa likizo na hata block teaching practise zako ulipaswa kuzifanyia kituoni pako, hii ingekufanya kujenga zaidi ukaribu na mkuu wako lakini pia ingekurahisishia kufuatilia release yako. Kumbuka hukuwa na ruhusa, hii ingevunja nguvu ya kutaka kukushughulikia maana mahudhurio kituoni yangesimama na wewe kipindi hiki.

3. Tambua kuwa, kwa kuwa hukuwa na ruhusa ulipaswa kukatiwa mshahara, lakini walipaswa kukuita na kukuhoji kuhusiana na hilo na muafaka ufikiwe, ulipaswa pia kufuatilia kwa ukaribu sana kuhusiana na hilo ili kuepusha haya yanayotokea. Bila shaka uli relax sana labda kwa kuwa ulikuwa na boom.

4. Lazima ujue kuwa kuna baadhi ya watu wenye vyeo wana roho mbaya na zenye kutu kuliko unavyo weza kufikiri! Kwa nini, kwa kuwa ulitimiza vigezo vya kwenda kusoma (miaka 2 kazini), busara ilikuwa wewe kupewa onyo na shule yako inufaiike na elimu uliyoipata bila kuwaathiri wanafunzi na kuiathiri familia yako pamoja na wewe mwenyewe.

Chakufanya!

1. Dhambi kubwa kuliko zote ni woga, vaa ujasiri upambane ili kama ni kupoteza upote kwa jasho. Usikate tamaa na pambana na waone kuwa una dhati ya kupambana nao kuisaka haki yako. Uliandika barua ya kuomba ruhusa na hawakukupa ruhusa, umeondoka umerudi na jiwe ili ufundishe hawataki, shule ina uhaba!

2. Jua uhalali wa kuzia fedha zako (mishahara) kama umefuata taratibu, huenda kuna watu wamefaidika nayo, lazima ujue maana ilikuwa inakuja kwako kama haki yako.

3. Nenda kwa mkurugenzi wako muelezee inshu nzima table hii inshu nzima kwake.

Nitarejea baada ya kusoma mchango wa wadau wengine.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Mkuu mwl.RTC.
Kwanza nikupe pole kwa mtihani huo uliokupata. Inasikitisha kiukweli kukosa mshahara wako halali kwa miaka yote hiyo. Hii ni dhulma ambayo watu wengi tunatendewa na waajiri au wasimamizi wetu hapa nchini.
Ishu yako iko too complicated kiukweli na mimi napatwa ugumu nianze kushauri kushughulikia lipi na kumalizia na lipi.

Labda niseme tu kuwa kuna tatizo ambalo hapa litakuandama, nalo ni kuondoka kazini kwako bila ruhusa ya Afisa elimu wako. Hii inawezekana wakaitumia kama fimbo ya kukuchapia ktk sakata lako hili.
Labda ushauri wangu ungeomba ajira mpya kwa maana ulipomaliza chuo kwa shahada yako hiyo upangiwe ajira mpya na kituo kipya cha kazi kipya. Baada ya hapo ndio uanze kupambana na Afisa elimu wako ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mshahara wako uliokosekana kwa kipindi chote hicho unalipwa. Unaweza lipeleka ngazi ya juu zaidi kama ataonekana kuwa mbabe ila ukweli busara inaitaji. Yeye anayosababu ya kukuadhibu kwa kuondoka kazini bila kupewa idhini.
Haya ni matukio ya kawaida na wengi yanawatokea sana.
By the way, wewe kwa sasa si mwalimu wa secondari tena kwa facult yako uliyosoma unapaswa kufundisha vyuo vya ualimu. Huko uliko upo kwa bahati mbaya. Mimi ni mfano wako nimesoma facult kama hiyo na specialization yangu ni Mathematics. Wewe ni marketable kuliko wanavyo kudiscredit. Fanya maamuzi ima upangiwe ajira mpya upiganie mshahara wako wa nyuma ukiwa unafanya kazi au.
Kama umeridhika kubaki hapo ulipo tumia busara na uombe busara za Afisa elimu(M) na wadau wengine.
Ngoja wengine watakuja.

  • Ndio anachokifanya afisa elimu kwa sasa, Maana anadiliki kuingilia na kuhoji maamuzi ya TSD (W), Pamoja na kukwamisha utendaji kazi wa afisa utumishi wilaya,
  • Swala la ajira mpya nimerifikiria na nitalifanyia kazi iwapo alternative zote za kupata haki yangu zitakwama.
  • KUpeleka ngazi za juu ndio hatua itakayofuata.
Nashukuru nitaufanyia kazi huu ushauri wako
 
Waone CWT hapo wilayani pako.

CWT (w) na CWT (Mkoa) wanataarifa, Wameshauri tusubili Mkurugenzi Mtendaji (W) atakaporudi, Sababu kwa sasa Huyu Afisa elimu sekondari ndiye anayekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji (w).
 
Mkuu.

Kwanza pole sana kwa maswahibu unayo kutana nayo, na hongera kwa maamuzi magumu uliyo chukua awali ya kuamua kwenda chuo/kusoma bila kuwa na ridhaa ya muajiri wako. Hongera kwa kukamata shahada yako pia maana bila shaka ilikuwa ndio ndoto yako na ndoto ya mtu yoyote anaye penda mafanikio!

Naomba niijikite kwenye masuala kadhaa kuhusu hii kadhia inayo kukabili.

1. Lazima ujue kuwa pamoja na shauku yako ya kwenda kusoma ulipaswa kuhakikisha kuwa una pata release kutoka kwa muajiri wako, ungekuwa na release haya yasinge tokea. Wanakukaba sasa hivi kwa kuwa huna release (hiyo ndio silaha yao kwako).

2. Ulipaswa kuwa unarejea kituoni kwako kila wakati wa likizo na hata block teaching practise zako ulipaswa kuzifanyia kituoni pako, hii ingekufanya kujenga zaidi ukaribu na mkuu wako lakini pia ingekurahisishia kufuatilia release yako. Kumbuka hukuwa na ruhusa, hii ingevunja nguvu ya kutaka kukushughulikia maana mahudhurio kituoni yangesimama na wewe kipindi hiki.

3. Tambua kuwa, kwa kuwa hukuwa na ruhusa ulipaswa kukatiwa mshahara, lakini walipaswa kukuita na kukuhoji kuhusiana na hilo na muafaka ufikiwe, ulipaswa pia kufuatilia kwa ukaribu sana kuhusiana na hilo ili kuepusha haya yanayotokea. Bila shaka uli relax sana labda kwa kuwa ulikuwa na boom.

4. Lazima ujue kuwa kuna baadhi ya watu wenye vyeo wana roho mbaya na zenye kutu kuliko unavyo weza kufikiri! Kwa nini, kwa kuwa ulitimiza vigezo vya kwenda kusoma (miaka 2 kazini), busara ilikuwa wewe kupewa onyo na shule yako inufaiike na elimu uliyoipata bila kuwaathiri wanafunzi na kuiathiri familia yako pamoja na wewe mwenyewe.

Chakufanya!

1. Dhambi kubwa kuliko zote ni woga, vaa ujasiri upambane ili kama ni kupoteza upote kwa jasho. Usikate tamaa na pambana na waone kuwa una dhati ya kupambana nao kuisaka haki yako. Uliandika barua ya kuomba ruhusa na hawakukupa ruhusa, umeondoka umerudi na jiwe ili ufundishe hawataki, shule ina uhaba!

2. Jua uhalali wa kuzia fedha zako (mishahara) kama umefuata taratibu, huenda kuna watu wamefaidika nayo, lazima ujue maana ilikuwa inakuja kwako kama haki yako.

3. Nenda kwa mkurugenzi wako muelezee inshu nzima table hii inshu nzima kwake.

Nitarejea baada ya kusoma mchango wa wadau wengine.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

Nimekusoma vyema kabisa mkuu, upo sahihi kabisa, Sitokata tamaa na nitapambana hadi hatma ya hili swala langu kueleweka, Mkurugenzi atakapo rudi ndiye atakuwa mtu wa kwanza kwenda kumuona, sababu kwa sasa nafasi ya Mkurugenzi anakaimu huyu Afisa Elimu. Nashukusa sana kwa mchango wako wa mawazo.
 
Nimepatwa na hasira ghafla baada ya kumkumbuka Afisa Elimu mshen.zi mmoja wilaya ya Sumbawanga mjini alivyokuwa anagoma kupitisha barua ya uhamisho ya mke wangu bila sababu za msingi, alipitisha baada ya kutaka kumchapa mangumi ofsini kwake mbele ya ps wake. Wanakera sana hawa watu, sijui wanadhani ukisoma utaenda kuwapora nafasi zao!?. Ntarudi hasira ikitulia. Usikate tamaa
 
Tuko pamoja Baba V , Nakusubiri, Mchango wako ni muhimu sana ili kupunguza na ikiwezekana kuondoa kabisa huu urasimu ulipo kwa sasa kwa hawa watendaji muhimu.
 
Last edited by a moderator:
  • Ndio anachokifanya afisa elimu kwa sasa, Maana anadiliki kuingilia na kuhoji maamuzi ya TSD (W), Pamoja na kukwamisha utendaji kazi wa afisa utumishi wilaya,
  • Swala la ajira mpya nimerifikiria na nitalifanyia kazi iwapo alternative zote za kupata haki yangu zitakwama.
  • KUpeleka ngazi za juu ndio hatua itakayofuata.
Nashukuru nitaufanyia kazi huu ushauri wako

pole sana kwa mahangaiko na usumbufu mkubwa. Suala la ajira mpya ni ligumu sana kwa sasa maana kuna hii kitu database inaonesha kwamba ulishaajiriwa tena hivyo hutoweza kufanikiwa katika hili. Ajira mpya utaomba utapata ila ikifika hatua ya kuripoti kazini kitendo cha kuingizwa kwenye payrol utaanza tena mtihani mwingine wa kwamba huwezi kuajiriwa tena coz tayari ulishakuwa na check no. Labda kama utabadilisha majina tofauti na yale uliyoajiriwa nayo diploma,ufanye hapo hata tofauti ya jina moja. Nakuambia haya maana yamenikuta mwaka huu nikahangaika sana. Mwisho wa siku nikaja saidiwa na afsa utumishi,,anakurudishia mshahara wako kama kawaida anakupa uhamisho wa juu kwa juu kwenda halmashauri nyingine ila uangalie namna ya kumlinda ili kupitisha barua yako ya uhamisho.
In short huyo afsa elimu wako ana roho mbaya sana maana anakufuatilia too much,,yeye ni mamilioni mangapi ya hela amekula hapo then anakuonea wewe mdogo ambaye haujafaidi chochote ? Jipe moyo yatapita na soon yatakuwa historia,na pia umuombe Mungu awaondolee moyo mgumu hao unaokutana nao ktk kusolve hili jambo
 
  • Ndio anachokifanya afisa elimu kwa sasa, Maana anadiliki kuingilia na kuhoji maamuzi ya TSD (W), Pamoja na kukwamisha utendaji kazi wa afisa utumishi wilaya,
  • Swala la ajira mpya nimerifikiria na nitalifanyia kazi iwapo alternative zote za kupata haki yangu zitakwama.
  • KUpeleka ngazi za juu ndio hatua itakayofuata.
Nashukuru nitaufanyia kazi huu ushauri wako

Mwl.RCT.
Kuna mdau pia ameshauri kwamba kwakuwa Afisa elimu wako amesema hata vipindi usipangiwe, hapa kuna kila dalili kuwa huyu jamaa anatengeneza mazingira ya wewe kukukatisha tamaa hatimae uache kazi au kuomba ajira mpya jambo litakalo pelekea mshahara wako wa nyuma kupotea. Kuna kila dalili kwamba huyu Afisa amekuwa akifaidika na mshahara wako kwa kipindi hicho ulichositishiwa mshahara. Kwahiyo fuatilia kwasasa Pay slips(PS) zako za muda wote uliopita kwakuwa hata ukiwa umesitisha mshahara pay slip zinaendelea kuja. Ukipata pay slip utakuwa upo sehemu nzuri ya kudai haki yako. Pay slip kuna uwezekano huyo Afisa Elimu amezifukia kwa hiyo kama haujaomba zitafute utampa presha. Inapasa uwe jasiri ktk sakata lako kama alivyoshauri Mohamedi Mtoi ila usitishie ngumi kama Baba V alivyotaka mfanyia afisa elimu wao huko; si wote wanaweza pigikika wengine wanaweza kukupiga wewe. Baada ya hapo sasa andika barua kwa muajiri wako Mkurugenzi(W) kuhusu kuachiliwa mshahara wako uliozuiwa na uambatanishe barua yako ya kuomba ruhusa kwenda kusoma. Nashauri sana busara itumike kuliko mababu yanaweza kukuletea usumbufu ktk kudai haki yako. Nikupe moyo tu kwamba utafanikiwa wala usipaniki na pesa yako itapatikana. Tena unaweza kuwa chanzo cha Afisa elimu wako kuachishwa kazi kama ikibainika kuna hujuma amezifanya katika mshahara wako. Pigania kupewa vipindi na kuwepo kazini kwako. Itakusaidia pia ktk kupangiwa mshahara wako.
 
Pay slip nilizofanikiwa kuzipata ni tatu (3), Ya mwezi wa 6 na 9 kwa mwaka 2011, Na ya January 2012. Zingine hazikuweza kupatikana.
4jf_1.PNG

4jf_2.PNG
 
Wana JF naomba Ushauri na msaada wenu katika hili.
Nilikuwa masomoni katika chuo kimojawapo hapa Tanzania, kwa masomo ya shahada ya elimu (Sayansi) kwa mchepuo wa Fizikiana na Chemia, Bachelor of Education in Science- (Physics, Chemistry). Tangu Nov 2010 hadi June 2013 Nilipomaliza masomo.

Niliporudi toka masomoni nikakuta:-
-Barua ya shitaka la utoro kazini ya tarehe 15/06/2011
-Baraua ya Kusimamishwa kazi kwa nusu mshahara ya tarehe 15/06/2011
Nikaandika barua yangu ya utetezi, Tarehe 4/07/2013. Kamati ya nidhamu na maadili TSD ikaka kikao kifupi wakanihoji na kutoa maamuzi ya shauri langu la nidhamu barua ya tarehe 04/07/2013, Ambayo nilikabidhiwa nimpelekee mkuu wangu wa shule na niwe chini ya uangalizi wake. Kama inavyojieleza hapa chini.Kilichofuata baada ya TSD wilaya kutoa Maamuzi
· Afisa Elimu Sekondari alipinga maamuzi ya kamati ya TSD kwa kuhoji kwanini swala langu limeshughulikiwa mapema.
· Nikiwa bado sijaondoka kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya, Afisa Elimu Sekondari (W), Alimpigia simu mkuu wa shule na kumpa agizo asipokee wala kupitisha barua yangu yoyote.
· (Katibu TSD ndiye aliyenijulisha kwamba simu imeshapigwa kwa mkuu wa shule hivyo akaomba nimrudishie ile barua sababu haitopokelewa). Haya matukio ni ya tarehe 04/07/2013

Tarehe 08/07/2013, Nilirudi halmashauri ya Wilaya ili kufuatilia barua iliyozuiwa.
Katibu TSD (W) na Afisa utumishi (W) wakaenda kwa afisa Elimu Sekondari na kujadiliana kwa muda, waliporudi wakanikabidhi barua na tarehe 10/07/2013 barua ikasainiwa na kupitishwa na mkuu wa shule.

Je ni sawa kwa Mwalimu alieenda kusoma na kurudi kituoni kwake kupewa adhabu hii.
· Kuanza na mshahara wa Daraja TGTS C kana kwamba ni mwajiriwa mpya wa Diploma mwajiriwa mpya. (Nilipaswa kuwa daraja D, Ni miaka mitano imepita tangu niajiriwe na Serikali,Nimeajiriwa March 2008),
· Kutokudai Mishahara/ Nusu mshahara yote ya nyuma kipindi chote nilipokuwa masomoni.
· Afisa Elimu Sekondari(W) kuzuia nisipewe vipindi labda mpaka nitakapoingizwa kwenye Payrol,ndio atanitambua kama mtumishi. Kumbuka shule zimefunguliwa tangu tarehe 15/07/2013

Na ikumbukwe kuwa shule haina mwalimu wa Sayansi hata mmoja kati ya walimu wapatao 17, ukiacha mkuu wa shule ambaye mara mojamoaja hufundisha chemia.

Je kipi kifanyike ili haki itendeke?, Maana Mwezi sasa nipo nyumbani na familia yangu bila kujua hatma ya maisha yetu hapa ugenini.

Je nani anahusika kumuajibisha huyu Afisa Elimu Sekondari (W)?
. Huyu Afisa Elimu kwa sasa ndiye anayekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji (w)

Kabla ya Kwenda masomoni: October 2010

· Niliomba ruhusa kwa maandishi nikiwa nimeamabatanisha Joining Instruction form toka chuo husika haikujibiwa.

· Nikamfuata ofisini Afisa Elimu Sekondari (W) kumuomba aweze kuniruhusu kwenda masomoni alikataa na kusisitiza "iwapo utaondoka kwenda masomoni bila ruhusa yangu na kutokuwepo kituoni kwa siku 5 mfululizo basi nitazuia mshahara wako".

· Pia siku hiyo hiyo nilijadiliana naye kuhusu likizo bila malipo ili niende kusoma, bado alikataa kwa kunieleza yeye hausiki labda kama ningekua naenda kusoma masomo nje ya taaluma ya ualimu. (Sababu niliajiriwa kama mwalimu Baada ya kumaliza masomo ya astashahada ya elimu, Diploma Course in Education).

Nililazimika kwenda kuendelea na masomo mpaka nilipomaliza ndipo nikarudi kufuatilia mstakabali wa ajira yangu katiaka Halmashauri ya Wilaya husika. Kipindi chote nilichokuwa masomoni sikuwahi pokea mshahara wowote. Mpaka muda huu sina mshahara. Na haifahamiki nilini wataingiza taarifa zangu kwenye Payroll.

Utata katika hili la mishahara.
· Termination date ya mshahara inaonekana kwenye system ilifanyika tarehe 02/03/2012
· Slip salary ya mpaka Mwezi January 2012 Inaonyesha kuwa nimekuwa nikipokea mshahara kamili.
· Maelezo Hati ya shitaka ya 15/06/2011 inaonyesha nilipaswa kupokea Nusu mshahara mpaka shitaka langu litakapo kwisha.
· Mshahara ulisitishwa (kutokuingiza kwenye account yangu) tangu Mwezi November 2010.

Swali: Je hii fedha (mshahara) ambayo/ambao inaonekana kana kwamba nilikuwa nikipokea zilikuwa zinasainiwa na kuchukuliwa na nani?

Nawasilisha naomba mchango wenu wa mawazo wadau.

cc: Zitto , MALICK MUSSA , CHAMVIGA , Jimmy Kadebedebe , MKWELItu , Rajasili , onduru ogy , Evelyn Salt , Massawe G. I , Madame B , Mohamedi Mtoi

sawa
Nimesoma kwa makini hoja yako na michango makini ya wadau ambayo si mpya sana ndani ya nchi yetu kama mdau mmoja alivyosema kwamba baadhi ya viongozi wetu wana roho mbaya sana .. nyeusi tii..

nimeangalia Slip yako pia unabanywa na Deni la NMB hapo pana kaaaz kweli kweli...

lakini jambo lako ni jepesi sana sana.. cha msingi wewe fanya haya...

1. zile barua ulizoandika kuhusu ruhusa ya kwenda masomoni lazima uwe nazo na udai ulishazisubmit..

2. Usiseme kwamba afisa elimu alikukatalia, just sema nilisubmit taarifa pamoja na joining instruction nikaenda kupiga kitabu.

3. andika barua nyingine ya taarifa ya kurejea toka shule pamoja na cerificate plus RS, ukipigilia msumari wa rejea ya barua zako za kuomba ruhusa ya kwenda masomoni na sasa umerejea tayari kuendeleza gurudumu, kisha mwaga Copy zako kwa huyo afisa ambaye pia ndiye afisa rasilimaliwatu, pamoja na mkuu wa shule. kisha wasili shule uendeleze kitabu kama kawa. sasa kama mkuu wa shule hatakupangia kipindi ndipo mnyuke barua kumuuliza why na uwe makini kuhifadhi all paper work zote maksudi kwa baaadae. atapokujibu ndipo wapandie juu kwa barua baaada ya nyingine.

4. obvious baadae watagoma ndipo mlengeshe jamaa mbele ya sheria ukiwa na ma-salary slip yakoya karibuni. ukimpeleka mahakamani yeye kama yeye (maaana sheria ya sasa mtumishi anaweza kufikishwa mbele ya sheria yeye kama yeye wala si kwa nafasi yake. kwamba flan amekataa nisifundishe.. that is all.

5. hapo lazima utapata haki yako na kulipwa mdurufu yako yote.

kwanini nimekuchorea mchoro huu.

kimsingi Mwajiri wa ajira zote ambazo si za serikali kuu ziko chini ya halmashauri.. Mkurugenzi na kurugenzi zake kama watendaji na Baraza la Madiwani kama policy makers. Watendaji hawa wa halmashauri hubaini mapungufu ya watumishi kama ni walimu, wauguzi, maafisa kilimo, misitu, mifugo n.k. kisha hupeleka taarifa yao kwa kwenye kikao cha madiwani ambao hupitia na kubariki mapendekezo hayo. kisha huingizwa kwenye Bajeti ya halmashauri kwamba kwa mwaka huu wa fedha halmashauri flan inaomba ipitishiwe watumishi kadhaa wa kada kadhaa kutokana na uhaba huo ndani ya halmashauri. Bunge lnapokaa na kupitisha bajeti hizo za tamisemi kazi inabaki kwenye ku-side fund kwa maombi husika, sasa serikali ikiside-fund kiasi fulani mara nyingi si chote chaweza kuwa robo kwenye halmashauri, na waksema fungu hili ni kwa ajili ya malipo ya mishahara let say some million..

Watendaji hawa wa halimashauri, Wauguzi wakuu, waganga wakuu, maaafisa elimu nk, hukaa kudigest priorities za ajira according to fungu lililotolewa na serikali, basi yule aliyeomba walimu sita atapewa wawili, yule aliyeomba manesi kumi anaweza kupata mmoja hivyo hivyo kwa kada zote. hatimaye huyapeleka mapendekezo hayo kwa madiwani ambao huvuja jasho kwelikweli manake kila mtu anataka kata yake ipate hao watendaji. hatimaye ikipita basi andiko huandikwa na kuwasilishwa serikalini kwamba kwa mshiko(fungu) kiduchu mlilotupa tumepanga kwaajiri watumishi kadhaa wa kadha kwenye mwaka huu wa shekeli. bandiko lao likipewa baraka basi ndipo ajira hutangazwa na wananchi tunazichangamkia. sasa watumishi wakishaajiriwa ndipo baraza la madiwani hupewa taarifa. sasa kwa kuwa inajulikana kwamba baadhi ya watumishi huomba uhamisho, hukimbilia kusoma, au kutoroka kituo huwaonya sana waganga wakuu au maafisa elimu kuhakikisha hapana kumwachia mtumishi atoke nje ya kituo in any way. lakini sheria mama zinamtaka mtumishi akishathibitishwa kazini (a year) ana haki ya kuhama, kubadilisha kituo au kusoma.

sasa kosa lao liko hapa, ikiwa mtumishi atakosa kwenye kituo chake cha kazi siku tatu au tano bila taaarifa kwa mwajiri basi atakuwa amepoteza haki zake zote kama mwajiri. atafukuzwa kazi na immediate nafasi yake itatangazwa kuwa wazi kwa ajili ya ajira ya mtu mwingine, sasa wao hawakukufuta kazi, mshahara wako unaflow tu, kesi yako ndio maana nikasema ni rahisi washindilie mahakamani buti kwanza fanya paper work vizuri.
 
Ningekuwa mimi hiyo mijitu wala nisingehangaika nayo. Mshahara wenyewe sawa na kodi ya watumishi wengine? Kisa hasa cha kutesana hivyo ni kipi haswa na shule unayo?
 
Nimekuelewa Chromium , Hiyo ndio hali halisi ya Mwalimu katika nchi yetu , Je ni wapi pa kuanzia? , Nini kifanyike?,Mchango wako ni muhimu kwa manufaa ya wengi! na Ndio sababu pia huu uzi uko hapa. Karibu.
th (1).jpg
 
Back
Top Bottom