Mwl.RCT
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 14,624
- 20,666
Wana JF naomba Ushauri na msaada wenu katika hili.
Nilikuwa masomoni katika chuo kimojawapo hapa Tanzania, kwa masomo ya shahada ya elimu (Sayansi) kwa mchepuo wa Fizikiana na Chemia, Bachelor of Education in Science- (Physics, Chemistry). Tangu Nov 2010 hadi June 2013 Nilipomaliza masomo.
Niliporudi toka masomoni nikakuta:-
-Barua ya shitaka la utoro kazini ya tarehe 15/06/2011
-Baraua ya Kusimamishwa kazi kwa nusu mshahara ya tarehe 15/06/2011
Nikaandika barua yangu ya utetezi, Tarehe 4/07/2013. Kamati ya nidhamu na maadili TSD ikaka kikao kifupi wakanihoji na kutoa maamuzi ya shauri langu la nidhamu barua ya tarehe 04/07/2013, Ambayo nilikabidhiwa nimpelekee mkuu wangu wa shule na niwe chini ya uangalizi wake. Kama inavyojieleza hapa chini.Kilichofuata baada ya TSD wilaya kutoa Maamuzi
· Afisa Elimu Sekondari alipinga maamuzi ya kamati ya TSD kwa kuhoji kwanini swala langu limeshughulikiwa mapema.
· Nikiwa bado sijaondoka kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya, Afisa Elimu Sekondari (W), Alimpigia simu mkuu wa shule na kumpa agizo asipokee wala kupitisha barua yangu yoyote.
· (Katibu TSD ndiye aliyenijulisha kwamba simu imeshapigwa kwa mkuu wa shule hivyo akaomba nimrudishie ile barua sababu haitopokelewa). Haya matukio ni ya tarehe 04/07/2013
Tarehe 08/07/2013, Nilirudi halmashauri ya Wilaya ili kufuatilia barua iliyozuiwa.
Katibu TSD (W) na Afisa utumishi (W) wakaenda kwa afisa Elimu Sekondari na kujadiliana kwa muda, waliporudi wakanikabidhi barua na tarehe 10/07/2013 barua ikasainiwa na kupitishwa na mkuu wa shule.
Je ni sawa kwa Mwalimu alieenda kusoma na kurudi kituoni kwake kupewa adhabu hii.
· Kuanza na mshahara wa Daraja TGTS C kana kwamba ni mwajiriwa mpya wa Diploma mwajiriwa mpya. (Nilipaswa kuwa daraja D, Ni miaka mitano imepita tangu niajiriwe na Serikali,Nimeajiriwa March 2008),
· Kutokudai Mishahara/ Nusu mshahara yote ya nyuma kipindi chote nilipokuwa masomoni.
· Afisa Elimu Sekondari(W) kuzuia nisipewe vipindi labda mpaka nitakapoingizwa kwenye Payrol,ndio atanitambua kama mtumishi. Kumbuka shule zimefunguliwa tangu tarehe 15/07/2013
Na ikumbukwe kuwa shule haina mwalimu wa Sayansi hata mmoja kati ya walimu wapatao 17, ukiacha mkuu wa shule ambaye mara mojamoaja hufundisha chemia.
Je kipi kifanyike ili haki itendeke?, Maana Mwezi sasa nipo nyumbani na familia yangu bila kujua hatma ya maisha yetu hapa ugenini.
Je nani anahusika kumuajibisha huyu Afisa Elimu Sekondari (W)?. Huyu Afisa Elimu kwa sasa ndiye anayekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji (w)
Kabla ya Kwenda masomoni: October 2010
· Niliomba ruhusa kwa maandishi nikiwa nimeamabatanisha Joining Instruction form toka chuo husika haikujibiwa.
· Nikamfuata ofisini Afisa Elimu Sekondari (W) kumuomba aweze kuniruhusu kwenda masomoni alikataa na kusisitiza iwapo utaondoka kwenda masomoni bila ruhusa yangu na kutokuwepo kituoni kwa siku 5 mfululizo basi nitazuia mshahara wako.
· Pia siku hiyo hiyo nilijadiliana naye kuhusu likizo bila malipo ili niende kusoma, bado alikataa kwa kunieleza yeye hausiki labda kama ningekua naenda kusoma masomo nje ya taaluma ya ualimu. (Sababu niliajiriwa kama mwalimu Baada ya kumaliza masomo ya astashahada ya elimu, Diploma Course in Education).
Nililazimika kwenda kuendelea na masomo mpaka nilipomaliza ndipo nikarudi kufuatilia mstakabali wa ajira yangu katiaka Halmashauri ya Wilaya husika. Kipindi chote nilichokuwa masomoni sikuwahi pokea mshahara wowote. Mpaka muda huu sina mshahara. Na haifahamiki nilini wataingiza taarifa zangu kwenye Payroll.
Utata katika hili la mishahara.
· Termination date ya mshahara inaonekana kwenye system ilifanyika tarehe 02/03/2012
· Slip salary ya mpaka Mwezi January 2012 Inaonyesha kuwa nimekuwa nikipokea mshahara kamili.
· Maelezo Hati ya shitaka ya 15/06/2011 inaonyesha nilipaswa kupokea Nusu mshahara mpaka shitaka langu litakapo kwisha.
· Mshahara ulisitishwa (kutokuingiza kwenye account yangu) tangu Mwezi November 2010.
Swali: Je hii fedha (mshahara) ambayo/ambao inaonekana kana kwamba nilikuwa nikipokea zilikuwa zinasainiwa na kuchukuliwa na nani?
Nawasilisha naomba mchango wenu wa mawazo wadau.
cc: Zitto , MALICK MUSSA , CHAMVIGA , Jimmy Kadebedebe , MKWELItu , Rajasili , onduru ogy , Evelyn Salt , Massawe G. I , Madame B , Mohamedi Mtoi

Last edited by a moderator: