Ushauri wa kitaalamu

Ushauri wa kitaalamu

Unyanga

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2011
Posts
402
Reaction score
83
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27, ila nimekuwa nina uzito mkubwa sana mpaka najiogopa, nina uzito wa kilo 98.5 kitu ambacho nahisi sio kizuri kwangu.

Kwa mara kadhaa nimekuwa nikikaribu kufanya mbinu za kupunguza uzito lakini nagonga mwamba, nimekuwa walau nikifunga wiki nzima nakufuturu machungwa tu, pia hufanya mazoezi kama kukimbia uwanja wa mpira mara nane kwa siku japo sio kila siku kutokana na majukumu mbali mbali, kuruka kamba walau mia tano kwa siku na kufanya mazoezi ya viungo, lakini mwili umekuwa haupungui kihivyo na isitoshe nikiacha mazoezi tu hata wiki ndo unarudi kwa kasi.

Vyakula ninavyotumia ni wali ugali, nyama, samaki, maharage na mikate mara kwa mara, pamoja na chipsi na mishikaki mara moja au mbili au mbili kwa wiki.

Kiukweli sina kitambi wala tumbo kubwa kihivyo ila nyama za tumbo ndo zinaongezeka. Plzzz kwa wataamu nishaurini nifanyeje walau nirejee kila 75 au 80 kwa muda mfupi.
 
Bwamdogo,

Kufunga kutokula hakusaidii lolote, ndiyo maana unasema manyama yanaanza kuongezeka. Katika milo yako mikuu samaki, kuku wa kuchemsha, maharagwe, mboga za majani na matunda ni muhimu sana. Vitu kama maparachichi, machungwa, maembe, mafyulisi, mapera, madafu na mapapai, ndizi za kuiva nk ni vya muhimu sana ktk milo yako,

Asubuhi kula kama mwehu (sio viporo), mchana kama chizi mdogo na jioni kuwa kama umevimbiwa so kula kidogo matunda, mboga za majani au hata kipande cha kuku wa kuchemsha. Kati ya hiyo milo mitatu mikubwa hakikisha unakula tunda na kunywa sana maji.

Mazoezi ni muhimu sana na kwa ratiba maalum. Mazoezi sio lazima kwenda gym, unaweza piga pushups kila ukiamka na kabla ya kulala, seat ups, au ruka kichura round kadhaa hapo nyumbani, kamba ni zoezi zuri, na ofisini kama upo peke yako au una nafasi unaweza funga mlango na kujinyosha, nyanyua mguu mmoja mmoja mbele, na pembeni, na kama una endesha gari basi ofisini ukifika paki mbali kabisa ili upate muda wa kutembea kidogo. Kama mna lift basi tumia ngazi, na kama unategemea usafiri wa magufuli basi mara moja moja unaweza shuka kituo cha nyuma au mbele na kutembea (kama vibaka sio ishu maana maisha bora ya kila mtanzania yapo bagamoyo tuu).

Mazoezi unaweza kufanya mara 3-5 kwa wiki na uwe na siku za mapumziko.

Achana na ma- chips mikate na punguza kabisa mambo ya ugali, wali na vyakula vya kukaanga.
 
Asante sana mkuu kwa ushauri ngoja nianze kuufuata
 
Back
Top Bottom