Ushauri wa kiuchumi kuhusu Dhahabu yetu kwa Serikali ya Tanzania

Ushauri wa kiuchumi kuhusu Dhahabu yetu kwa Serikali ya Tanzania

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo watakaoiuza ndani na nje ya Tanzania.

Hii ni wepesi sana kuhakikisha hatukaukiwi na fedha za kigeni na tunadhamana ya kutosha kukopa kwa masharti yetu. Uchumi tunao tunaukalia.

Niliwahi kuandika kuhusu dhahabu, ingawa mada nilikuwa sijaimaliza, lakini ilikuwa iishie kwenye ushauri nnaoutowa leo.

Niliwahi kuanza kuandika hivi:

- Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
 
Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo wtakaoiuza ndani na nje ya Tanzania...
Bei inao toka BOT iko chini ukiangalia na Market price ya dhahabu nje. BOT iki toa bei nzuri utakuja kuona 'Black Market' tena, labda kama una adopt command economy kama mwendazake, ambao imesha pita na wakati tuko kwenye 'free market economy' unauza pale ambapo unapata faida kubwa.
 
Ni maajabu sana, yaani umasikini mpaka kwenye fuvu
Tumepiga kelele sana kuhusu hili la kuwa na Gold reserves lakini wapi

Kuna nchi hawachimbi dhahabu wala hawana kabisa kwenye ardhi zao lakini wana hazina kibao tena ni tons za dhahabu

Leo kweli sisi ni wa kulia kukosa $
 
Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo wtakaoiuza ndani na nje ya Tanzania.

Hii ni wepesi sana kuhakikisha hatukaukiwi na fedha za kigeni. Uchumi tunao, tunaukalia.

Niliwahi kuandika kuhusu dhahabu, ingawa mada nilikuwa sijaimaliza, lakini ilikuwa iishie kwenye ushauri nnaoutowa leo.
Yaani Da FaizaFoxy hili jambo jema ila ukifanya watamuua hata waziri husika. Hizi ni cartel za wezi. Kama hospital ya Appolo ilitaka kufungua hapa Tanzania hospital kama ile ya India ila inasadikika cartel za hospital zingeua hata wahusika wote kama wangepitisha. Nchi zetu za kijinga sana yaani kuna vidume wamejimilikisha utajiri wetu halafu eti kila siku tunaimba umasikini hahaha
 
Ni maajabu sana, yaani umasikini mpaka kwenye fuvu
Tumepiga kelele sana kuhusu hili la kuwa na Gold reserves lakini wapi

Kuna nchi hawachimbi dhahabu wala hawana kabisa kwenye ardhi zao lakini wana hazina kibao tena ni tons za dhahabu

Leo kweli sisi ni wa kulia kukosa $
Tuna deficite national budget utakua je na reserve ya dhahabu kama kujanga simple flyover mpaka ukope hiyo reserve inakua na maana kweli? Jamani tafakari zaidi.
 
Ni maajabu sana, yaani umasikini mpaka kwenye fuvu
Tumepiga kelele sana kuhusu hili la kuwa na Gold reserves lakini wapi

Kuna nchi hawachimbi dhahabu wala hawana kabisa kwenye ardhi zao lakini wana hazina kibao tena ni tons za dhahabu

Leo kweli sisi ni wa kulia kukosa $
Kwakweli kwa hili inasikitisha sana. Tatizo naloliona wakubwa wanawaogopa hao tuliowakodishia migodi ya dhahabu. Magufuli alitingisha kidogo nadhani akawashindwa je nani ataweza? Lakini naamini atatokea atakaeweza.
 
Bei ya BOT iko chini ukiangalia Market price nje BOT iki offer bei nzuri utakuja kuona Black Market tena, labda kama una adopt command economy ambao imesha pita na wakati.
Naamini mleta mada amelenga, kukomesha wizi, utoroshaji na ujanjaujanja wa mauzo ya haya madini.
Hivyo hii ni njia nzuri mojawapo. Lakini je ikifanywa hivyo hao huko BOT wanaaminika au itafutwe njia zingine pia za udhibiti wa jinsi ya kuuza bidhaa zetu nje ya nchi?
Mm kwa mtazamo wangu mwiguru anahitaji kusaidiwa, maana naona kashindwa kusimamia uchumi wa nchi yetu.
Maana nimeona tangu mwanzo njia anazotumia kukuza uchumi ni za kizamani na hazisaidii kitu.shiling inazidi kupolomoka.kiufupi kila kitu hakiendi vizuri.
 
Unajuwa maana ya wanunue na wauze wao?

Kama ulikuwa huelewi hiyo ndiyo maana ya Biashara.

Bia = uza, shara = nunuwa.

Kwa Kiarabu rasmi kabisa, ambacho ndipo Kiswahili kiliilipata neno hilo.
Umeshaanza mahaba na Waarabu wako.

Nimekuuliza swali rahisi hiyo pesa ya kununuwa dhahabu kutoka Barrick na Ggm tunayo?

Au unataka BOT ijigeuze kuwa Dalali?
 
Back
Top Bottom