Ushauri wa kiuchumi kuhusu Dhahabu yetu kwa Serikali ya Tanzania

Shida Iko kwenye mikataba, serikali iliingia mikataba kandamizi. Hujiulizi kwanini kwenye mgodi Kuna uwanja wa ndege. Hata data zinazo tolewa ni uongo. Mfano. Mgodi wanasema wametoa kilo 50, kumbe kilo 500 Ili kukwepa Kodi. Sheria zetu zinawabeba wawekezaji. Na ukijifanya mjuaji, mabepari wanakuua.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Kiwanja cha ndege usikione ajabu kuwepo popote, ni kwa ajili ya usafiri wa haraka.

Data zinazotolewa na nani?

Mgodi upi unauongelea? Au ni fikra zako tu?

Sheria za uwekezaji wa Kimataifa ni sheria za Kimataifa.

Sasa hapa wewe hujajifanya "mjuaji"? Vipi, bado upi hai au "mabepari" wamesha "kuua"

"Kula uliwe" - Kikwete.
 
Tena wauzaji dhahabu wakiwa wajanja waseme kila dhahabu ya zaidi ya million 100 walipwe kwa hati fungani. Serikali haitokataa.
Serikali ina madeni ya ma billions mpaka ya stationeries na halipi mpaka kesho...
 
Yote uliyosema yanafanyika, na zaidi ya hayo.
Wakifaulu hili Tanzania itangara na itakuwa juu mno, e payment card, twende step by step, swap machine ziwe connected na tra, kwanza tra itakuwa inachukuwa chake mapema asubuhi, serekali itakujakuwa na fedha za kufuru
 
Binafsi sikubaliani kabisa na hii, yani mtu alipie vibali achimbe alafu umlazimishe akauze sehemu fulani, ni muhimu kuwa na vibali hususani kwa wanao export lakini isiwe lazima waiuzie serikali. Serikali yenyewe itengeneze soko la ushindani kuwavutia watu, Uchimbaji wa dhahabu ni biashara kama biashara nyingine na watu huweka mabilioni ya pesa. Shida apa naona ni tatizo la watanzania kuaminishwa kuwa Dhahabu ni yetu sote ,"Dhahabu yetu yote", Na hii inapelekea kuona watu waki export kama wanaiba vile wakati wamelipia vibali na wamewekeza pesa. Nikuhakikishie tu kwamba ukiendelea ku settle unasema "dhahabu yetu", hiyo dhahabu unayosema yetu sote siku utasikia imeisha nahujawahi ona hat a a single gram.
Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo watakaoiuza ndani na nje ya Tanzania.

Hii ni wepesi sana kuhakikisha hatukaukiwi na fedha za kigeni na tunadhamana ya kutosha kukopa kwa masharti yetu. Uchumi tunao tunaukalia.

Niliwahi kuandika kuhusu dhahabu, ingawa mada nilikuwa sijaimaliza, lakini ilikuwa iishie kwenye ushauri nnaoutowa leo.

Niliwahi kuanza kuandika hivi:

- Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
 
Binafsi sikubaliani kabisa na hii, yani mtu alipie vibali achimbe alafu umlazimishe akauze sehemu fulani, ni muhimu kuwa na vibali hususani kwa wanao export lakini isiwe lazima waiuzie serikali. Serikali yenyewe itengeneze soko la ushindani kuwavutia watu, Uchimbaji wa dhahabu ni biashara kama biashara nyingine na watu huweka mabilioni ya pesa. Shida apa naona ni tatizo la watanzania kuaminishwa kuwa Dhahabu ni yetu sote ,"Dhahabu yetu yote", Na hii inapelekea kuona watu waki export kama wanaiba vile wakati wamelipia vibali na wamewekeza pesa. Nikuhakikishie tu kwamba ukiendelea ku settle unasema "dhahabu yetu", hiyo dhahabu unayosema yetu sote siku utasikia imeisha nahujawahi ona hat a a single gram.
Kama hukubaliani ulilazimishwa?
 
Ni maajabu sana, yaani umasikini mpaka kwenye fuvu
Tumepiga kelele sana kuhusu hili la kuwa na Gold reserves lakini wapi

Kuna nchi hawachimbi dhahabu wala hawana kabisa kwenye ardhi zao lakini wana hazina kibao tena ni tons za dhahabu

Leo kweli sisi ni wa kulia kukosa $
Ni matokeo ya kuwa na Viongozi wa serikaki VIFUU!!!
 
Haswa Mkuu ila tutakuwa hivi mpaka lini? Wale vijana tuliodhani wataibadilisha nchi wameingia nao wamekuwa na tamaa na wanazeekea kwenye ajira hizi kila leo kupangiwa kazi zingine wanakuwa wanajipa wanaojuana
 
Ni maajabu sana, yaani umasikini mpaka kwenye fuvu
Tumepiga kelele sana kuhusu hili la kuwa na Gold reserves lakini wapi

Kuna nchi hawachimbi dhahabu wala hawana kabisa kwenye ardhi zao lakini wana hazina kibao tena ni tons za dhahabu

Leo kweli sisi ni wa kulia kukosa $
Hili lilianzishwa zamani sana, wakati wa Mkapa kama sikosei. BoT walianza kununuwa dhahabu, tatizo likawa wafanyakazi wa BoT walioaminiwa kununuwa dhahabu wakawa wanapiga dili, wananunuwa shaba iliyochovekwa kwenye maji ya dhahabu (coated)na kuisababishia nchi hasara kubwa.

Mpango ukafa na "vigogo" waiyoyafanya hayo wakaachiwa huru, alipokuja Kikwete akawashika kw mengine kabisa, akawaamia sasa mkajiulize kidogo, wakawa wanafagilishwa viwanja vya Hospita li ya Sinza. Kma umewasahau, mmoja wao ni Mramba.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi, kweli nawakumbuka kina Basil
Mramba na wenzie
Ila nchi imejaa uozo na watu wasiokuwa na huruma wala Soni na nchi yao

Ni sawa na mtoto kumuibia baba yake tu
Wizi na Rushwa havitaisha
 
Back
Top Bottom