imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Kweni ukosefu wa vipara umesababishwa "huyu bibi"? mbona Waziri wa Fedha alisema kuna reserve ya vipara bilioni tano?huyu bibi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweni ukosefu wa vipara umesababishwa "huyu bibi"? mbona Waziri wa Fedha alisema kuna reserve ya vipara bilioni tano?huyu bibi
Bibi hamna kitu uliza wa Suriname watakwambiaKweni ukosefu wa vipara umesababishwa "huyu bibi"? mbona Waziri wa Fedha alisema kuna reserve ya vipara bilioni tano?
Dhahabu unadhani haichimbwi mrangi? Wachimbaji wadogo wanapata sana dhahabu na serikaki ina uwezo wa ku collect ya kutosha sana tuu kwa ajili ya kuitumia kama fedha za kigeni .ni kwamba tu bado naona serikali haijaweka nia ya dhati na mkazo kwenye uchumi huu wa vito. Sisi ni matajiri sanaa.Njoo lindi nkupe maeneo na wewe ujichukulie dhahabu
Mjipange kwanza ndiyo muanze na nyie mnunue dhahabu mjiweke gold reserve yenu
Ova
No wanunuwe wachumba wako wa Walodi.Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo wtakaoiuza ndani na nje ya Tanzania.
Hii ni wepesi sana kuhakikisha hatukaukiwi na fedha za kigeni. Uchumi tunao, tunaukalia.
Niliwahi kuandika kuhusu dhahabu, ingawa mada nilikuwa sijaimaliza, lakini ilikuwa iishie kwenye ushauri nnaoutowa leo.
Niliwahi kuanza kundika hivi:
Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
Nilijibu uzi fulani humu JF kwa haya: Ni mengi sana yanaongelewa lakini ni wachache sana wenye uelewa wa mambo ya uchumi mkubwa na teknolojia za kuzalisha uchumi mkubwa yanavyoendeshwa na hao wenye teknolojia hiyo, ambao ndiyo hao hao wenye uchumi mkubwa. Kama hiyo haitoshi, ndiyo hao hao...www.jamiiforums.com
Ukiacha ushabiki mandazi wa Udini na uccm hapa unaonesha unaakili kidogo.Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo wtakaoiuza ndani na nje ya Tanzania.
Hii ni wepesi sana kuhakikisha hatukaukiwi na fedha za kigeni. Uchumi tunao, tunaukalia.
Niliwahi kuandika kuhusu dhahabu, ingawa mada nilikuwa sijaimaliza, lakini ilikuwa iishie kwenye ushauri nnaoutowa leo.
Niliwahi kuanza kundika hivi:
Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
Nilijibu uzi fulani humu JF kwa haya: Ni mengi sana yanaongelewa lakini ni wachache sana wenye uelewa wa mambo ya uchumi mkubwa na teknolojia za kuzalisha uchumi mkubwa yanavyoendeshwa na hao wenye teknolojia hiyo, ambao ndiyo hao hao wenye uchumi mkubwa. Kama hiyo haitoshi, ndiyo hao hao...www.jamiiforums.com
Waziri mwenye dhamana na katibu wake wangeweza kabisaKwakweli kwa hili inasikitisha sana. Tatizo naloliona wakubwa wanawaogopa hao tuliowakodishia migodi ya dhahabu. Magufuli alitingisha kidogo nadhani akawashindwa je nani ataweza? Lakini naamini atatokea atakaeweza.
Katiba na tume huru ya uchaguzi kwanza acha kucheza na maneno.Eti sisi leo ni wakupitwa na Kenya kiuchumi hawachimbi hata mchanga hapo Kenya nchi imejaa udongo mtupu ile. Botswana inakaribia kufikia nchi za ulaya kwa GDP lakini wameweza baada ya ku manage vizuri dhahabu yao.
Hapa ndo tunapofeli viongozi wamesoma lakini akili hawana. Tunapata tabu na mali tunazo Mungu atatuuliza niliwapa kila kitu watanzania mlitaka niwafanyie nini tena?. Rais anahitaji kushauriwa tuu tena tuna rais msikivu sana na mwelewa.Na kama linaendelea bas kwa % chache sna kwa nchi hii
Ndio anashauri sasa hizo sera za ubinafsishaji zitungiwe sheria upya zibadilishwe serikali inunuee dhahabu.Ndugu Faiza Foxy, Nasikitika unatoa ushauri uliopitwa na wakati. Nadhani bado unaishi zama za Nyerere na enzi za ucommunist . Sasa hivi kila kitu kinasukumwa na nguvu ya soko, wewe unawaza itungwe Sheria ya kuzuia watu wasiuze wanakotaka.!! Dhahabu yenu ni yenu kwasababu inachimbwa kwenye ardhi yenu, lakini kiuhalisia siyo yenu kwasababu yote mlishaibinafisisha kwa wageni.
Nakuelewa usemalo.Yaani Da FaizaFoxy hili jambo jema ila ukifanya watamuua hata waziri husika. Hizi ni cartel za wezi. Kama hospital ya Appolo ilitaka kufungua hapa Tanzania hospital kama ile ya India ila inasadikika cartel za hospital zingeua hata wahusika wote kama wangepitisha. Nchi zetu za kijinga sana yaani kuna vidume wamejimilikisha utajiri wetu halafu eti kila siku tunaimba umasikini hahaha
Sidhani kama wana majibu ya kueleweka hawa viongozi wetu hata huko kwenye cabinet sijui agenda zinazojadiliwa ni zipi kama masuala ya msingi kama haya hawayaoni.Waziri mwenye dhamana na katibu wake wangeweza kabisa
Tusiende mbali hapa Africa Algeria wana 174 metric tons of gold reserves na ndio wanaongoza Africa
Huo ni utajiri tosha kwa miaka kadhaa
Ngozi nyeusi ni mtihani
Wizi wa kijinga na hawatumii akili
Tumuulize waziri wa fedha na gavana wetu kwanini hatuna dhahabu ya akiba?
Kwani mikataba ikigeuzwa ama tuseme sera ielekeza hao "wachimbaji wakubwa" waajiriwe kwa kazi ya kuchimba na kuchenjua na kulipwa kwa kazi hiyo tu.Unachosema ndio ukweli angalau kwa wachimbaji wadogo tunaweza kuwadhibiti serikali ikanunua. Kwa wakubwa ni shughuli pevu
Meshindwa kumaliza tatizo la madarasa na matundu ya choo leo hii ndio mtaweza kununua dhahabu.Ipitishwe sheria bungeni, dhahabu yetu yote, inayochimbwa na wachimbaji wadogo na wakubwa inunuliwe na BOT, kitengo cha hazina ya Taifa. Na wao pekee ndiyo wtakaoiuza ndani na nje ya Tanzania.
Hii ni wepesi sana kuhakikisha hatukaukiwi na fedha za kigeni. Uchumi tunao, tunaukalia.
Niliwahi kuandika kuhusu dhahabu, ingawa mada nilikuwa sijaimaliza, lakini ilikuwa iishie kwenye ushauri nnaoutowa leo.
Niliwahi kuanza kundika hivi:
Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na Laana zake
Nilijibu uzi fulani humu JF kwa haya: Ni mengi sana yanaongelewa lakini ni wachache sana wenye uelewa wa mambo ya uchumi mkubwa na teknolojia za kuzalisha uchumi mkubwa yanavyoendeshwa na hao wenye teknolojia hiyo, ambao ndiyo hao hao wenye uchumi mkubwa. Kama hiyo haitoshi, ndiyo hao hao...www.jamiiforums.com
Katiba na tume huru havitakusaidia kama hatujabadili mindset za viongozi wetu. Unadhani ukibadili katiba na tume ndio viongozi watashindwa kuvunja hiyo katiba? Mara ngapi magufuli kavunja katiba na hakuna wa kumwambia kitu. Upinzani msidhani katiba ikibadilishwa CCM ndio itaondoka madarakani mnajidanganya. Katiba itabadilika na tume itabadilika lakini kama CCM hawataki kuachia madaraka mtabaki kumshtakia Mungu tu.Katiba na tume huru ya uchaguzi kwanza acha kucheza na maneno.
Sio serikali hii ya wezi wa ccm mtakuta majivu huko Biotiii.Unachosema ndio ukweli angalau kwa wachimbaji wadogo tunaweza kuwadhibiti serikali ikanunua. Kwa wakubwa ni shughuli pevu
Utaratibu huo unawezekana ila mpaka iwezekane ndio kazi ilipo. Haya makampuni ya uchimbaji makubwa ni makampuni ya nchi za magharibi marekani haswaa na Uingereza na hii dhahabu inapelekwa huko kwahiyo ukiamua kufanya hivyo ni kwamba Tanzania inataka marekani na Uingereza wasiwe na dhahabu sasa fikiria reaction yake hapo.Kwani mikataba ikigeuzwa ama tuseme sera ielekeza hao "wachimbaji wakubwa" waajiriwe kwa kazi ya kuchimba na kuchenjua na kulipwa kwa kazi hiyo tu.
Yaani serikali iwe na kampuni ya kulipa wachimbaji, kununua na kuuza dhahabu kwenye masoko ya nje.
Siyo utaratibu mbovu uliopo sasa wanachimba na kumiliki dhahabu na kuuza watakako na serikali kuambulia royalty ya kidwanzi.
Kwani utaratibu huo hauwezekani?
Tukiwa na akili za wizi basi ndio tukubali kuishi maisha haya ya umasikini wa kujitakia kila mmoja apambanie tumbo lake.Sio serikali hii ya wezi wa ccm mtakuta majivu huko Biotiii.