Ushauri wa kukopa na kujenga

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
2,399
Reaction score
1,014
Tafadhali rejea hapo juu nataka kukopa kama milioni 10 nimalizie NYUMBA niliyoianza kuijenga mwaka Jana Kwa mkopo mwingine kwa sasa nikipata hiyo m10 nitamaliza bati NA MADIRISHA
 
Tafadhali rejea hapo juu nataka kukopa kama milioni 10 nimalizie NYUMBA niliyoianza kuijenga mwaka Jana Kwa mkopo mwingine kwa sasa nikipata hiyo m10 nitamaliza bati NA MADIRISHA
Unapokopa ni lazima uwe na source nyingine mbadala ya uhakika wa kuweza kulipa deni. Bila shaka hiyo unayo, iwapo unataka kutegemea nyumba hiyo unayoijenga kama kitega uchumi cha kurudisha yenyewe deni lake angalia kwa makini lengo hilo kutokana na location ya nyumba ilipo (Kwa kupangisha) na gharama yake kimaslahi. Vile vile iwapo unataka kumaliza nyumba hiyo ili uishi mwenyewe ni vyema iwapo kama utakuwa unasave kiasi kikubwa cha pesa ambacho ulikuwa ukilipa kama kodi na kuihamishia benki kulipa deni ( Hii inategemeana na Kiasi cha Marejesho utakachopangiwa). Muhimu ni kuwa makini na malengo yako yasije kukutumbukiza kwenye deni kubwa litakalokugharimu maradufu. Na pia kutumia pesa hiyo kwa malengo kusudiwa. All the best!
 
Hiyo siyo smart choice.

Kifupi utataabika kurudisha mkopo.

Hebu fikiria hivi.

Kama sehemu utakayochukulia mkopo wanataka interest rate ya chini kabisa let say 10% hapo maana yake utalipa 1m juu ya hiyo 10m unayokopa.

Lakini ukiende mbele zaidi utagundua hiyo nyumba unayojenga wala si asset kwasababu unataka uishi humo.

Kwahiyo utalazimika kulipa bills, umeme na maji.

Pia utaingia gharama ndogo ndogo za repair kila wakati inapobidi kufanya hivyo.

Haya mambo yanachomoa pesa mfukoni mwako.

Usipo kuwa makini you will end up in debt trap.

Nakushauri kopa fedha unabopata deal ya biashara.

Naposema deal namaanisha umeshapata wateja tayari kwahiyo unatumia mkopo wa benk kama levarage.

Mkuu badilisha mtazamo wako kuhusu mkopo na fedha utaona jinsi ilivyo rahisi.

Let me know what you think.
 
Tafadhali rejea hapo juu nataka kukopa kama milioni 10 nimalizie NYUMBA niliyoianza kuijenga mwaka Jana Kwa mkopo mwingine kwa sasa nikipata hiyo m10 nitamaliza bati NA MADIRISHA
Ni wazo zuri, wasiliana na TUJENGE utapata ushirikiano nzuri na kufanikisha kumalizia nyumba yako
 
Inahitaji kutuliza akili.

Kukopa ili ukamalizie nyumba kwangu ni ngumu kidogo kukubaliana nawe

Atleast ukope hiyo 10 mil uchukue mil 5 umaliziea upande mmoja wa nyumba uhamie then mil 5 nyingine uingize kwenye mzunguko ili uwe unapata vijihela vya kusukuma siku ambavyo ukiwa makini nazo unaweza kumalizia sehemu iliyobaki ya nyumba.

Kuliko mil 10 yote kuielekeza kwenye ujenzi unaleta ukakasi kidogo in case umepata tatizo kubwa la ghafla.

Narudia tena kuwa makini,tafakari kwa kina

Kamwe usiruhusu mkopo uje kukutia fedheha mbele za watu.

May Allah Right Your Dreams.
 
Nilishakataa kamwe.....

Sitokopa kujenga au kumalizia nyumba ya kuishi.

Ntakopa kuongeza mzunguko wa biashara, ela ya ujenz wa nyumba ya kuishi itatokana na faida inayotokana na mzunguko wa biashara.

Vinginevyo unajenga Guest house, Ukumbi wa kukodisha au Apartment
 
Mshahara wako ni kiasi gani na baada ya mkopo, mabaki ya mshahara yatatosha kuihudumia familia bila usumbufu?

If yes, kopa if not usikope
 
Mkopo wa kwa ajili ya kujenga = umasikini. Mkopo wa kwanza au kumaliza nyumba wa pili utaweka madirisha, milango na finishing ni mkopo wa 3 au ? . Zinduka kopa hela izalishe faida jengea,sio kuzika pesa.
 
Kama rejesho la mkopo wako ni kutoka kwenye mshahara wako na ni mtumishi wa umma usijiulize mala mbili mbili kakope malizia nyumba yako

Kama rejesho lako la mkopo ni kutokana na biashara zako my dear achana na hill wazo biashara zinakufa kila siku kwa sasa hali ya kibiashara siyo nzuri, ukitembelea tasisi za kifedha hususani mabank sana Mali nyingi za wateja wanaziuza kisa wadaiwa wamekosa kufanya marejesho


Nyumba ni kitu cha kudumu, biashara zipo tu madau ukijenga leo utaabika mda mfupi kisha utatafuta pesa ya biashara ukiwa tayali unakwako
 
mkuu dhamira kuu ya mkopo ni kuwekeza kwenyevitu virudishavyo hela. usiweke hela kwenye liability utaumia sana ka mkuu mmoja amesema unaingia kwenye dept trap.

Pata mkopo wekeza katika biashara ambayo unaona inaredesha then pata hela toka kwenyebiashara then jenga taratibu pasipo presha na maumivu makali, ila kama unabiashara nyingine inakuingizia vizuri unaweza chukua huo mkopo bila shida ila ka huna fanya kutathimini sana ila sikuzote usichukue mkopo kwaajili ya liability mkuu.
 
Other things being constant.
Je kuna uhakika gani ya kuwa biashara italipa?
 
Mfano nimepanga kila mwezi kodi 200,000 salary take home haifiki 600k. Je nikikopa na kujenga then 200,000 ya kodi iwe inalipa loan badala ya kupanga nalo ni kosa.
 
Mwenzio anakwambia akope amalizie milango na madirisha, sio amalizie nyumba

Mkopo mbaya sana huu
 
Kopa malizia uhamie au upangishe hakikisha kiasi utakachokopa kitamaliza nyumba yako
Akope aimalizie halafu aipangishe yote ili umsaidie marejesho. Kumbuka usipoweza kumiliki nyumba now while working ukistaafu kwa hizi kanuni mpya za 25% take home nyumba utaiona kwa Wenzio.
 
Mkuu Uwoga acha woga... kama upo chini ya 35 usi-panic na hii mikopo ya nyumba mkuu maana nyumba hata ukope vipi huwa haziishi maana mahitaji ya nyumba ni mengi ....angalau ungekuwa umekomaa na kupiga bati na ma-grill kwa hela zako ndogondogo alafu ukikopa unaitumia kumalizia kabisa vitu vya msingi na kuingia ndani
 
Akope aimalizie halafu aipangishe yote ili umsaidie marejesho. Kumbuka usipoweza kumiliki nyumba now while working ukistaafu kwa hizi kanuni mpya za 25% take home nyumba utaiona kwa Wenzio.
Kwani akipangisha analipwa mavu.... ? Nachomanisha ni kuwa waweza jenga nyumba ukawa mbali nayo kwa sababu ya uhamisho ukapangisha ili ikupunguzie mzigo wa makato ya mkopo au ukiishi mwenyewe maana yake umeepukana na kodi ya kila mwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…