Ushauri wa lishe kwa watu wenye Shinikizo kubwa la damu (Hypertension)

Ushauri wa lishe kwa watu wenye Shinikizo kubwa la damu (Hypertension)

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Watu wenye changamoto ya shinikizo kubwa la damu hupaswa kufuata masharti sahihi ya mlo ili kupunguza athari za ugonjwa huu, pamoja na kusaidia katika udhibiti wake.

Kwa kuzingatia umuhimu wa lishe kama sehemu ya mkakati muhimu wa kuboresha afya kwa watu wenye changamoto hii, Shirika la afya Duniani (WHO) hushauri mambo yafuatayo-
  • Punguza matumizi ya Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi. Husaidia kushusha msukumo wa damu pamoja na kupunguza nafasi ya kuugua kiharusi
  • Tumia vyakula vyenye kiasi kikubwa cha madini ya Potassium hasa mboga za majani na matunda. Ni madini muhimu katika kudhibiti kupanda kwa shinikizo la damu
  • Shiriki mazoezi mepesi yanayoongeza utimamu wa mwili
  • Wekeza muda mwingi kwenye ulaji wa Mtindo wa DASH (Dietary Approaches to Stopping Hypertension) ambao huhusisha matumizi ya nafaka zisizo kobolewa, ulaji wa mafuta kidogo, kutokutumia nyama nyekundu, ulaji mkubwa wa matunda na mboga za majani pamoja na kupunguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi.

Shinikizo kubwa la damu ni ugonjwa unaoongeza nafasi ya kupatwa na kiharusi, kuugua magonjwa mbalimbali ya mfumo wa damu na moyo pamoja na kufeli kwa figo hivyo ni muhimu kufuata kanuni sahihi za lishe huku matumizi ya dawa za kutibu tatizo hili yakidumishwa.

Chanzo: WHO
 
Mkuu Kurunzi salam kwako. Nakubaliana na wewe kuwa walivyoeleza hii "Detonic" imekaa kipromo sana ikizingatiwa hawajaeleza "Side Effects' zake. ningetamani kutoka kwako na kwa wadau wengine hasa "Doctors" kuhusu hii Idea ya kusafisha mishipa na jinsi inaweza kuwa tiba mbadala ya vidonge kwa wale wenye shinikizo la damu.
Ahsante
 
Back
Top Bottom