Habari mkuu naomba nikujibu kwa uelewa wangu.
Vifaa vinahitajika
1. Sehemu/frame ya kufanyia kazi.
Hapa ni sehemu pa kufanyia kazi, malipo ya frame hutegeana na sehemu yenyewe.
2. AC Welding machine (stick/arch Welding).
Bei zake zinaanzia TZS 300K Kwa machine ndogo, Nzuri zaidi Ni zile za kusukwa mtaani. Jambo la kuhakikisha tu unapata fundi mzuri wa kusuka welding machine ( Kama uko Mbeya naweza kukuelekeza kwa mafundi wazuri wa usukaji machine)
3.Welding stick.
Hizi Ni stick kwa ajili ya kuchomelea, hua Zina size mbali mbali, Bei yake Ni TZS 15K -17K kwa KG 3.
4.Angle grinder
Hii itatumika kukatia vyuma au kunolea vyuma. Hapa aina/brand zinazopendelewa zaidi ni angle grinder za Makita au Bosch. Bei zake huanzia TZS 350K. Unaponunua kuwa makini kutambua Makita au Bosch original maana copy zimejaa sana.
5. Cutting disk/ grinding disk.
Hizi ni kwa ajili ya kukata au kunoa vyuma. Bei ya reja reja ni TZS 5K kwa cutting disk moja kwa huku nilipo.
Cutting disk za kampuni ya PS FORTE zinazotengenezwa South Africa hudumu Zaidi ,sijajua brand nyingine.
6.Meza ya Chuma.
Hii ni kwa ajili ya kukunjia maua ya mageti au fensi au madirisha. Bati lake la juu liwe angalau ni plate ya 6mm. Miguu yake bomba za Chuma aina black pipe, ziwe na diameter angalau 1-1.5 Inch.
***********************
Nitaendelea.
7. Bench Vice.
Hiki kifaa hufungwa kwenye meza ya Chuma, hiki kifaa hutumika kubana vyuma ili uweze kuvikata vizuri na kwa urahisi. Japo Kama ndio unaanza sio ya muhimu sana, unaweza kua unakata vyuma juu ya meza ya Chuma bila vice Ila inachosha na kuleta ugumu fulani. In the long run Ni muhimu kuwa na ili kurahisisha kazi ya ukataji vyuma.
Bei ya vice iliyotengenezwa kwa forging huenda mpaka TZS 500k na ndio vice imara ukifunga umefunga mpaka mjukuu ataitumia,
Zipo zilizotengenezwa kwa kumelea (Welding) au kwa kufungwa bolts na nuts Bei yake huwa chini ya hapo.
Vice huwa inafungwa juu ya meza ya Chuma asubuhi unapofungua ofisi na kuifungua jioni unapofunga ofisi ili kuepusha wezi kuiiba.
8.Futi (Tape measure).
Hutumika kupima urefu wa vyuma. Zipo za TZS 3K, 5K huuzwa kulingana na urefu was tape yake
9.Hacksaw( Msemeno wa mkono).
Hutumika kukatia vyuma vilivyopimwa kwa futi(tape measure) ili viweze kutumika kwa geti,fensi, Mlango n.k
Bei ya frame yake Ni TZS 2K, 3.5K n.k , blade yake huuzwa TZS 2K.
(Hacksaw Frame ya kutengeza mwenyewe hua imara zaidi kuliko za kununua dukani)
10.Nyundo.
Kwa ajili ya kugonga
11. Compressor.
Kwa ajili ya kupulizia rangi mageti,fensi,vitanda, madirisha n.k. Ukiaanza na ka compressor kadogo sio mbaya.
12.Rangi.
Red oxide, Prima n.k, huuzwa kwa jumla au reja reja madukani.
13.Puti.
Hutumika kufanyia finishing kabla ya rangi kupulizwa. Huuzwa pia jumla au reja reja kipimo kidogo kuanzia TZS 2K. Ni vizuri kununua kopo zima kwa ajili ya matumizi endelevu.
14. Material (vyuma).
Furniture tube, black pipe, hollow section, angle bar, flat bar, nondo,solid section n.k
Size zake huanzia nusu Inch,robo tatu, 1, moja robo, moja nusu n.k
Kwa nondo size huanzia 8mm,10mm n.k
Bei zake hutegeana na mkoa na mkoa zungukia maduka ya hardware kupata Bei zake.
Ni vizuri zaidi kununua material (vyuma) kwa jumla ila frame yako iwe na mahali pa kuhifadhia. Kununua vitu kwa Bei ya jumla husaidia kuongeza faida.
15. Drilling machine.
Kwa ajili ya kutobolea mashimo kwenye vyuma, Kama utakuwa na utengeneza vitanda vya chuma, kutengeneza majukwaa ya magari ya matangazo (PA), kuezeka kwa Chuma/Paa za Chuma, utahitaji drilling machine.
16.Angle line (90 degree).
Hiki kifaa husaidia kukata Chuma ili kuweza kutengeneza Kona ya 90 degree kwenye frame ya geti, dirisha, mlango n.k.
17. Maka Peni.
Kwa ajili ya kumaki vipomo vyako, mfano kwenye bati la Chuma(sheet).
****************
Naomba niishie hapo, Kama kuna Cha kuongeza nitaongeza.