Ushauri wa Mahitaji kuhusu biashara ya kuchomelea (welding)

SEASON 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
481
Reaction score
1,008
Nakuja kwenu ndugu zangu naomba kwa wenye uzoefu na wenye taarifa sahihi kuhusu biashara ya welding (kuchomelea) naomba kujua

gharama ya vifaaa vinavyohitajika,
Aina ya vifaa na Bei zake
Ubora wa Kifaaa na Madhaifu ya vifaa husika
Makadirio kwa vifaa vyote mpaka fundi anaanza kuchomelea Geti au dirisha linasimama tayari kwenda site itahitaji mtaji kiasi gani?

naomba msaada wenu naamini mpo wengi ambao mnafahamu tips ya vitu kadhaa kuhusu hili jambo langu nililowashirikisha.
 
Habari mkuu naomba nikujibu kwa uelewa wangu.
Vifaa vinahitajika

1. Sehemu/frame ya kufanyia kazi.
Hapa ni sehemu pa kufanyia kazi, malipo ya frame hutegeana na sehemu yenyewe.

2. AC Welding machine (stick/arch Welding).
Bei zake zinaanzia TZS 300K Kwa machine ndogo, Nzuri zaidi Ni zile za kusukwa mtaani. Jambo la kuhakikisha tu unapata fundi mzuri wa kusuka welding machine ( Kama uko Mbeya naweza kukuelekeza kwa mafundi wazuri wa usukaji machine)

3.Welding stick/Electrodes.
Hizi Ni stick kwa ajili ya kuchomelea, hua Zina size mbali mbali, Bei yake Ni TZS 15K -17K kwa KG 5.

4.Angle grinder
Hii itatumika kukatia vyuma au kunolea vyuma. Hapa aina/brand zinazopendelewa zaidi ni angle grinder za Makita au Bosch. Bei zake huanzia TZS 350K. Unaponunua kuwa makini kutambua Makita au Bosch original maana copy zimejaa sana.

5. Cutting disk/ grinding disk.
Hizi ni kwa ajili ya kukata au kunoa vyuma. Bei ya reja reja ni TZS 5K kwa cutting disk moja na TZS 8K kwa grinding disk moja kwa huku nilipo.

Cutting disk/grinding disk za kampuni ya PS FORTE zinazotengenezwa South Africa hudumu Zaidi ,sijajua brand nyingine.

6.Meza ya Chuma.
Hii ni kwa ajili ya kukunjia maua ya mageti au fensi au madirisha. Bati lake la juu liwe angalau ni plate ya 6mm. Miguu yake bomba za Chuma aina black pipe, ziwe na diameter angalau 1-1.5 Inch.

***********************
Nitaendelea.
 
Habari mkuu naomba nikujibu kwa uelewa wangu.
Vifaa vinahitajika

1. Sehemu/frame ya kufanyia kazi.
Hapa ni sehemu pa kufanyia kazi, malipo ya frame hutegeana na sehemu yenyewe.

2. AC Welding machine (stick/arch Welding).
Bei zake zinaanzia TZS 300K Kwa machine ndogo, Nzuri zaidi Ni zile za kusukwa mtaani. Jambo la kuhakikisha tu unapata fundi mzuri wa kusuka welding machine ( Kama uko Mbeya naweza kukuelekeza kwa mafundi wazuri wa usukaji machine)

3.Welding stick.
Hizi Ni stick kwa ajili ya kuchomelea, hua Zina size mbali mbali, Bei yake Ni TZS 15K -17K kwa KG 3.

4.Angle grinder
Hii itatumika kukatia vyuma au kunolea vyuma. Hapa aina/brand zinazopendelewa zaidi ni angle grinder za Makita au Bosch. Bei zake huanzia TZS 350K. Unaponunua kuwa makini kutambua Makita au Bosch original maana copy zimejaa sana.

5. Cutting disk/ grinding disk.
Hizi ni kwa ajili ya kukata au kunoa vyuma. Bei ya reja reja ni TZS 5K kwa cutting disk moja kwa huku nilipo.

Cutting disk za kampuni ya PS FORTE zinazotengenezwa South Africa hudumu Zaidi ,sijajua brand nyingine.

Elon Mzebuluni endelea ndugu yangu nasoma taratibu na kwa umakini mkubwa sana
 
Hizo AC welding Machine naziona kwa mafundi welding zile ndogo za kubeba kama brief case,vipi ubora wa zile ndogo mkuuu zina kuaga na matatizo na bei zake zipo vipi?
 
Elon Mzebuluni na hizii welding za kusukwa Zinakuaga na matatizo gani kiufundi? haziharibiki haribiki,na kama zikiharibika hasa zinaharibika kitu gani na zinatengenezeka au ndo ikiharibika unanunua mpya tu?
 
7. Bench Vice.
Hiki kifaa hufungwa kwenye meza ya Chuma, hiki kifaa hutumika kubana vyuma ili uweze kuvikata vizuri na kwa urahisi. Japo Kama ndio unaanza sio ya muhimu sana, unaweza kua unakata vyuma juu ya meza ya Chuma bila vice Ila inachosha na kuleta ugumu fulani. In the long run Ni muhimu kuwa na ili kurahisisha kazi ya ukataji vyuma.
Bei ya vice iliyotengenezwa kwa forging huenda mpaka TZS 500k na ndio vice imara ukifunga umefunga mpaka mjukuu ataitumia,
Zipo zilizotengenezwa kwa kumelea (Welding) au kwa kufungwa bolts na nuts Bei yake huwa chini ya hapo.
Vice huwa inafungwa juu ya meza ya Chuma asubuhi unapofungua ofisi na kuifungua jioni unapofunga ofisi ili kuepusha wezi kuiiba.

8.Futi (Tape measure).
Hutumika kupima urefu wa vyuma. Zipo za TZS 3K, 5K huuzwa kulingana na urefu was tape yake

9.Hacksaw( Msemeno wa mkono).
Hutumika kukatia vyuma vilivyopimwa kwa futi(tape measure) ili viweze kutumika kwa geti,fensi, Mlango n.k
Bei ya frame yake Ni TZS 2K, 3.5K n.k , blade yake huuzwa TZS 2K.
(Hacksaw Frame ya kutengeza mwenyewe hua imara zaidi kuliko za kununua dukani)

10.Nyundo.
Kwa ajili ya kugonga

11. Compressor.
Kwa ajili ya kupulizia rangi mageti,fensi,vitanda, madirisha n.k. Ukiaanza na ka compressor kadogo sio mbaya.

12.Rangi.
Red oxide, Prima n.k, huuzwa kwa jumla au reja reja madukani.

13.Puti.
Hutumika kufanyia finishing kabla ya rangi kupulizwa. Huuzwa pia jumla au reja reja kipimo kidogo kuanzia TZS 2K. Ni vizuri kununua kopo zima kwa ajili ya matumizi endelevu.

14. Material (vyuma).
Furniture tube, black pipe, hollow section, angle bar, flat bar, nondo,solid section n.k
Size zake huanzia nusu Inch,robo tatu, 1, moja robo, moja nusu n.k
Kwa nondo size huanzia 8mm,10mm n.k
Bei zake hutegeana na mkoa na mkoa zungukia maduka ya hardware kupata Bei zake.
Ni vizuri zaidi kununua material (vyuma) kwa jumla ila frame yako iwe na mahali pa kuhifadhia. Kununua vitu kwa Bei ya jumla husaidia kuongeza faida.

15. Drilling machine.
Kwa ajili ya kutobolea mashimo kwenye vyuma, Kama utakuwa na utengeneza vitanda vya chuma, kutengeneza majukwaa ya magari ya matangazo (PA), kuezeka kwa Chuma/Paa za Chuma, utahitaji drilling machine.

16.Angle line (90 degree).
Hiki kifaa husaidia kukata Chuma ili kuweza kutengeneza Kona ya 90 degree kwenye frame ya geti, dirisha, mlango n.k.

17. Maka Peni.
Kwa ajili ya kumaki vipomo vyako, mfano kwenye bati la Chuma(sheet).

****************
Naomba niishie hapo, Kama kuna Cha kuongeza nitaongeza.
 
Mkuu Elon Mzebuluni nakushukuru sana ndugu yangu kwa moyo wako wakujitoa kujibu maswali na mahitaji yangu lakini naomba usinichoke nina maswali zaidi

kuna huu msumeno wa mkono ni wa kazi gani tena kama tayari mtu utakua tayari na grander ambayo unaweza kukatia vyuma/bomba?

lakini compressor hii huwa inauzwa kiasi gani hyo ndogo ya kuanzia tu inaweza cost kiasi gani mkuu? lakini kuna maswali zaidi huko juu nimekuuliza nitafurahi kama ukiyajibu pia,asante tena mkuu.
 
Hizi Bench Vice za kutengeneza zinapatikana wapi?
 
Hizo AC welding Machine naziona kwa mafundi welding zile ndogo za kubeba kama brief case,vipi ubora wa zile ndogo mkuuu zina kuaga na matatizo na bei zake zipo vipi?
Zile AC welding machine ndogo (viportable) mafundi wengi huwa wanazitumia wakienda site, zile mkuu kwa kazi nzito (heavy duty) hazistahili utashangaaa machine imeungua, ila zipo machine viportable ambazo Ni heavy duty na Bei zake zimesimama, kuanzia TZS 600K utapata portable AC welding machine nzuri. Zipo za TZS 300K ila zitasumbua kwa kazi nzito.
 
Elon Mzebuluni na hizii welding za kusukwa Zinakuaga na matatizo gani kiufundi? haziharibiki haribiki,na kama zikiharibika hasa zinaharibika kitu gani na zinatengenezeka au ndo ikiharibika unanunua mpya tu?
AC welding machine za kusukwa mtaani ukipata fundi mzuri akakusukia machine heavy duty kwa kutumia material sahihi unaweza kutumia machine mpaka miaka 7+ bila kusumbua. Yanaweza kutokea matatizo madogo madogo kama mashine kutoa Moto mdogo Sana au mkali sana ama machine ukiunganisha earth wire inajizima yenyewe n.k. Matatizo hayo hurekebishika pasipo kununua machine nyingine.
 
Mkuu Elon Mzebuluni nakushukuru sana ndugu yangu kwa moyo wako wakujitoa kujibu maswali na mahitaji yangu lakini naomba usinichoke nina maswali zaidi

kuna huu msumeno wa mkono ni wa kazi gani tena kama tayari mtu utakua tayari na grander ambayo unaweza kukatia vyuma/bomba?

lakini compressor hii huwa inauzwa kiasi gani hyo ndogo ya kuanzia tu inaweza cost kiasi gani mkuu? lakini kuna maswali zaidi huko juu nimekuuliza nitafurahi kama ukiyajibu pia,asante tena mkuu.
Usijali mkuu nitayajibu yote kwa kadri niwezavyo.

Msumeno wa mkono unatumika kukatia vyuma kwa usahihi zaidi kwa mfano unataka kuunga vyuma viwili tofauti katika degree 90 ili kuweza kuform kona za frame ya dirisha au geti au kitanda n.k utahijika kutumia msumeno ili uweze kukata kwa unyoofu zaidi, kwa kutumia grinder kutokana na mtikisiko wa grinder au umakini wa mkataji utakuta umepindisha na ukipindisha hutaweza kutengeneza Kona ya frame kwa degree 90.
Pia kukata kwa grinder hutoa nyama Nene kwenye Chuma tofauti na msumeno.

Grinder hutumika pale ambapo unataka kukata bati la Chuma(sheet) au Chuma kinene au kukata sheet juu juu pale ambapo unatengeneza ile miinuko/migongo ya geti au mlango.
 
Mkuu Elon Mzebuluni nakushukuru sana ndugu yangu kwa moyo wako wakujitoa kujibu maswali na mahitaji yangu lakini naomba usinichoke nina maswali zaidi

lakini compressor hii huwa inauzwa kiasi gani hyo ndogo ya kuanzia tu inaweza cost kiasi gani mkuu?
Air compressor ndogo ya 2HP/ Lita 24 unaweza kupata kwa TZS 380K ikiwa mpya kabisa.
 
mkuuu asante sana kwa kutochoka kujibu maswali yangu nakushukuru katika hili mkuu Mungu akubariki sana
 
Habari mkuu naomba nikujibu kwa uelewa wangu.
Vifaa vinahitajika

1. Sehemu/frame ya kufanyia kazi.
Hapa ni sehemu pa kufanyia kazi, malipo ya frame hutegeana na sehemu yenyewe.

2. AC Welding machine (stick/arch Welding).
Bei zake zinaanzia TZS 300K Kwa machine ndogo, Nzuri zaidi Ni zile za kusukwa mtaani. Jambo la kuhakikisha tu unapata fundi mzuri wa kusuka welding machine ( Kama uko Mbeya naweza kukuelekeza kwa mafundi wazuri wa usukaji machine)

3.Welding stick.
Hizi Ni stick kwa ajili ya kuchomelea, hua Zina size mbali mbali, Bei yake Ni TZS 15K -17K kwa KG 3.

4.Angle grinder
Hii itatumika kukatia vyuma au kunolea vyuma. Hapa aina/brand zinazopendelewa zaidi ni angle grinder za Makita au Bosch. Bei zake huanzia TZS 350K. Unaponunua kuwa makini kutambua Makita au Bosch original maana copy zimejaa sana.

5. Cutting disk/ grinding disk.
Hizi ni kwa ajili ya kukata au kunoa vyuma. Bei ya reja reja ni TZS 5K kwa cutting disk moja kwa huku nilipo.

Cutting disk za kampuni ya PS FORTE zinazotengenezwa South Africa hudumu Zaidi ,sijajua brand nyingine.

6.Meza ya Chuma.
Hii ni kwa ajili ya kukunjia maua ya mageti au fensi au madirisha. Bati lake la juu liwe angalau ni plate ya 6mm. Miguu yake bomba za Chuma aina black pipe, ziwe na diameter angalau 1-1.5 Inch.

***********************
Nitaendelea.
Umemaliza kila kitu

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Bench Vice ndogo ya KG 7 unaweza kupata mpya maduka ya hardware kwa TZS 100K. Bei zinaweza kubadilika.
KUNA ka video nilikua nakaangalia youtube kuhusu utendaji kazi wa bench vice na hata muonekano wake ukoje nikabahatika kuona bench vice ndogo hyo ya kg 7 na kuna kadogo tena chini ya hapo,ukiangalia hii video utaziona zote mbili mkuu

nina swali mkuu,wakati naangalia hii video kuna vifaa alikua anatumia kupima diameter za chuma sentimeter vifaaa hivi mkuu vinapatikana wapi nikivihitaji maana nimegundua n vya muhimu sana wakati wa utendaji kazi ili kuepuka makosa madogo madogo ambayo yatafanya fundi uonekane hujui unachokifanya.

na hizi vice za kg 7 utofauti wake na hzo vice kubwa ni upi maana kama chuma kinaweza ingia kati kati cha size yyte vice itashndwa kukikamata au kukikaza?

kazi za vice kubwa kubwa ni zipi mkuu?
 
Back
Top Bottom