Mkuu,kwanza kabisa hongera kwa swali zuri sana.Pamoja na kwamba wengi wa wachangiaji wamechukulia swali lako kama mzaa ila mimi nitakupa Jibu serious kabisa kwa faida yako na ya wengine watakaotembelea uzi huu.
Kwanza tuelewe hasa maana ya kujiajiri.Kujiajiri kimsingi ni kuanzisha shughuli za kibiashara au uzalishaji mali ambayo unafanya mwenyewe au kwa kushirikiana na wengine.Hata hivyo kujiajiri hasa ni pale ambapo unafanya shughuli zako wewe mwenyewe na hujaajri watu wengine.Unapoanza kuajiri watu wengine unaingia katika kundi la Mjasiriamali ingawa pia hataka ukiwa umejiajiri unaweza kujiita Mjasiriamali.
Sasa nikirudi kwenye swali lako la msingi kuhusu unavyoweza kujiajiri baada ya kuhitimu.Kama lengo lako ni kujiajiri baada ya kuhitimu basa wakati wa kufanya maandalizi ni sasa.Wakati wa kuanza kujiajiri ni sasa.Ni lazima uanze kujiajiri sasa ili uweze kuelewa changamoto na fursa na pia uweze kutumia mtandao ulio nao kama mwanafunzi.Hata kama lengo lako likiwa ni kuajiriwa ni lazima uanze kujijenga sasa hivi.
Kama ulivyoainisha kwamba unasoma Kozi ya Computer Science katika CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.Sifahamu sana kuhusu Ubora wa Mafunzo katika chuo cha uhasibu ARusha hasa katika fani husika Ila kama ushauri.Fani za Computer zinaweza kuwa rahisi kujiajiri hata unapokuwa Chuo na hata Baada ya kuhitimu kwa kuzingatia yafuatayo:
- Jitazame wewe mwenyew ni mzuri katika maeneo gani ili uongoze mkazo katika maeneo hayo.Katika eneo la IT kuna maeneo kama vile Software Development hasa Mobile Application ambapo wewe unapaswa kuwekeza katika kufahamu software mbalimbali ambazo ni maarufu sokoni na hata zile mpya ili uweze kuanza kwa kuziporomote na kuwapatia watu support.Ni rahisi zaidi kutengeneza kipato kwa kutumia READY made systems wakati ukiendelea kutafuta eneo ambalo unaweza kujikita
- Pili tazama teknoljia zinazobamba uangalie kama unaweza kutengeneza niche yako ambayo unaweza kuitumia kujitofautisha.Hapa kuwa makini kufauatilia teknolojia mpya kama Akili mnembe na mbadiliko mengine ya kiteknolijia yanayoendelea kwani kila teknolojia mpya inakuja na fursa na kila fursa inategemea na uwezo wako wa kuitambua na kuitumia.
Katika ujumla wake ninakushauri uwekeze katika Akaunti ya GOOGLE PLAYSTORE DEVELOPER kwa ajili ya Kuweka Apps kwenye Play store.Unaweza anza kwa kutengeneza Apps ndogo ndogo tu na kuziweka Play store huku ukifanya Maboresho na kuongeza UJUZI wako.
Pili Tafuta namna uwekeze Pia katia server kwa ajili ya kuhost Website yako na websites za wengine na Pia uwekeza katika kujifunza teknoljia mbalimbali kwa ajili ya kutengeneza Websites na Web Apps.Ukianza Sasa hivi itakusaidia kuongeza umahiri katika masomo yako na kujijejengea kujiamini na baada ya khitimu utakuwa na ujasiri wa kuingia katika ulimwengu wa kujiajri na ujasiriamali ukiwa na Ujasiri.
Ninakutakia Kila la heri