Ushauri wa Profesa Janabi kuhusu krismas, kuleni kwa kuzingatia afya, msile kupitiliza

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
“Watu wanaenda Krismasi na nyie wote mlioko hapa mnaenda Krismasi, wapo wa Moshi, wapo wa Arusha, wapo wa Mbeya, wapo wa Iringa na wengine Songea nyumbani kwetu, ulaji utakuwa wa kupitiliza, ulaji wa nyama utaongezeka, vinywaji vya kupitiliza kila kitu kitakuwa cha kupitiliza , wapo ambao wakirudi Januari wanaweza kurudi sawa kwa lugha za waandishi kurest lakini salamu zangu za Krismasi kuzingatia ulaji.”

Prof. Mohamed Janabi

Screenshot 2024-12-12 114909.png
 
Wale jamaa zangu wa kule mkoani wanapenda kula sana msimu huu wa sikukuu. Unakuta kijana mdogo ana kitambi, je akifikisha miaka 50 itakuaje? Hapo yale magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa kilafi yatakuwa yanatamalaki mwilini mwake, kutoboa miaka 70 ni shughuli pevu
 
“Watu wanaenda Krismasi na nyie wote mlioko hapa mnaenda Krismasi, wapo wa Moshi, wapo wa Arusha, wapo wa Mbeya, wapo wa Iringa na wengine Songea nyumbani kwetu, ulaji utakuwa wa kupitiliza, ulaji wa nyama utaongezeka, vinywaji vya kupitiliza kila kitu kitakuwa cha kupitiliza , wapo ambao wakirudi Januari wanaweza kurudi sawa kwa lugha za waandishi kurest lakini salamu zangu za Krismasi kuzingatia ulaji.”

Prof. Mohamed Janabi

View attachment 3175090
Toka lini mlo wa mara moja kwa mwaka ukawa ni mjadala. Tutakula, tutakunywa hadi kusaza. Kesho yake tunaingia shambani kulima matuta ya viazi🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kila mtu na afanye aonavyo ni sahihi kwake, mbuzi zichomwe, ka mbege, na machalari niache kula kisa utaratibu wake, Tena issue yenyw siku kadhaa au wiki tuu.......

Ila siku hz nimeacha kula vitu vingi nisaidieni ndugu zanguni nirudi kwenye ufakamiaji

secretarybird nipe dawa siku hz vyakula vingi sili mpaka mama anasema khaa ni wewe au 😂

Nikienda ugenini naona kuwapa watu taabu ya kuwaambia sitaki msosi
 
Professor Anatukosea Sana Tanzania
Acha Tule Tu Maana Milo Mitatu Adimu Sana
 
Kila mtu na afanye aonavyo ni sahihi kwake, mbuzi zichomwe, ka mbege, na machalari niache kula kisa utaratibu wake, Tena issue yenyw siku kadhaa au wiki tuu.......

Ila siku hz nimeacha kula vitu vingi nisaidieni ndugu zanguni nirudi kwenye ufakamiaji

secretarybird nipe dawa siku hz vyakula vingi sili mpaka mama anasema khaa ni wewe au 😂

Nikienda ugenini naona kuwapa watu taabu ya kuwaambia sitaki msosi
Tumtafute yule mchungaji wa Kenya aitwaye Mackenzie atupige mfungo then tukipigwa na njaa hamu ya msosi itarudi.
 
Huyo Propesa anachoweza ni kudunga wenzie sindano. Kwani miaka yote huwa anatushauri yeye?
 
Huu ushauri akiupeleka kule WHO tutakosa Kura kabisa , muelezeni madawa ya hayo magonjwa ni biashara za mabepari ndio maana hawajaweka preventive measures
 
Sio lazima wote tufate kanuni za ulaji, nyie madokta mnatosha kutuwakilisha.
 
Toka lini mlo wa mara moja kwa mwaka ukawa ni mjadala. Tutakula, tutakunywa hadi kusaza. Kesho yake tunaingia shambani kulima matuta ya viazi🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Huyu dingi wakati mwingine anazingua sana.
 
Back
Top Bottom