Ushauri wa talaka kwa wanawake ............

mbona nahisi kama uvumilivu wangu ulizaa matunda
au hiyo pia haijalishi

Gaga....kila ndoa inahitaji uvumilivu, hata mie nilivumilia ikazaa matunda, nadhani Boss anaongelea ile kudhalilishwa /mapenzi yameisha/vituko vyote bado unavumilia tu, na wengi we2 2navumilia coz ya jamii, jamii itasema/nitaonekanaje etc...kweli mie naheshimu talaka kwenye suala la kuwa na amani...mama alivyo2somba baada ya miezi kadhaa mwili ulianza kurudi sasa, aliisha kila akifikiria leo mume wake anakuja na ki2ko gani hapati ucngizi.....kwa kweli 2liishi maisha na mama ya raha sana sana, tena 2liridhika na ndizi chukuchuku kuliko yale maisha na baba....divorce ina uzuri wake kwa upande wa pili wa shs.
 
wanabakwa na kutukanwa daily....
au mwanaume anahamia kwa kimada
na kukaa miezi auu mwaka..
na wewe unavumilia eti atarudi tu....
ujinga huo ndo nauzungumzia hapa....

Lakini pia tajiriba binafsi zinahusika katika msimamo mtu anaochukua

Wakati mwengine mtu role model wake ni baba yake kwa mfano, kwa hiyo anachukia kuwa mama yake alidai talaka akamkimbia baba yake japo kuwa alikuwa na vituko (labda ana wanawake anabadilisha kila siku).

Kwa hiyo na yeye anakuwa anamvumilia mwanamme (mume wake) afanye vituko as long as ni sawa na alivyokuwa anafanya baba yake. (Akikiri kuwa vituko vya mume havivumiliki na ni ushenzi, vitavunja mtizamo wake kwa baba yake)

Pili kwa vile yeye alichukia mama yake alipoondoka kwa baba yake, nae anaogopa kuwa labda watoto wake watamchukia, kwa hiyo anashindwa kudai talaka

Na wale ambao role models wao ni mama zao, na mama zao walivumilia kila aina ya kipondo, wao hutafsiri kuwa yale ni mapenzi ya kweli, kwa hiyo na wao wanastahamili adhabu zote wakiamini ni mapenzi ya kweli kama waliyokuwa nayo mama zao.
 
wanabakwa na kutukanwa daily....
au mwanaume anahamia kwa kimada
na kukaa miezi auu mwaka..
na wewe unavumilia eti atarudi tu....
ujinga huo ndo nauzungumzia hapa....
Hapo nimekwelewa, kuna mateso mengine hayavumiliki kabisa, ndio maana siku zote nasema navumilia mengi ila kipigo naona sitaweza kabisa, au jamaa anahama mie namsubiria
 


Wewe ni mwalimu kweli Gee.....
ndo maana nikasema wanahitaji kuwa na knowledge na ueelewa
wa madhara ya kisaikolojia ya 'ndoa mbovu'.....
na kujadili kama hivi ni one step ya kuelekea huko....
sasa wao hata kujadili tu kwao ni ishu....
 
Kuna vitu Boss una mix hapa.

Maisha ya ndoa ni ku dance according to the tune.

Wewe unataka kila mwanamke/msichana achangie huu uzi.

Lakini nakwambia kuchangia ni one thing kutenda ni another.

Hao wanaosema wana support divorce 100% unaweza kuta ndio hawaachiki ng'o no matter what.

Ni ngumu ku predict future; ni very situational na watu tuna tofautiana. Ndio maana kuna watu labda wanaona haina maana kuzungumzia matatizo ambayo hawana; that can even affect their health relationships. Divorce si kitu cha kushadadia wakati huko kwenye ndoa yenye neema. Speaking of a ghost....

Waweza kuta wale wanaodai talaka hawana hata sababu za msingi; kuna dada namjua aliomba talaka kwa kuwa mume kafulia na wao kwao mambo safi hawezi ishi kwenye shida.

No matter how well we will discuss this it wont change maamuzi ya mtu.

Ni wrong ku praize wale wanao dare kudai talaka au kubeza wavumilivu. Kila mtu ana way ya ku reason jinsi ya ku solve matatizo ya ndoa yake.

kila kitu ni wewe na principle zako
kama kwako ku cheat sio ishu,ni poa tu...
but mimi nazungumzia zaidi ndoa ambayo
'imeshakufa' lakini mwanamke hataki talaka
sisemi makosa yasisamehewe....nasema ni kuwa
umechoka na ndoa lakini unavumilia...why?
 


niliposema kujadili sikumaanisha sana uzi huu
nilimaanisha aliyoyasema NN kuhusu uzi uliowahi kuletwa na Mwanakijiji kuhusu
sheria za talaka....na zaidi namaanisha ile culture ya 'kutotaka kuitazama talaka'
kama one of the choices na options za 'ndoa mbovu'
kuhusu uzi huu nafurahi wanawake mliojitokeza kuchangia
thanx.....nyote....
 
mimi kinachonishangaza ni woga wa hata kujadili....
yaani hapo nabaki mdomo wazi....kujadili tu woga
je kutenda?????

mkuu suala la mjadala ni gumu sana kwetu , kwani hata katika hali ya kawaida watu hawana utamaduni wa kujadili jambo hadi kufikia mwafaka bali wengi hupenda kutoa maamuzi kwa kuamini wako sahihi
 
Ukitaka kuachika Boss unasomba kilicho chako unasepa; I have seen that in most cases.

Kwa Bongo ni very rare kusikia mwanamke aliyeamua kuwa ndoa yangu sasa basi anaulizia sheria inasemaje.

Hayo mambo ya sheria yanafuata baadae sana baada ya some years; lakini sheria haimzuii mtu ku step out of her house.

My mum alienda mahakamani baada ya 5 years ya kusepa kienyeji.

Na ni ndugu zangu ndio walimshauri kwa kuwa waliona kuwa if dad ataoa mwanamke mwingine jasho la mama litapotea.
 


Sio lazima mtu awe na tatizo ndio alijadili. Kama ilivyokuwa kuwa ukiwa kwenye perfect health ndio wakati mzuri wa kujadili UKIMWI na VVU ni hivyo hivyo kwa masuala ya ndoa. Tunajadili options zilizopo katika ndoa mbovu na pia tunajadili sababu za kumfanya mtu aendelee kubaki kwenye ndoa hizo. Hiyo ya sijui "speaking of the devil ......." sidhani kama ina nafasi kwenye masuala kama haya

Naamini suala kama hili linapojadiliwa linaweza hata kuwapa moyo wale waliopo kwenye ndoa za mateso kuwa si lazima kuvumilia, na wapo watu watakao waelewa iwapo wataamua kutalikiana
 
Habari zenu wan jamvi
Jamani mimi ni muislam na kwa perspective ya uislam ,talaha ni halali ambayo allah /mungu anaichukia
Ni halali kwa sababu kuna wakati ndoa inakuwa ngumu saaaana na inaweza leta madhara makubwa kwa wana ndoa na watoto na hata vifo ,kwa nini ifikie hivi wakati ndoa ni muungano wa hiari unatarajiwa kuleta mapenzi na kujenga badala ya kubomoa jamii na kusababaisha chuki zisizoisha?
HUWA TUNAAMBIWA WAKATI WA KUFUNGA NDOA - OWANENI KWA WEMA NA MKISHINDWA KABISA NA IKIBIDI KUACHANA BASI MUACHANE KWA WEMA ,MSILETE MADHARA KWA WATOTO NA JAMII JUU YA KUACHANA KWENU
hIVYO Ieleweke kuwa talaka ni last option kunusuru wanandoa na jamii kwa ujumla

KWA NINI ALLAH ANACHUKIA TALAKA INGAWA AMEHALALISHA
Ni kwa kuwa inaleta utengano wa familia ,baba mama na watoto na inavunja undugu baina ya pande mbili ambazo ndoa iliunganiahsha
Mara nyingi ndoa hazivunjwi kwa wema kunakuwa na maugomvi na msambaratiko hasa ktk jamii na utulivu na amani vyaweza kupotea kabisa

Kwa hiyo basi kuna sababu za msingi zikitokea mume anaweza mpa talaka mke wake na pia kuna sababu za msingi zinazomruhusu mke kudai kuvunja ndoa
Hana amani na mumewe anapigwa na kunyanyaswa na mume hajirekebishi ,hapatiwi mahitaji yake na watoto ,kuyimwa unyumba na kutofikizwa hukoooooooo kunakotajwa,hata kama mume ni mgonjwa kama mke akisema yy hawezi vumilia asije akazini basi ana haki ya kudai talaka kama ugonjwa ni zaidi ya mwaka ,sembuse ukimwi!!!!!!!
Suala la mali linaangaliwa kam ifuatavyo
jE MALI NI UBIA kAMA NDIO INABIDI MGAWANE kufuatana na ubia wenu kama ni ya mke atachukua mke na kama ni ya mume atachukua mume ,mume pia anajukumu la kumpa KITOKAUNYUMBA MKE WAKE ILI APATE CHA KUANZIA MAISHA ,HASA KAMA MKE HANA MALI

WATOTO
Je wapo chini ya umri wa miaka 7.-wanabaki na mama ila baba anatakiwa atoe matunzo kufuatana na hali
Watoto wakubwa wanaweza kaa na baba .lakini pia wanahaki ya kuchagua kukaa na nani
Haifai kumkataza mtoto kwenda kwa mzazi yeyote

Hayo ni kwa ufupi
NDOA IKIWA NGUMU SINGANAGNII ILA SIWEZI KUVUNJA NDOA BILA SABABU ZA MSINGI NI DHAMBI MAANA WENGI WANAFANYA MCHEZO NA HII RUHUSA YA KUVUNJA NDOA
jitahidi kutafuta suluhu kwanza kwa kushirikisha wazazi na wazee wa pande mbili kama kwleli manapendandana bado na mungu atasaidia kuikoa ndoa ikishindikana basi huenda mungu atakupa mwingine alie bora kuliko kufia hapo

wanabakwa na kutukanwa daily....
au mwanaume anahamia kwa kimada
na kukaa miezi auu mwaka..
na wewe unavumilia eti atarudi tu....
ujinga huo ndo nauzungumzia hapa....
 

exactly.....kusema watu wakichoka tu waondoke
hakuna sheria za kutosha bongo,hakuhalalishi
culture ya kuvumilia 'ndoa za mateso'
na vizuri watu wajadili hata kabla hawajaingia kwenye hizo 'ndoa'
 
Hili sredi lilitoka hewani lini?

Khaa! Yaani na ujanja wangu wote nalikuta limekaribia level ya kuchakachuliwa?

Anyway, kwakuwa mie si muumini wa talaka ngoja nifanye kazi ya kuwagongea watu ma-Likes ya kufa n'tu!
 
exactly.....kusema watu wakichoka tu waondoke
hakuna sheria za kutosha bongo,hakuhalalishi
culture ya kuvumilia 'ndoa za mateso'
na vizuri watu wajadili hata kabla hawajaingia kwenye hizo 'ndoa'

Na hata kama watu wanafanya kienyeji na kuondoka tu, hiyo ilikuwa kipindi hicho.

Sasa kwa mfano mwanamke wewe ndo pesa yako imetumika kujenga nyumba mnayokaa, na watoto wewe ndio unalipia shule, lakini uondoke kimya kimya?

Ni muhimu kwa suala zima la sheria kuwekwa wazi ili wanawake (na wanaume) wajue haki yao wanaipata vipi.
 
Unadhani ni busara kujadili matatizo ya ndoa before marriage; What for? get prepared?
exactly.....kusema watu wakichoka tu waondoke
hakuna sheria za kutosha bongo,hakuhalalishi
culture ya kuvumilia 'ndoa za mateso'
na vizuri watu wajadili hata kabla hawajaingia kwenye hizo 'ndoa'
 
Kwa mtazamo huo ili kurahisisha kazi ya kuachana basi wanandoa wa jinsi hiyo kila mtu awekeze kivyake; gari yangu; nyumba yangu; only that is shared ni watoto wetu.

Maana naona mali ndio zawaweka watu roho juu.

oooh yeah :]
 
Unadhani ni busara kujadili matatizo ya ndoa before marriage; What for? get prepared?

ni busara na ni recommended world wide
Any information is useful hata kama hiyo inormation hauhitaji kwa wakati huo.....
ndo maana tunajua ukipatwa na msiba umuone nani kwa mazishi,sanduku,kaburi
hata kama hauna mgonjwa......ndoa is no exceptional......
 
Kun member Magazeti ameuliza suala hili kwenye jukwaa la sheria.


Vitu hivi ni muhimu kujua kabla hamjaoana
 
Kwa mtazamo huo ili kurahisisha kazi ya kuachana basi wanandoa wa jinsi hiyo kila mtu awekeze kivyake; gari yangu; nyumba yangu; only that is shared ni watoto wetu.

Maana naona mali ndio zawaweka watu roho juu.

ishu sio mali
ishu ni kuepusha 'watu kutofikia maamuzi'
wanapokuwa kwenye mgogoro na hawawezi kuzungumza tena
umewahi kusikia kitu kinaitwa 'PRE NUPTIAL AGREEMENT ..??????
 
Kwa mtazamo huo ili kurahisisha kazi ya kuachana basi wanandoa wa jinsi hiyo kila mtu awekeze kivyake; gari yangu; nyumba yangu; only that is shared ni watoto wetu.

Maana naona mali ndio zawaweka watu roho juu.



Hivi kuingia kwenye ndoa ndio kunaniondoshea uhalali wa kuwa na Mali zangu mimi mwenyewe?

Kwa mfano nimeachiwa urithi mali nyingi sana mzazi alipofariki wakati nipo kwenye ndoa tayari. Ile mali unaihesabuje? Yetu mimi na mume au yangu mke?

Mfano mwengine mimi nna biashara yangu, inalipa pesa za kutosha, unaihesabuje hiyo kampuni? Yangu au ya mume? a

In my opinion there is nothing wrong kwa wana ndoa kuwekeza kivyao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…