Habari zenu wan jamvi
Jamani mimi ni muislam na kwa perspective ya uislam ,talaha ni halali ambayo allah /mungu anaichukia
Ni halali kwa sababu kuna wakati ndoa inakuwa ngumu saaaana na inaweza leta madhara makubwa kwa wana ndoa na watoto na hata vifo ,kwa nini ifikie hivi wakati ndoa ni muungano wa hiari unatarajiwa kuleta mapenzi na kujenga badala ya kubomoa jamii na kusababaisha chuki zisizoisha?
HUWA TUNAAMBIWA WAKATI WA KUFUNGA NDOA - OWANENI KWA WEMA NA MKISHINDWA KABISA NA IKIBIDI KUACHANA BASI MUACHANE KWA WEMA ,MSILETE MADHARA KWA WATOTO NA JAMII JUU YA KUACHANA KWENU
hIVYO Ieleweke kuwa talaka ni last option kunusuru wanandoa na jamii kwa ujumla
KWA NINI ALLAH ANACHUKIA TALAKA INGAWA AMEHALALISHA
Ni kwa kuwa inaleta utengano wa familia ,baba mama na watoto na inavunja undugu baina ya pande mbili ambazo ndoa iliunganiahsha
Mara nyingi ndoa hazivunjwi kwa wema kunakuwa na maugomvi na msambaratiko hasa ktk jamii na utulivu na amani vyaweza kupotea kabisa
Kwa hiyo basi kuna sababu za msingi zikitokea mume anaweza mpa talaka mke wake na pia kuna sababu za msingi zinazomruhusu mke kudai kuvunja ndoa
Hana amani na mumewe anapigwa na kunyanyaswa na mume hajirekebishi ,hapatiwi mahitaji yake na watoto ,kuyimwa unyumba na kutofikizwa hukoooooooo kunakotajwa,hata kama mume ni mgonjwa kama mke akisema yy hawezi vumilia asije akazini basi ana haki ya kudai talaka kama ugonjwa ni zaidi ya mwaka ,sembuse ukimwi!!!!!!!
Suala la mali linaangaliwa kam ifuatavyo
jE MALI NI UBIA kAMA NDIO INABIDI MGAWANE kufuatana na ubia wenu kama ni ya mke atachukua mke na kama ni ya mume atachukua mume ,mume pia anajukumu la kumpa KITOKAUNYUMBA MKE WAKE ILI APATE CHA KUANZIA MAISHA ,HASA KAMA MKE HANA MALI
WATOTO
Je wapo chini ya umri wa miaka 7.-wanabaki na mama ila baba anatakiwa atoe matunzo kufuatana na hali
Watoto wakubwa wanaweza kaa na baba .lakini pia wanahaki ya kuchagua kukaa na nani
Haifai kumkataza mtoto kwenda kwa mzazi yeyote
Hayo ni kwa ufupi
NDOA IKIWA NGUMU SINGANAGNII ILA SIWEZI KUVUNJA NDOA BILA SABABU ZA MSINGI NI DHAMBI MAANA WENGI WANAFANYA MCHEZO NA HII RUHUSA YA KUVUNJA NDOA
jitahidi kutafuta suluhu kwanza kwa kushirikisha wazazi na wazee wa pande mbili kama kwleli manapendandana bado na mungu atasaidia kuikoa ndoa ikishindikana basi huenda mungu atakupa mwingine alie bora kuliko kufia hapo
wanabakwa na kutukanwa daily....
au mwanaume anahamia kwa kimada
na kukaa miezi auu mwaka..
na wewe unavumilia eti atarudi tu....
ujinga huo ndo nauzungumzia hapa....