Ushauri wa Vijana unatishia usalama wa maamuzi yako

Ushauri wa Vijana unatishia usalama wa maamuzi yako

Anonymous77

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2022
Posts
589
Reaction score
1,515
Siku za hivi karibuni ndio nimeelewa ile kauli ya "heshimu wazee" watu wengi wamekuwa wakitusisitiza vijana kuheshimu wazee na kuwaomba ushauri wazee na wale waliokuzidi umri sababu mara waliopitia mengi na wenye matatizo mengi ndio wenye ushauri mzuri.

Lakini vile vile nimekumbuka ile kauli ya "ujana maji ya moto" sisi vijana tunapopeana ushauri hasa unapokuta unamuomba ushauri kijana wa rika lako, huwa tunapeana ushauri fulani hivyo high risk, risk.. usipokuwa makini jera hii hapa inakuita.

Japo sio kila mzee ana busara hata machizi nao huzeeka kuwa makini na watu wa kuwaomba ushauri hasa wale wa rika lako maana jera inakuita muda sio mrefu.

Hebu tuambie kidogo ni ushauri gani uliwai kupewa na kijana mwenzio mpaka leo unajutia.
 
"Acha kuhangaikia uchi Muda unaopoteza haupotei unapotea wewe" -- Lloyd Sr.
 
Ila kuna situation nyingine unahitaji ushauri wa vijana ule hard core, mchungu utakasirika lakini unakupa adrenalin ya kuchukua maamuzi,kuliko ushauri laini wenye busara
 
Ukipewa ushauri na mtu yoyote iwe mzee, kijana au mdogo kwako usiufanyie kazi hapo hapo. Ufanyie kazi baada ya siku mbili. Kama ni swala la dharura sana fanyia kazi mtazamo wako juu ya hilo swala (usiwe muoga)
 
Back
Top Bottom