Safi sana mkuu kwa kupata wazo la kujiajiri mwenyewe.
Mawazo ya biashara yapo mengi sana lakini siyo yote yatakufaa wewe..
Biashara yoyote ili ifanikiwe inabidi ufanye biashara unayoijua na unayoipenda. Kwa nini nasema hivyo? Ukifanya biashara ambayo hauijui undani wake , inafanyikaje, risk zake itakubidi uwe na hela za kutosha ili uajiri manager atakaye manage kila kitu. Ambapo kwa mtaji wako wa 2M ni ngumu sana.
Ngoja nikupe mfano, hauwezi kufanya biashara ya kuuza nguo kama wewe haupendi mambo ya nguo au mambo ya fasheni. Kwa sababu utajikuta unauza nguo za mwaka 2000 huko na wakati zilishapitwa na wakati sasa hivi ni 2019. Inatakiwa iwe ni kitu unachokipenda hata swaga mpya ikiingia mjini ujue kabisa.
Ngoja nijitolee mimi kama mfano, tangu nikiwa mdogo shuleni nilikuwa napenda sana kusuka watu nywele, nilivyofika secondary kazi ikaendelea kusuka watu maana tulikuwa tunaruhusiwa kusuka. Nilivyofika chuo kikuu sikupata mkopo na niliwaza ni biashara gani ambayo naweza kuifanya nikiwa chuoni huku nasoma pia. Nilishauriwa mambo mengi ya kufanya , wengine wakanishauri hadi kwenye kilimo. Guess what.. Kila biashara niliyofanya ilifeli kabisa ndipo nikagundua nilikuwa najihusisha na vitu ambavyo sivijui na ikapelekea kufanya vibaya.
Akili ilinirudia kwamba Mimi ni Msusi, najua kusuka najua kupamba kumbi za ibada , sherehe nk. Ndipo nikagundua kwamba biashara ya kuuza urembo wa wakina Dada, nywele , lipstick nk hiyo ndiyo itanifaa. Nitauza rasta na pia nitazitumia hizo hizo kusuka wateja watakaokuja kusuka.
Mpaka namaliza chuo mwaka wa tatu tayari nilishafanikiwa kufungua saloon yangu mwenyewe na nikaajiri wafanyakazi. Nimejaribu kujiingiza kwenye biashara nyingine zinafeli feli tuu na kunitia hasara. Mpaka sasa nimeamua nijikite hapo hapo kwa sababu ndiyo biashara pekee ninayoijua vizuri, ninayoipenda na inayofanya vizuri. Na biashara inafanya vizuri na pamoja na kwamba nimeajiriwa ila biashara hiyo ndiyo inanipa jeuri mjini. Naipenda sana na kila siku lazima nigoogle kujua mtindo mpya ulioingia nk.
Hivyo mkuu usiangalie tuu ni wazo gani la biashara, jiangalie wewe jee ni kitu gani unakipenda? Unakijua? Na utaweza kukifanya vizuri na ukifurahia kabisa. Hapo lazima ufanikiwe.
Kama unacho kitu au vitu unavyovipenda, au hata kama unapenda kulima sema ili tujue tunakupa wazo lililo base kwenye mambo hayo.