Ushauri wana JF: Milioni 25 itatosha kumalizia nyumba yenye sifa hizi?

Ushauri wana JF: Milioni 25 itatosha kumalizia nyumba yenye sifa hizi?

Hapo mkubwa ndio kwenye ujenzi, hapo ndipo utakapogombana na mafundi kama haujengi kwa contracting. Fedha utaona inaenda nyingi lakini kilifanyika kama hukioni. Kwa hio 25m naweza kusema inatosha au haitoshi, kwani kila ulichokitaja hapo kina standard yake na mafundi wa namna tofauti, Gypsum ziko tofauti, vifaa vya umeme, maji pia tofauti; kwahiyo kama una muda tafuta fundi akupe mahitaji ya kila kitu halafu pitapita madukani kufanya utafiti mwenyewe. Kama utataka nyumba ya finishing yenye kuonekana mtaani, inabidi uwe na 35-40m, ila kama unataka nyumba ya kawaida (ya kati kwa kati), unaweza kwenda nayo vizuri hiyo hela. Au kama vipi jenga kwa awam ya kukuwezesha kuhamia then utapamba mdogomdogo
 
Duuuh! Mkuu king kong III vipi tena, haya niunganishe basi nikamkope (ila kulipa mpaka matanga)

Haina Haja ya kukopa JF likija swala nyumba wanaweka bei za hajabu ambazo wao wamepigwa ebu fikiria kuna mdada humu ramani ya nyumba tu alichorewa kwa 2.5m! Kiukweli hyo fedha inatosha na chenji inabaki siwezi nikaweka mambo yote hapa ila inatosha! Ulishawah kufikiria kench za mnazi? Zinaponguza gharama karibia 65% ingekuwa kazi yangu hyo juu ningetumia 2m,milango ningeagiza mkoa yote ningeweza kusave 30% madirisha ninge order china mwenyewe ningesave 40% katika hyo 25m ningebakiwa na 10m
 
Mbuzi huwa kwa urefu wa Kamba yake.

Hayo mahesabu mie sikubalianoi nayo,maana wengine wameandika hadi ziungu kuchangaya tu.

Pesa inatosha kwa hali zetu,naka we unaona ndogo basi kaanayo uone kama baada ya muda utabaki na pesa,pesa sheatni inaweza kuzuka shida hata ujui imeenda watu,na marafiki au ndugu wakijua unapesa mra inaingia kwenye mipango minhyine unabaki ningejua.

Hao Jamaa hapo juu wanakupoteza.

Kwa nyumba ilipofikia ni kwamba hiyo 25M inatosha sana kibongobongo.Ila ukitaka uhamie kama vile VIP,hata milioni 100 utaambiwa haitoshi hapa.

Weka bati,milango,madirisha,na chini weka cement floor ya kawaida tu,ukipata pesa utabailisha,juu weka ceiling board la kawaida,ukipata pesa utabadilisha.Then hamia.
 
Shukurani. Idadi ya milango iko nadhani 12 au 11 hivi

Sasa kwa milango 11 alafu mbao ya mninga. Itaweza kukugharimu si chini ya mil 6 mpaka 10. Lakini ungeweza kupunguza matumizi kwa kuweka milango ya aliminium ndani na nje kuweka mlango wa mbao
 
Hazitoshi kwa haraka tu....
Bati sio chini ya 7m, mbao 5m, milango 3.5m (frem+mlango+vitasa), tiles 2m, aluminium 4m, bado umeme, rangi, makabati, tiles, plast, rangi, gypsum etc

Nakubaliana na wewe kabisa. Hiyo hela labda inatosha 2/3 au 3/4. Asisahau kuna gutters, kuna kumlipa fundi, usafiri, misumari, na korokoro nyingi tu.

But, you can do it! Cut somewhere else to fill the gap.
 
Ukifikia kwenye mbao na bati hapo nicheki kwenye no. 0762525846,kiwaleisaya@gmail.com,www.kiwalepromo.blogspot.com. hizo ndio kazi zangu mkuu.nitakuletea mpaka uwanjani kwako bureeee

Asante mkuu kwa kuongeza nia, lakini unaonaje japo ukitoa "general overview" ya bei zako ili wana JF wengi tunufaike na tumiminike kwako. Yaan kwa wastan ft moja ya bati kiasi gani na mbao vilevile kwa saizi zote kama ni 2x2, 2x4 na 2x6. Otherwise, shukurani sana
 
Sasa kwa milango 11 alafu mbao ya mninga. Itaweza kukugharimu si chini ya mil 6 mpaka 10. Lakini ungeweza kupunguza matumizi kwa kuweka milango ya aliminium ndani na nje kuweka mlango wa mbao
Ni ushauri mzuri huu mkuu, na kwa kuwa mwanzo siku naujua lakini nitaufanyia kazi kikamilifu. Kwa hiyo hoja yako ni kwamba milango ya Aluminium ni rahisi sana kuliko ya mbao siyo, je waweza jua mlango mmoja waweza kadiriwa kiasi gani. Otherwise shukrani sana, bila shaka JF jukwaa la kipekee kwa ushauri kwa sisi vijana wanyonge
 
Haina Haja ya kukopa JF likija swala nyumba wanaweka bei za hajabu ambazo wao wamepigwa ebu fikiria kuna mdada humu ramani ya nyumba tu alichorewa kwa 2.5m! Kiukweli hyo fedha inatosha na chenji inabaki siwezi nikaweka mambo yote hapa ila inatosha! Ulishawah kufikiria kench za mnazi? Zinaponguza gharama karibia 65% ingekuwa kazi yangu hyo juu ningetumia 2m,milango ningeagiza mkoa yote ningeweza kusave 30% madirisha ninge order china mwenyewe ningesave 40% katika hyo 25m ningebakiwa na 10m
Ooooooookey, nimekupata sana bwana King Kong III, ni kweli kabisa wako watu huwa wanapenda kushindana na level ya binaadamu. Umekuja na idea pana sana ya kufikiria maisha halisi badala ya kutaka maisha kama watu wa Kuwait. Nadhani huu ndio ugonjwa wetu watanzania kama siyo dunia nzima. Ila mbao za mnazi mhh? Hiyo nyumba itaishi kwa miaka mingapi kwa mbao hizo?
 
Hizo hela kwanini usimpelekee mzee wa upako kama sadaka halafu atakwombea kwa yesu utaenda peponi,unaonaje mkuu?
 
Si lazima utumie milango ya alminium lakini unaweza kutafuta hata haina nyingine ya milango ambayo itakuwa ni imara zaidi na nafuu kaka. Maana siku hizi kila wakati teknolojia inabadilika
 
Ooooooookey, nimekupata sana bwana King Kong III, ni kweli kabisa wako watu huwa wanapenda kushindana na level ya binaadamu. Umekuja na idea pana sana ya kufikiria maisha halisi badala ya kutaka maisha kama watu wa Kuwait. Nadhani huu ndio ugonjwa wetu watanzania kama siyo dunia nzima. Ila mbao za mnazi mhh? Hiyo nyumba itaishi kwa miaka mingapi kwa mbao hizo?

Mkubwa mbao za mnazi miaka 100 na kuendelea cha msingi ni kuchagua uliokamaa,ushawahi kwenda saba saba banda la JKT? vitanda vyao vyote ni vya minazi.
 
Ukweli mchungu ila haitoshi mkuu

approximately

Bati 3m + fundi
mbao kench 1.2 + fundi
Blandering laki 5 + fundi
Madirisha 1.5 laki@
Mniga frame 80 thou@
Top 130@+hinges+locksets+stoppers+finishing materials(sanding seal,wod glue&polish)+ufundi
Gypsum board 12500@pc + Mikanda 3500@+ corners 4000@+ powder 16500/bag+ scrws+ fiber tapes+ufundi
Tiles kujenga 3000/sqm+cement 25bags@16000+tiles granite /unpolished+scating20000@box+ grout
umeme kuna wiring na fittings+ufundi+service line
maji kuna plumbing+furniture + sewerage+ufundi
Ukuta kuna skimming na rangi yenyewe+white cemnt/G-powder+ufundi
Makabati ya jikoni kunambao+marble/tiles+ufundi

Mkuu andaa hiyo na contingency (20-30%) just in case

Really umenisaidia na mimi, thanx for this
 
Really umenisaidia na mimi, thanx for this

Pamoja mkuu,tujitahidini ili watoto wetu waje kuwa proud na nyumbani kwao na sisi wazazi wao

Kuna vitu tulisahau pale
Plastering;mchanga ,cement +fundi
madirisha;metal grills
Fisherboard+ pvc strips
Nails;Roofing and wood nail

iIle contingency ndo huwa inamegwa na vitu kama hivi due to oversights,sasa imagine ndo tenda umepeleka quotation na umewin halafu unakuta kuna such a serious omission!!!!
 
Haina Haja ya kukopa JF likija swala nyumba wanaweka bei za hajabu ambazo wao wamepigwa ebu fikiria kuna mdada humu ramani ya nyumba tu alichorewa kwa 2.5m! Kiukweli hyo fedha inatosha na chenji inabaki siwezi nikaweka mambo yote hapa ila inatosha! Ulishawah kufikiria kench za mnazi? Zinaponguza gharama karibia 65% ingekuwa kazi yangu hyo juu ningetumia 2m,milango ningeagiza mkoa yote ningeweza kusave 30% madirisha ninge order china mwenyewe ningesave 40% katika hyo 25m ningebakiwa na 10m

Du kwa kunena ni rahisi sana hebu ingia kwenye zoezi lenyewe hiyo millioni 10 utakuta imeishia kwenye bati
 
Back
Top Bottom