#COVID19 Ushauri Wangu Kuhusu Miradi Inayojengwa na Msaada wa Fedha za COVID-19

#COVID19 Ushauri Wangu Kuhusu Miradi Inayojengwa na Msaada wa Fedha za COVID-19

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Nimekuwa nikiona kupitia luninga jinsi viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa na hata Taifa wanavyohangaika na kukamilishwa kwa miradi hii. Walipewa agizo kuwa miradi hii iwe imemalizika katika muda wa miezi mitatu.

Mimi binafsi natofautiana na agizo hili. Kwa Mhandisi anayejua maana ya ujenzi huwezi kukamilisha jengo kwa muda wa miezi mitatu. Unapojenga msingi kwanza kunatakiwa kuwe na maandalizi na hii inaweza kuchukua hata mwezi mmoja ukichukulia kuwa lazima msingi umwagiliwe maji na uwe imara.

Kujenga Boma nayo hivyo hivyo na unapokuja kumaliza mpaka plasta huwezi ukamaliza jengo kwa miezi mitatu. Ujenzi unaoendelea ni ulipuaji wa hali ya juu na baadaye tutakuja kujuta. Leo nimesoma kwenye Jamii forums kuwa Mkuu wa Mkoa fulani ametoa masaa 48 kumaliza majengo 452.

Je hii inawezekana? Tuwe wakweli tuna haraka gani? Tutekeleze miradi hii polepole na kipaumbele uwe ni UIMARA(quality).
 
Ni sahihi mawazo yako. Spidi ya ujenzi vile vile inategemea vifaa vyako vya utendaji mfano aina ya simenti, aina ya zege, shindilia, nondo nk. Haya majengo kama yatafuata viwango vilivyowekwa ni sahihi sana. Mafundi wako wengi na vibarua wao wakipewa malengo wanamaliza. Angalizo viwango na masharti kuzingatiwa otherwise zitatatitia
 
Back
Top Bottom